'
Wednesday, August 17, 2016
TIMU YA NETIBOLI YA JWTZ YATWAA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI
Na Selemani Semunyu JWTZ
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ wamekabidhiwa Medali za Dhahabu ikiwa ni sehemu ya kunyakua ubingwa wa Mchezo huo katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Kigali nchini Rwanda.
Mbali na zawadi hiyo Mchezaji Nasra Suleiman wa Timu hiyo ya JWTZ ameshinda tuzo ya Most Valuable Player (MVP) na hivyo kuongeza shangwe kwa T imu ya Tanzania.
Akitoa tuzo hizo ni Mkuu wa Jeshi la Anga la Rwanda Brigedia Generali Charles Karamba alisema katika mashindano haya ambayo ushiriki ndio jambo muhimu kwani sote ni washindi lakini wapo waliofanya vizuri wanaopaswa kupongezwa.
Alisema Katika Netball Tanzania imefanya Vizuri ikifuatiwa na Uganda kisha Kenya hivyo ni nafasi nzuri kuwapongeza waliofanya vizuri zaidi na pia waliofanya vibaya ili kujipanga upya katika mashindano yajayo.
Akizungumza na Waadishi wa habari mkuu wa Msafara wa Timu za Tanzania na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Timu za Tanzania Brigedia Jairos Mwaseba aliipongeza Timu hiyo na kuda ushindi huo waliutarajia kutokana na maandalizi yaliyofanyika.
Kwa upande Mlinzi wa Timu hiyo Joyce Kaira na Mshambuliaji Mwanaidi Hasan walisema wamefurahi kwani waliupoteza ubingwa huo mwaka jana.
Naye Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema maandalizi mazuri yaliyofanywa na Jeshi ndio siri ya ushindi huo sambamba na Nidhamu na kujituma.
Timu hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kombe katika sherehe za ufungaji wa mashindano hayo katika uwanja wa amahoro ambapo mchezo wa mwisho wa Soka kati ya Rwanda na Tanzania utachezwa na kuamua mshindi wa mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment