KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, September 15, 2012

FFU NGOMA AFRIKA KUTUMBUIZA AFRIKA-MESSE,BREMEN,UJERUMANI LEO

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU, yenye maskani yake kule ujerumani, inayokamatia taji la kimataifa la "IDA-International Diaspora Award' inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine makubwa leo jumamosi ya 15.9.2012

Kikosi kazi hicho kitapeleka nguvu zote katika maonyesho makubwa ya biashara ya kiafrika "AFRIKA-MESSE" Bremen,yatakayafanyika mjini Bremen,Ujerumani.

Bendi hiyo inayotamba CD mpya "Bongo Tambarare" ambayo imeshatua kwa kishindo katika vituo vya redio mbali mbali ndani na nje.

Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 muhasisi wake Kamanda Ras Makunja, wa FFU,ambaye pia ndiye kiongozi wa kikosi kazi hiko.

Kikosi kazi hiko kilichojizolea washabiki kila kona duniani kimekua tishio la kimataifa,inasemekana kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyo fanikiwa kuteka nyoyo za washabiki wa kimataifa na kuwafanya washabiki kuwa ndio wamiliki wa bendi hiyo.

Usikose kuwasikiliza bofya at http://www.ngoma-africa.com/


No comments:

Post a Comment