'
Tuesday, November 15, 2016
AGYEI ATIA SAINI MIAKA MITATU AZAM
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayo furaha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.
Agosti mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.
Agyei anasaini mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.
Tunaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni, hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa kipindi chote atakachokuwa akiipigania jezi ya Azam FC.
Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.
Lengo kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata matokeo bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi tulilokuwa nalo, wachezaji wazuri walioko kikosini na wengine watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza kutuvusha kuelekea safari ya mafanikio msimu huu.
Hivyo, tunawaomba mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu kwani tunaamini ya kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika kuwapa hamasa wachezaji ya kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu kiujumla.
Wakati huo huo, Azam imewapokea wachezaji saba kwa ajili ya majaribio ya kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast) na kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),
Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.
Monday, November 14, 2016
NAPE AMKABIDHI BENDERA MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MISS AFRICA 2016
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.
Nape ametoa ahadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Nnauye ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija kwa Taifa hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini” alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd,Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“ kwa niaba ya Millen Magese group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika mashindano haya”Alisema Chuma.
Kwa upande wake Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi kuitangaza nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika urembo” Alisema Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi bendera ya Taifa kwa mlimbwende Julieth Kabete ambaye ameshiriki Shindano la Miss Tanzania na kufanikiwa kushika namba nne Julietha ambapo anakwenda nchini Nigeria kushiriki shindano ya Afrika, litakalofanyika baadae mwezi huu. Katika picha akiwa pamoja na baadhi ya waandani wa Miss Tanzania Hashim Lundenga na mwakilishi wa Milen Magese Matukio Chuma na mama mzazi wa Julieth.
Wednesday, November 9, 2016
SIMBA YAPIGWA 2-1 NA PRISONS
TIMU kongwe ya soka ya Simba, jana, iliendelea kupunguzwa kasi ya kuwania taji la ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Prisons.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Simba katika kipindi cha wiki moja. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Simba ilichapwa bao 1-0 na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na kupokea kipigo hicho, Simba imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 35, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 30 na Azam yenye pointi 25.
Iliwachukua Simba dakika 43 kuhesabu bao lililofungwa na Jamal Mnyate baada ya kuunganisha wavuni kwa kichwa mpira wa krosi kutoka kwa Shizza Kichuya.
Prisons ilisawazisha dakika ya 47 kwa bao lililofungwa na Victor Hangaya baada ya kuunganisha wavuni kwa kichwa krosi kutoka kwa Salum Bosco.
Bao la pili la Prisons lilifungwa na Hangaya tena dakika ya 63 baada ya kuunganisha wavuni mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mohammed Samatta.
Tuesday, November 8, 2016
TWIGA STARS YAENDA CAMEROON, SERENGETI BOYS YAENDA KOREA KUSINI
WAKATI timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ ikiondoka leo Novemba 8, 2016 kwenda Yaounde, Cameroon kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Vijana wa Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Boys, wao wanatarajiwa kuondoka kesho Novemba 9, 2016 kwenda Korea Kusini, kupitia Dubai, Falme za Kiarabu.
Twiga Stars imeondoka na nyota 17 na viongozi sita kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) ambako walipita Nairobi, Kenya ilihali Serengeti Boys kwa upande wao watatumia ndege ye Emirates katika safari itakayoanza saa 10.30 jioni. Inakwenda kushiriki michuano maalumu ya kimataifa ya vijana ambako itaripoti Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, kuanzia saa 7.00 mchana.
Wakati Serengeti wakiwa wamealikwa huko Korea Kusini, Twiga Stars wao wamealikwa na Waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016 – Cameroon ambao wameamua kuipa heshima Tanzania na kuona kuwa timu hiyo ina ubora wa na kwamba inafaa kuipimana ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
Twiga Stars ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya kuwa kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni mabinga wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko Uganda.
Rekodi hizo zimesukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT) – nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo kuomba kucheza nayo mwishoni mwa wiki hii. Tayari Twiga Stars imeanza maandalizi ya kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake Edna Lema na El Uterry Mohrery.
Kikosi cha Twiga Stars wamo makipa, Fatma Omari na Najiat Abbas; mabeki ni Wema Richard, Sophia Mwasikili, Anastasia Katunzi, Maimuna Hamisi, Fatuma Issa, Happiness Mwaipaja na Mary Masatu wakati viungo ni Donisia Minja, Stumai Abdallah, Amina Ally, Anna Mwaisura na Fadila Kigarawa ilhali washambuliaji ni Fatuma Swalehe, Asha Rashid na Mwanahamisi Omari.
Vijana wanaosafiri kesho ni makipa Ramadhani Kabwili, Kelvin Kayego na Samwel Brazio; mabeki ni Shomari Ally, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ally Msengi na Enrick Vitalis wakati viungo ni Ally Ng’anzi, Shaban Ada, Asad Juma, Issa Makamba huku washambuliaji wakiwa ni Muhsin Makame, Ramadhani Gadaffi, Rashid Chombo, Cyprin Mtesigwa na Mohammed Abdallah.
Kwa upande wa Taifa Stars, kikosi cha Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuondoka Ijumaa Novemba 11, mwaka huu kikiwa na nyota 20 kati ya 24 waliotangazwa wiki iliyopita. Stars inakwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo, nasi mara moja tukakubali.
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY
KESHO NI SIMBA NA PRISONS, YANGA KUIVAA RUVU SHOOTING ALHAMISI
Wakati michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016, mchezo kati ya Young Africans na Ruvu Shooting utafanyika Alhamisi Novemba 10, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, imefahamika.
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili iliyopita ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya Young Africans umesogezwa mbele.
Michezo mingine ya kesho Jumatano inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo.
Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

TFF YATUMA RAMBIRAMBI VIFO VYA SITTA NA MWENYEKITI WA AZAMA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutokana na kifo cha Spika Mstaafu wa bunge hilo la Tanzania, Samwel Sitta.
Mzee Sitta ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Urambo lililopo mkoani Tabora amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 7, 2016 kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Technical iliyopo Munich nchini Ujerumani usiku wa kuamkia leo Novemba 7, 2016.
Rais Malinzi amesema kwamba Sitta ameacha alama ya ucheshi na upenzi katika michezo hususani soka kwani enzi zake hakuficha mapenzi yake kwa klabu ya Simba alikokuwa mwanachama.
Salamu za rambirambi za Rais Malinzi zimekwenda pia kwa Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Amewataka kuwa watulivu wakati huu mgumu wa kumpoteza Mzee Samwel Sitta na kwamba anaungana nao kwenye maombolezo.
Akimwelezea zaidi Mzee Sitta, Rais Malinzi amesema kwamba "Binafsi nitamkumbuka na kuenzi uchapakazi wake. Alikuwa Mwanamichezo aliyekuwa na Mzalendo hususani alipokuwa Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na alikuwa pia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.
MALINZI AMLILIA SHEIKH SAID MOHAMMED WA AZAM
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad aliyefariki dunia leo Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Taarifa za kufariki dunia kwa Mzee Said Muhammad ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi zimethibitishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba aliyesema kwamba alifariki dunia katika wodi ya Wagonjwa mahututi (ICU) hospitalini hapo baada ya kuzidiwa ghafla nyumbani kwake.
Kutokana na kifo hicho, Rais wa TFF Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Yahya Mohammed, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, Uongozi wa Klabu ya Azam, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Amewataka kuwa watulivu wakati huu mgumu wa kumpoteza Mzee Said Muhammad.
Katika salamu zake, Malinzi amemwelezea marehemu Said Muhammad kuwa alikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo katika Kamati ya Utendaji ya TFF.
Aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.
“Ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Mzee Muhammad ndiye aliyekuwa na umri mkubwa ukilinganisha na wajumbe wengine, lakini alikuwa hakosi vikao muhimu. Mchango wake wa mawazo ulikuwa nguzo kwetu. Nimepokea taarifa hizi za kifo chake kwa masikitiko makubwa,” amesema Rais Malinzi leo mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho.
Taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwa marehemu. Sheikh Said Muhammad atazikwa kesho Jumanne alasiri katika makaburi ya Kisutu baada ya mwili wake kuswaliwa msikiti wa Maamur ulioko Upanga, jijini Dar es Salaam.
Inna lillah wainn ilayh Rajiuun.

SIMBA YAZIMWA, YANGA YAFUFUA MATUMAINI
BAO lililofungwa na mshambuliaji Abdalla Mguhi dakika ya 89 limeiwezesha African Lyon kuichapa Simba bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mguhi, mchezaji wa zamani wa kikosi cha pili cha Yanga, alifunga bao hilo akimalizia krosi maridhawa kutoka kwa Miraji Adam na hivyo kuamsha shangwe kwa mashabiki wachache wa African Lyon huku wale wa Simba wakiondoka uwanjani kwa majonzi.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, mabingwa watetezi Yanga walifufua matumaini ya kutwaa taji hilo baada ya kuichapa Prisons bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Bao pekee na la ushindi la Yanga lilifungwa kwa njia ya penalti na mshambuliaji Simon Msuva baada ya James Mwasote wa Prisons kumchezea rafu mbaya Obrey Chirwa wa Yanga.
Prisons ilipata nafasi nzuri ya kufunga bao la kuongoza dakika ya 55 baada ya kupata adhabu ya penalti, lakini shuti la Lambert Sabiyanka wa Prisons, liliokolewa na kipa Benno Kakolanya wa Yanga.
MSUVA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA
Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).
Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

MCHEZO KATI YA BULYANHULU, GREEN WARRIORS
Mchezo Na. 4 wa Ligi Daraja la Pili kati ya Bulyanhulu na Green Warriors ulikuwa ufanyika jana Novemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa CCM-Kambarage, mkoani Shinyanga haukufanyika.
Mchezo huo haikufanyika kwa sababu ya kukosa mawasiliano kati ya msimamzi wa kituo huko Shinyanga, Kamisaa na Mchezo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa taarifa hii, TFF inapenda kufahamisha familia ya mpira wa miguu kuwa mchezo huo utafanyika hapo baadaye kwa kupangiwa tarehe nyingine mpya baada ya kuondolewa kwa changamoto inayohusu leseni za wachezaji ambazo ziko tayari shirikishoni.
AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUZINDULIWA TANGA NOVEMBA 19, 2016
Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu, itaanza rasmi Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika mkoani Tanga.
Bingwa wa Mkoa wa Tanga msimu 2015/2016, Muheza United itacheza Sifa Politan ambayo ni Bingwa wa Temeke, Dar es Salaam – mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.
Siku hiyo kabla ya mchezo kutakuwa na shamrashamra kupamba michuano hiyo zitakazoandaliwa na Wadhamini Azam Tv ambayo kwa msimu wa 2016/17 zimeongezwa timu 22 kutoka mabingwa wa mikoa-- Muheza na Sifa Politan ni miongoni mwa timu hizo. Ongezeko hilo tofauti na msimu uliopita ambako kulikuwa na timu 64.
Mwaka huu kuna timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu zote 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL) na timu 22 za mabingwa wa mikoa. Mashindano hayo yatakuwa ni ya mtoani na yataendeshwa kwa raundi tisa (9).
Raundi ya Kwanza itashirikisha timu zote 22 za Mabingwa wa Mikoa katika makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu zitaingia raundi ya pili.
Raundi ya Pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya kwanza na kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya timu zote kuwa 32 kwa hatua ya pili.
Raundi ya Tatu itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane zitakazoingia hatua ya nne.
Raundi ya Nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha timu nane (8) zilizoshinda Raundi ya Tatu (3) kufanya timu zote kuwa 32.
Raundi ya Tano, itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya Nne (4) na kumuisha timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya timu zote katika raundi hii kuwa 32.
Raundi ya Sita itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika Raundi ya Tano na mzunguko huo utaitwa Hatua ya 16 Bora.
Raundi ya Saba (7) itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na mzunguko huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .
Raundi ya Nane ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu Raundi ya Saba (Robo Fainali) na mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni Nusu Fainali.
Raundi ya Tisa itashirikisha timu mbili zilizofuzu Raundi ya Nane na washindi hao wa Nusu Fainali na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa msimu wa 2016/2017.
LIGI YA VIJANA KUANZA KUPIGWA NOVEMBA 15, 2016
Ligi ya Vijana ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) wenye umri wa chini ya miaka 20, inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 mwaka huu kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwa timu za vijana za Kagera Sugar na Young Africans ya Dar es Salaam kuchuana siku hiyo.
Timu hizo ambazo zimepangwa kundi A, zitaanza mchezo wao siku hiyo saa 10.30 jioni (16h30) ikiwa ni baada ya shamrashamra za uzinduzi wake. Kwa kuwa itakuwa ni uzinduzi, basi siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja tu, lakini kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi ya TFF kwa siku kutakuwa na michezo miwili kwa tofauti ya saa – mchana na jioni.
Mbali ya Kagera Sugar na Young Africans, timu nyingine ambazo zitakuwa kwenye kundi hilo la A ni Stand United na Mwadui za Shinyanga ambazo zitacheza siku inayofuata (Novemba 16, 2017) saa 10.30 jioni na kwa kukamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo, Novemba 17, mwaka huu Azam itacheza na Mbao FC katika mchezo utakaopigwa saa 8.00 mchana (14h00) kabla kuzipisha Toto Africans na African Lyon saa 10.30 jioni.
Kwa upande wa Kundi B ambalo kituo chake rasmi kitakuwa Dar es Salaam, Simba itafungua dimba na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini - mchezo utakaonza saa 8.00 kabla ya kuzipisha timu za JKT Ruvu na Ruvu Shooting kucheza saa 10.30 jioni siku hiyo hiyo.
Ili kukamilisha mzunguko wa kwanza, siku inayofuata Novemba 17, mwaka huu Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City saa 8.00 mchana (14h00) wakati Majimaji itacheza na Mtibwa saa 10.30 jioni.
Ligi hiyo ya mkondo mmoja, hatua ya makundi inatarajiwa kufikia ukomo Desemba 12, 2016 ambako timu nne vinara kutoka katika kila kundi zitapangiwa ratiba mpya na kituo ili kutafuta bingwa wa msimu kwa timu za vijana. Kituo hicho kitatangazwa baada ya kumalizika hatua ya makundi hapo Desemba 12, mwaka huu.
Ujio wa ligi hiyo ni utekelezaji au kukidhi matakwa ya maelekeo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kategori ya uwepo wa timu za vijana zinazoshindana mbali ya kupata huduma za shule na matibabu kwa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza.
MKWASA ATAJA TAIFA STARS ITAKAYOIVAA ZIMBABWE NOVEMBA 13
Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo Novemba 04, 2016 ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri wiki ijayo kwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Novemba 07, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kikosi hicho siku inayofuata ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako itakuwa funga dimba la duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:
Makipa
Deogratius Munishi –Young Africans
Said Kipao –JKT Ruvu
Aishi Manula –Azam FC
Mabeki
Erasto Nyoni -Azam FC
Michael Aidan -JKT Ruvu
Mwinyi Haji -Young Africans
Mohamed Hussein –Simba SC
David Mwantika -Azam FC
James Josephat –Tanzania Prisons
Vicent Andrew -Young Africans
Viungo wa Kati
Himid Mao -Azam FC
Mohammed Ibrahim –Simba SC
Jonas Mkude –Simba SC
Muzamiru Yassin –Simba SC
Viungo wa Pembeni
Abdulrahman Mussa -Ruvu Shooting
Shiza Kichuy –Simba SC
Simon Msuva -Young Africans
Jamal Mnyate –Simba
Washambuliaji
Ibrahim Ajib –Simba SC
John Bocco -Azam FC
Mbwana Samatta -K.R.C Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli –Oman
Thomas Ulimwengu –Mchezaji huru
Omar Mponda -Ndanda
Kwa sababu mbalimbali hususani majeruhi, Mkwasa amewaacha wachezaji Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Juma Abdul na Juma Mahadhi wa Young Africans.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo, nasi mara moja tukakubali.
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45).
Wachezaji wa Zimbabwe watakaochuana na Tanzania ni makipa: Tatenda Mukuruva (Dynamos) na Donovan Bernard (How Mine).
Mabeki: Godknows Murwira (Dynamos), Hardlife Zvirekwi (CAPS United), Ronald Pfumbidzai (CAPS United), Honest Moyo (Highlanders), Lawrence Mhlanga (Chicken Inn) na Teenage Hadebe (Chicken Inn).
Viungo: Tendai Ndlovu (Highlanders), Farai Madhanhanga (Harare City), Jameson Mukombwe (Chapungu), Tafadzwa Kutinyu (Chicken Inn), Ronald Chitiyo (Harare City), Talent Chawapihwa (ZPC Kariba) na Malvern Gaki (Triangle).
Washambuliaji: Pritchard Mpelele (Hwange), Gift Mbweti (Hwange), Leonard Tsipa (CAPS United), Rodreck Mutuma (Dynamos) na William Manondo (Harare City)
MAZUNGUMZO YANGA, SIMBA KUHUSU HASSAN KESSY YAENDELEA VEMA
Mazungumzo kati ya Viongozi wa Young Africans na Simba, katika shauri la madai, yanaendelea vema na mwishoni mwa wiki hii huenda wakakamilisha kwa kuridhiana.
Viongozi hao wamefanya hivyo kwa dhana kuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayosisitiza uungwana katika soka ikisema: “My Game is Fair Play”. Kwa upande wa Young Africans, uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit wakati upande wa Simba alikuwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Katika kikao hicho ambacho Msuluhishi wake, Wakili na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Said El – Maamry hakuhudhuria kwa sababu za udhuru, Baraka wa Young Africans aliongozana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Young Africans, Omar Said pamoja na Mawakili Oscar Magolosa na Alx Mushumbusi.
Kwa hali halisi ya uchumi kwa sasa, timu hizo zimezungumza hadi kufikia mwafaka wa kiwango kisichozidi Sh milioni 200 kutoka dola dola 600,000 (zaidi ya Sh milioni 1,200 au Bilioni 1.2). Mazungumzo ya wikiendi hii yanakwenda kukamilisha mvutano wao, kama ambavyo walikubaliana kwenye kikao kilichoketi jana Novemba 03, 2016.
Madai makuu ya Simba ni dhidi ya mchezaji Hassan Hamis Ramadhani maarufu kwa jina la Hassan Kessy na dhidi ya Young kudaiwa kuvunja mkataba na kuingilia makubaliano mapya wakati tayari mchezaji alikuwa na mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

TWIGA STARS KUIPIMA UBAVU CAMEROON
Waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016, wameipa heshima Tanzania na kuona kuwa Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake inafaa kuipima ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
Twiga Stars ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya kuwa kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni mabingwa wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko Uganda.
Rekodi hizo zimelisukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT) – nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo kuomba kucheza nayo mwishoni mwa wiki ijayo. Tayari Twiga Stars imeanza maandalizi ya kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake Edna Lema na El Uterry Mollel.
Kutokana na kuitikia wito huo kutakuwa na mabadiliko kidogo ya ratiba kwa Ligi Kuu ya Wanawake. Ligi hii itaendelea kama ilivyo kwenye ratiba kwa makundi yote mawili ya A na B, isipokuwa kwa michezo miwili tu ambayo yote ni ya Kundi A.
Mchezo kati ya JKT Queens na Viva FC kadhalika Evergreen Queens na Mlanduzi Queens, ambayo itapangiwa tarehe nyingine. Michezo yote hii ilikuwa ichezwe tarehe 09.11.2016 kwenye viwanja vya Karume na Uhuru, Dar es Salaam.
Timu za JKT Queens na Mlandizi Queens zina wachezaji zaidi ya wawili kwenye Twiga Stars ambako JKT Queens wana wachezaji 11 na Mlandizi Queens ina wachezaji watatu.

Wednesday, November 2, 2016
SIMBA HII NI KAMA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS MAGUFULI
KIU ya Simba kutwaa tena taji la ligi kuu ya Tanzania Bara, imeendelea kujidhihirisha leo baada ya kuichapa Stand United bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Bao hilo la pekee na la ushindi la Simba lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya kwa njia ya penalti dakika ya 33, baada ya Laudit Mavugo kuangushwa na beki Adeyum Ahmed wa Stand United ndani ya eneo la hatari.
Kutokana na ushindi huo, Simba imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13. Stand inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 14.
Katika pambano hilo, timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao, lakini umaliziaji mbovu wa washambuliaji wake ulikuwa kikwazo.
Wakati huo huo, mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam leo wameendelea kufufua matumaini ya kutwaa taji hilo baada ya kuwachapa Toto African bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Bao pekee na la ushindi la Azam lilifungwa na mshambuliaji Shabani Iddi dakika ya 81 baada ya kupokea pasi kutoka kwa John Bocco.
YANGA MAJANGA, YAPIGWA 2-1 NA MBEYA CITY
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara, Yanga leo wamekwaa kisiki mbele ya Mbeya City baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Mbeya City iliyokuwa ikishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wake, ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao hayo 2-1.
Matokeo hayo yameiwezesha Mbeya City kufikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 14 wakati Yanga inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 13.
Mbeya City ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya sita lililofungwa na Hassan Mwasapili kwa shuti la mbali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Dida wa Yanga akigaagaa.
Bao la pili la Mbeya City lilifungwa na Kenny Ally dakika ya 36 kwa shuti la mbali baada ya kupokea pasi fupi ya mpira wa adhabu kutoka kwa Haruna Shamte.
Wachezaji wa Yanga walililalamikia bao hilo na kumzonga mwamuzi Rajab Mrope kutoka Ruvuma kwa madai kuwa halikuwa halali. Baada ya kujadiliana na wasaizidi wake, mwamuzi huyo aliashiria kwamba lilikuwa bao halali.
Bao la kujifariji la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 45.
Katika kipindi cha pili, Mbeya City ilicheza zaidi mchezo wa kujihami na kuwapa usumbufu mkubwa washambuliaji wa Yanga kujaribu kutafuta bao la kusawazisha.

MWAMUZI WA TANZANIA KUCHEZESHA FAINALI ZA AFRIKA ZA WANAWAKE
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limemteua Jonesia Rukyaa - Mwamuzi wa soka kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi wa kati 10 watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka huu.
Kwa uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amempigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za kimataifa.
Rais Malinzi amesema kwamba Mwamuzi Jonesia ameliletea heshima taifa la Tanzania kwa kujijengea heshima ya kuaminika mbele ya Kamati ya Ufundi ya CAF – Waratibu na Waandaaji wa fainali hizo zitakazofanyika Cemaroon ambako mechi za mechi ya mwisho ya fainali itafanyika Desemba 3, mwaka huu.
“Namtakia kila la kheri, naamini kwamba Jonesia atafanya vema. Nina uhakika kwamba hii ndiyo njia yake pekee ya kufanikiwa zaidi kwani ipo siku atateuliwa kuchezesha hata fainali za Kombe la Dunia,” yalikuwa ni maneno ya Malinzi akimwelezea Jonesia kwenye simu leo mchana.
Jonesia anafanya idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchi za Afrika Mashariki kuwa watano kwani wengine kwa mujibu wa orodha ya CAF ni Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne Wanjala (Kenya) na Suan Ratunga (Burundi).
Waamuzi wengine ni Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe (Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou (Cameroon) na Aissata Amegee (Togo). Katika orodha hiyo pia yumo Mary Njoroge wa Kenya ambaye mwamuzi wa pembeni pekee.
Katika fainali hizo, timu shiriki ni Cameroon, Afrika Kusini, Misri na Zimbabwe zipo kundi A wakati Nigeria, Ghana, Kenya na Mali zimo kundi B.

SIMBA, YANGA VITANI TENA LEO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15, Novemba 12, mwaka huu.
Vinara ligi hiyo kwenye msimamo msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Africans Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea mkoani humo – JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ilihali Ndanda itawakabiri Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao Fc ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Wakati ligi hii ikiingia ukiongoni kwa nusu msimu, TFF inatoa wito kwa timu kuajiandaa na dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15, mwaka huu kusajili wachezaji mahiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwendelezo wa ligi hiyo nusu ya msimu uliobaki utakaoanza baadaye Desemba.
Wakati wa usajili wa dirisha dogo ndipo michuano ya hatua ya awali ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/2017 inatarajiwa kuanza Novemba 19, mwaka huu ambako pia imepangwa kuzindua michuano hiyo hukop mkoani Mara.
Safari hii timu shiriki zimeongezwa mabingwa wa mikoawa mwaka jana hivyo kufikisha idadi itakayofika 86 badala ya 64 za msimu ulioipita. Imechukuliwa mikoa 22 baada ya ile mitano, kupanda Daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu huu ambayo imeanza kushika kasi.

TAIFA STARS SASA KUJIPIMA NGUVU NA ZIMBABWE
Baada ya kukosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ethiopia, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepata mwaliko wa kucheza na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika jijini Harare, Novemba 13, mwaka huu.
Kama ilivyotokea kwa Ethiopia kuomba nafasi hiyo kwa Tanzania, pia Zimbabwe imefanya hivyo na mara moja Tanzania imethibitisha kucheza mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa wenye kutoa tathmini ubora ili kuingia kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kuikosa Ethiopia ambayo ilitoa taarifa baadaye kuwa isingeweza kuihodhi Taifa Stars kwa sababu ya hali mbaya ya hewa kwa kipindi cha Oktoba mwanzoni, kulisababisha Tanzania iliyokuwa imejiandaa kucheza mechi hiyo kushushwa kwa kiwango kikubwa nafasi ya ubora wa viwango vya FIFA kutoka ya 132 hadi zaidi ya 144. Zimbambwe kwa sasa ni ya 110 na Ethiopia ni ya 126.
Tayari Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amepewa majukumu ya kuanza maandalizi na wakati wowote wiki hii atatangaza kikosi ambacho kitawavaa vijana hao wa Mheshimiwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
“Ni kipimo kizuri, ni timu nzuri kucheza nayo,” alisema Mkwasa alipozungumza na Mtandao wa TFF ambao ni www.tff.or.tz.
Taifa Stars ambayo kwa sasa haina mashindano au kujiandaa na mashindano yoyote baada ya kutolewa nafasi ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika, inajipanga huku ikisubiria ratiba mpya za Baraza la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki (CECAFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

EL MAAMRY KUZIKUTANISHA SIMBA NA YANGA KUHUSU KESSY
Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan Hamisi Ramadhani maarufu kama Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa mwadai hayo.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Young Africans kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.
Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Young Africans kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.
Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Young Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.
Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa.”
Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.
Subscribe to:
Posts (Atom)