HATIMAYE wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya soka ya Kombe la Shirikisho, Yanga wamemaliza hatua ya makundi kwa kupokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa TP Mazembe ya DRC.
Mechi hiyo ya mwisho ya kundi A, ambayo ilikuwa ya kukamilisha ratiba kwa Yanga, ilichezwa jana kwenye Uwanja wa Mazembe ulioko katika mji wa Lubumbashi.
Kutokana na matokeo hayo, TP Mazembe imemaliza mechi za kundi hilo ikiwa ya kwanza, kwa kuwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi sita, wakati Yanga imeshika mkia kwa kuambulia pointi nne.
Yanga ililazimika kumaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki wake, Andrew Vincent Chikupe, kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 30.
Mazembe ilihesabu bao lake la kwanza dakika ya 28 kupitia kwa Jonathan Bolingi baada ya kupokea pasi maridhawa kutoka kwa Deo Kanda.Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Ranford Kalaba aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 55 kabla ya Bolingi kuongeza la tatu dakika ya 64.
Bao la kujifariji la Yanga lilifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 75.
No comments:
Post a Comment