'
Monday, June 27, 2016
MASHABIKI KUZISHUHUDIA YANGA NA MAZEMBE KESHO BILA KIINGILIO, KAMISAA ATAKA WATAZAMAJI 40,000 PEKEE
YANGA SC imefuta viingilio katika mchezo wa Jumanne wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC na sasa mashabiki wataingia bure.
Taarifa ya Yanga SC jioni hii imesema lengo la kufuta viingilio ni kuvutia mashabiki wengi zaidi uwanjani wajitokeze kuishangilia timu ya nyumbani dhidi ya timu kutoka DRC.
Awali, Yanga ilitaja viingilio viwili tu katika mchezo huo ambavyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP na tiketi ilikuwa zianza kuuzwa kesho.
Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
Wakati huo huo, wanachama wa klabu ya Simba wameahidi kuiunga mkono Yanga katika mechi yao ya kesho dhidi ya TP Mazembe.
Wakizungumza jana mbele ya Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Murro, wanachama hao walisema wamefikia uamuzi huo ili kuonyesha uzalendo kwa taifa lao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment