'
Monday, June 20, 2016
YANGA YAPIGWA 1-0 NA WAALGERIA
YANGA jana ilianza vibaya michuano ya soka ya ligi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa bao 1-0 na MO Bejaia ya Algeria karika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia.
Katika mchezo huo, Yanga ilipata pigo dakika ya 90 baada ya beki wake, Haji Mwinyi kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kjadi ya pili ya njani.
Bao pekee na la ushindi la Waalgeria lilifungwa na beki Yassine Salhi dakika ya 2, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Ismail Belkacemi.
Kutokana na matokeo hayo, MO Bejaia inashika nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambayo juzi iliichama Adeama ya Ghana mabao 3-1.
Katika mechi zijazo za kundi hilo, Yanga wataikaribisha TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati MO Bejaia watakuwa wageni wa Adeama mjini Accra.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment