KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 5, 2016

MISRI YAITUNGUA TAIFA STARS MABAO 2-0


TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilitupwa nje katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika za 2017, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Misri.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars ilifanikiwa kupata penalti kipindi cha pili, lakini iliota mbawa baada ya shuti la Mbwana Samatta kutoka nje ya lango.

Mshambuliaji Mohamed Salah ndiye aliyeiwezesha Misri kutokana na ushindi ugenini baada ya kuifungia mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi.

Samatta: Sikutarajia  kupoteza penalti

NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars',  Mbwana Samatta,  amesema hakutarajia kupoteza penalti katika mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Misri.

Samatta, alikosa mkwaju wa penalti katika kipindi cha pili cha mchezo huo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika za 2017, uliochezwa juzi, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Taifa Stars ilifungwa mabao 2-0 na Misri na kuondoshwa kwenye kinyan'ganyiro hicho, baada ya kupoteza mechi mbili na kutoka sare moja.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Samatta aliwaomba radhi Watanzania kwa kusema, ni hali ya kawaida kutokea katika soka.

“Sikutarajia wala sikudhani kama naweza nikakosa penalti, lakini ndiyo ilishatokea, ni sehemu ya mchezo. Nisingeweza kubadilisha nikauchukue mpira nje nipige tena,” alisema Samatta.

Mshambuliaji huyo anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Genk ya Ubelgiji, alisema Taifa Stars iliuanza mchezo huo vizuri, lakini baada ya wapinzani wao kupaa goli la kuongoza, walibadilika.

Alisema mchezo ulibadilika kwa sababu Wamisri wanajua kutumia nafasi wanazopata kufunga mabao, tofauti na Taifa Stars, ambayo ilijitahidi kutengeneza nafasi nyingi, lakini walishindwa kuzitumia.

Samatta alisema goli la kwanza la Misri, liliwavuruga wachezaji wa Taifa Stars,  hali iliyosababisha waruhusu goli la pili ndani ya muda mfupi.

“Baada ya wao kupata goli la kwanza, walituvuruga kwa sababu hatukutegemea. Muda mwingi sisi tulikuwa na mpira na tunashambulia, lakini ndiyo mchezo, hauwezi kubadilisha matokeo,” alisema.

Taifa Starsa imebakiwa na mchezo mmoja ugenini dhidi ya Nigeria, utakaochezwa Septemba, mwaka huu, lakini hata kama itashinda, haiwezi kusonga mbele.

Katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Misri, iliyochezwa mjini Cairo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment