KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, October 5, 2012

SIMBA KUKIPIGA NA OLJORO JKT, YANGA NA KAGERA SUGAR WIKIENDI HII


Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
Jumapili (Oktoba7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).

1 Simba SC     5  4  1  0  10  3  7  13


2 Azam 4 3 1 0 7 2 5 10

3 JKT Oljoro 5 2 3 0 8 5 3 9

4 Coastal Union 5 2 3 0 7 5 2 9

5 Young Africans 5 2 2 1 8 6 2 8

6 Tanzania Prisons 5 2 2 1 6 5 1 8

7 Mtibwa Sugar 4 2 1 1 6 3 3 7

8 Kagera Sugar 5 2 1 2 6 5 1 7

9 African Lyon 5 2 0 3 5 9 -4 6

10 JKT Ruvu 5 2 0 3 4 10 -6 6

11 Toto African 5 0 4 1 4 5 -1 4

12 Ruvu Shooting 5 1 0 4 6 10 -4 3

13 Polisi Morogoro 5 0 2 3 1 4 -3 2

14 Mgambo JKT 5 0 0 5 2 8 -6 0

No comments:

Post a Comment