'
Sunday, May 29, 2016
MBEYA CITY YAANZA KUSAKA NYOTA WAPYA
SIKU chache baada ya pazia la ligi kuu ya soka Tanzania bara kufungwa,Kocha mkuu wa Mbeya City Fc Kinnah Phiri ameanza zoezi maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha moja kwa moja kwenye vikosi vya timu yake msimu ujao.
Akizungumza muda mfupi baada ya majaribio ya siku ya kwanza kwa wachezaji wapya vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha vipaji walivyonavyo navyo, afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa muitikio umekuwa mzuri katika siku hii kwanza ambayo nyota hao wa baadae wamefika kuonysha uwezo wao mbele ya kocha huyo raia wa malawi.
“Leo ni siku ya kwanza, kitu kizuri mwitikio umekuwa mkubwa, takribani vijana 50 wamejitokeza kujaribu bahati zao kulingana na vipaji walivyonavyo, haya ni majaribio ambayo kocha Phiri ameyaitisha ili kusaka vipaji vipya ambavyo moja kwa moja vitaingia kwenye timu yetu kubwa na ile ya U20, alisema.
Akiendelea zaidi, Ten alisema kuwa, hii imekuwa ni kawaida kwa City kila inapofika mwisho wa msimu kuwaleta pamoja vijana wote wanaoamini wanauwezo wa kucheza mpira, kufichua vipaji vyao ili waje kuwa wachezaji wakubwa baadae.
“Hii ni kawaida yetu, kila tunapomaliza msimu huwa tunafanya hivyi, vijana wote wenye umri kuanzia miaka 17-22 ni fursa kwao kujitokeza, zoezi hili la kusaka vipaji litakuwepo kwa juma zima, leo hatukuwa na kocha Phiri kwa sababu alikuwa kwenye majukumu mengine lakini kesho tutakuwa kwenye uwanja Sokoine na mwalimu atakuwa, kwa hiyo vijana wote ndani ya jiji la Mbeya na mikoa ya jirani waje kujaribu bahati zao.
Kwa upande wa vijana waliojitokeza siku ya leo, walishukuru kuwepo kwa zoezi hili kwa sababu limerahisisha uwezekano wa vipaji walivyonavyo kuonekana mapema hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji wakubwa siku za usoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment