'
Wednesday, July 2, 2014
MBEYA CITY, PRISONS KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na Tanzania Prisons zinacheza
mechi ya kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa
matumizi ya tiketi za elektroniki kwa washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili
jioni.
Kiingilio ni sh. 3,000 kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo (Julai Mosi
mwaka huu).
Wakati huo huo, keshokutwa (Julai 3 mwaka huu) kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya
tiketi za elektroniki yatakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
kuanzia saa 3 asubuhi.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa mechi katika uwanja huo, viongozi wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), meneja wa Uwanja wa
Sokoine na msaidizi wake, makatibu wa Tanzania Prisons na Mbeya City, maofisa
habari wa Mbeya City na Tanzania Prisons, Ofisa Usalama wa MREFA na wasimamizi
wa milangoni (stewards).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment