'
Sunday, May 29, 2016
MBEYA CITY YAPATA NYOTA WAPYA 44
ZOEZI kusaka nyota wapya (vijana) ambao wataingizwa kwenye timu mbili za Mbeya City Fc U20 na ile ya wakubwa limefikia kwenye hatua nzuri hivi sasa baada ya wachezaji 44 kupatikana kwenye mchujo wa awali uliolifanyika leo ikiwa ni baada ya siku nne za mazoezi.
Akizungumza na mbeyacityfc.com, mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya leo (Clinic day 5) kwenye uwanja wa Sokoine kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema kuwa Vijana 44 wamefanikiwa kuvuka kwenye mchujo wa kwanza hivyo wataingia kwenye wamu ya pili inayotaraji kuanza hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine.
“Tulikuwa na kundi kubwa la wachezaji zaidi ya 106, baada ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata 44 ambao wataingia kwenye awamu ya pili hapo kesho, lengo letu ni kuona tunapata Cream nzuri kwa ajili ya timu yetu ya vijana na pia wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema.
Kuhusu lini itakuwa siku ya mwisho, kocha huyo kijana alitanabaisha kuwa, mchakato huu wa kuska vipaji ulikuwa ufikie tamati hapo kesho lakini uongozi wa City umeamua kusogeza mbele mpaka siku ya jumamosi ambapo wachezaji watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho watapata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Ilemi Fc.
“Ilikuwa tuhitimishe kesho lakini tumesogeza mpaka jumamosi ambapo vijana wetu wapya watakaopatikana watacheza mchezo wa kirafiki , na baada ya hapo zoezi litafungwa tayari wa kusubiri maandalizi ya msimu mapema mwezi ujao” alimaliza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment