NAHODHA wa Timu ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta ameahidi kujenga kituo maalum nchini cha kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wachanga ili wafikie viwango vya kimataifa.
Hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika juzi katika kijiji cha wasanii kilichopo Mwenzanga, wilayani Mkuranga.Hayo yamebainishwa na baba wa mwanasoka huyo wa kimataifa, Ali Samtta alipozungumza kwa niaba ya mwanae, katika halfa ya kukabidhiwa ekari tano za eneo la ujenzi wa kituo hicho kulikofanywa na Mtandao wa Wasanii na Wanamichezo nchini, (SHIWATA.).
Alisema, Salamu alizoziacha Mbwana kwa wasanii kwanza ni kuishukuru SHIWATA kwa hatua ya kutambua mchango wake kitaifa, hivyo, katika kulipa fadhila ni kujenga uwanja utakaokuwa na hadhi ya kimataifa kwa taifa.Akizungumza kwa niaba ya mwanae, baba wa nyota huyo alisema, azma ya Samatta (Mbwana) ni kujenga kituo kikibwa cha kimataifa ambacho, moja ya madhumuni ni kuendelea kuwaibua na kuwakuza akina 'Samatta' wengine wajao.
"Niliongea na Mbwana amenituma niwakilishe salamu zake kwa kwanza kwa kuishukuru SHIWATA na kisha kueleza nia yake ya kutaka kuendelea kuibua vipaji vya soka la vijana kupitia kituo kitakachojengwa hapa katika kijiji cha wasanii Mwenzange" alisema Ali Samatta na kuongeza.
Katika hatua nyingine, mwakilishi wa mgeni rasmi, Nape Mnauye, Bi Leah Kihindi aliipongeza SHIWATA kwa hatua yake ya kuwawekea misingi wanachama wake ili wawe na makazi ya kudumu kupitia kijiji hicho.
"Engekuwapo hapa leo, lakini alilazimika kusafiri mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Stars dhidi ya Misri, kurejea Ubelgiji kwa wito wa haraka, lakini anatarajia kurejea tena nchini kwa mapumziko, na mimi amenituma nimwakilishe kwa kauli zake hizi"
Sambamba na hilo, alilipongeza shirikisho hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana Samatta katika soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35 walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akiwatoa taarifa fupi ya kijiji hicho alisema lengo ni kuwasaidia wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari kujenga nyumba za kuishi ili kujiandaa kwa ajili ya kuishi maisha ya taabu baada ya kustaafu kazi zao.
SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.
No comments:
Post a Comment