SIMBA ya jijini Dar es Salaam, jana
ilipunguzwa kasi na maafande wa
JKT Ruvu baada ya kutoka sare
tasa katika mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania bara, uliochezwa uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Timu zote zilianza pambano kwa
kasi huku washambuliaji wa kila upande
wakifanya juhudi za kutikisa nyavu
dakika za mapema.
Katika dakika ya 10, mshambuliaji
wa Simba Laudit Mavugo, aliikosesha
bao timu yake baada ya mkwaju aliopiga,
kudakwa kiufundi na kipa wa JKT Ruvu.
Nayo JKT Ruvu, ilijibu mapigo dakika
sita baadae, ambapo Said Kipanga alipiga
shuti ambalo halikulenga lango.
Pamoja na kipa wa Simba Agban
Vicent kutoka golini, Kipanga alishindwa
kukwamisha mpira kimiani, lakini beki
wa Simba, Novarty Lufunga alisaidia
kuokoa.
Kasi ya kushambuliana kwa zamu
ilizidi. Dakika ya 23, Shiza Kichuya nae
alikosa bao na mpira kuwababatiza
walinzi wa JKT Ruvu kabla ya kumfi kia
Mavugo ambaye awali, alipasiwa na
Mohammed Hussein.
Katika kuonyesha shughuli ni
pevu tangu dakika za awali, JKT Ruvu
walimpumzisha Michael Aidani na nafasi
yake kuchukuliwa na James Msuya.
Kipindi cha pili kilianza kwa maafande
wa JKT Ruvu kumtoa Msuya na badala
yake, akaingizwa Naftari Nashon. Simba
nao walimtoa Jamal Mnyate na Mwinyi
Kazimoto akaziba pengo hilo.
Jonas Mkude, katika dakika ya 55,
alijaribu bahati yake kwa kuachia shuti,
lakini liliishia mikononi mwa mlinda
mlango wa JKT Ruvu.
Dakika mbili baadae, maafande hao
kupitia kwa Hassan Matalema, alimjaribu
Agban, kipa huyo akadaka.
Katika kuimarisha safu ya
ushambuliaji, Simba ilimuingiza Ibrahim
Ajib, akapumzishwa Fredrick Blagnon.
Baada ya kuingia, Ajib aliongeza
chachu ya mashambulizi langoni mwa JKT
Ruvu. Katika dakika ya 70, mshambuliaji
huyo alipiga shuti fyongo.
Juuko Murshid naye aliingizwa
kuiongezea nguvu Simba dakika ya 74,
akichukua nafasi ya Lufunga.
Dakika zaidi ya 16 ambazo zilisalia
kabla ya mpira kumalizika, ilikuwa ni
kushambuliana kwa zamu na mashuti
yasiyolenga.
Mpaka dakika 90 zinamalizika,
milango ilibaki kuwa migumu. Kwa
matokeo hayo, Simba imefi kisha pointi
nne, kufuatia ushindi wake katika mchezo
wa kwanza dhidi ya Ndanda FC.
JKT Ruvu: Said Kipao, Michael Aidan,
Salum Gila, Nurdin Mohammed, Rahim
Juma, Ismail Amour, Hassan Matalema,
Hassan Dilunga, Atupele Green, Saad
Kipanga na Pera Mavuo.
Simba: Vicent Agban, Malika Ndeule,
Mohammed Hussein, Novat Lufunga,
Jonas Mkude, Method Mwanjali, Shiza
Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo,
Fredrick Blagnon na Jamal Mnyate
No comments:
Post a Comment