KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 18, 2017

SINGIDA UNITED YAMNASA NYOTA WA KIMATAIFA WA RWANDA


Timu ya Singida United imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Rwanda ambaye alikuwa anacheza timu ya Polisi,Danny Usengimana na kuwa mchezaji wa sita wa kigeni kusajiliwa na matajiri hao.

Mshambuliaji huyu anayetabiliwa kuwa nitishio katika kufumani nyavu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ameingia kandarasi ya miaka miwili na kikosi cha Kocha Mkuu wa zamani wa Mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ,Hans Van Der Pluijm.

Timu ya Singida United ni timu tatu zilizopanda kushiriki Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na nyingine ni Lipuli pamoja na Njombe Mji.

HATIMAYE MKUDE AMWAGA WINO SIMBA


Hatimaye Nahodha wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amezima ndoto za Yanga baada ya kuongeza mkataba na klabu yake hiyo wa miaka miwili wa kukitumikia kikosi cha mabingwa wa Kombe la FA.

Kulikuwa na mvutano na timu yake kwa dau kubwa ambalo alilokuwa anataka huku kukienea tetezi kuwa mahasimu wao wakubwa Yanga walikuwa wanamhitaji hii baada ya mshambuliaji wao hatari Ibrahimu Ajibu kujiunga na Mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania.

“Ameongeza mkataba wa miaka miwili, ilikuwa ni baada ya kukamilisha majadiliano ambayo yalikuwa yamefikia zaidi ya asilimia 99,” kilieleza chanzo.

VIGOGO WAZIDI KUJITOSA UCHAGUZI MKUU WA TFF


Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umepangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Tayari wagombea wameanza kuchukua fomu na wamekuwa wakijitokeza kwa kasi kubwa.
Kinachoshangaza zaidi ni idadi kubwa ya wale wanaowania nafasi ya urais inayoshikiliwa na Jamal Malinzi.
Waliojitokeza ni watatu hadi sasa wakionyesha kwamba wanaitaka nafasi hiyo ili kufanya sahihi zaidi.
Wadau hao wamejitokeza kuchukua fimu hizo kwa kipindi cha siku mbili tu, yaani jana Ijumaa na leo Jumamosi katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam.
URAIS
Jamal Malinzi
Imani Madega
Wallace Karia
Fredrick Masolwa
MAKAMU RAIS
Mulamu Nghambi
Michael Wambura
Geofrey Nyange
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI
Soloum Chama
Ephraim Majinge
Elias Mwanjala
Saleh Alawi
Kaliro Samson
Vedastus Lufano
Kenneth Pesambili
Mbasha Matutu
Samwel Daniel
Dunstan Mkundi
Athuman Kambi
Shaffi Dauda
Golden Sanga
Charles Mwakambaya
Benista Rugola.
Thabit Kandoro
Goodluck moshi
James Mhagama
Husen Mwamba
Sarah Chao
Isaa bukuku
Stewat Masima
Emmanuel Ashery
Abdul Sauko
Musa Sima
Stanslaus Nyongo
Ayoub Nyenzi
John Kadutu
Baraka Mazengo
Khalid Mohamed
Mohamed Aden
Cyprian Kuyava
Saleh Abdul
IMETOLEWA NA LEO
Alfred Lucas

Ofisa Habari TFF

Saturday, June 17, 2017

HANSPOPE AMPANDIA NDEGE OKWI NA KUNASA SAINI YAKE

HATIMAYE klabu ya Simba imekamilisha mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.
Simba imenasa saini ya mchezaji huyo baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope kufunga safari kwenda Kampala, Uganda kukamilisha mazungumzo na nyota huyo.
Okwi ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa Simba walioiletea mafanikio makubwa klabu hiyo katika ligi kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa.
Hata hivyo, bado haijawekwa wazi kuhusu kiwango cha fedha alicholipwa mshambuliaji huyo ili arejee Simba.

MCHAKATO WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE TANZANIA (TWFA)


Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA), leo Juni 16, 2017 imetangaza rasmi Uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni. Ratiba kamili kuelekea uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-
Juni 23, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.
Juni 24, 2017- Kamati ya Uchaguzi kutangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katib au kanuni za TWFA.
Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa
Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa
Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Julai 04 hadi 07, 2017-Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili
Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA


Mushumba amesema kwamba nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. Sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.


Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000. Fomu zitapatikana ofisi za Hosteli ya TFF zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

NENO KUTOKA KWA RAIS WA TFF KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Ndugu zangu viongozi, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania.


Kama ilivyotangazwa na kamati yetu ya uchaguzi leo tumeanza rasmi mchakato wa uchaguzi wetu.


Hiki ni kipindi muhimu kwa ustawi wa mpira wetu.


Ninaomba niwahakikishie wadau wa mpira wa miguu Tanzania kuwa Sekretarieti ya TFF ambayo kikatiba ninaisimamia mimi itaendelea na shughuli zake bila kuathiriwa na mchakato huu, hii itakuwa ni pamoja na kuandaa timu zetu mbalimbali za Taifa na kushughulikia majukumu yake mengine ya kila siku.


Aidha ninaomba niwahakikishie viongozi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania kuwa mimi kama Rais wa TFF sina kundi katika uchaguzi huu.


Msimamo wangu ni kuwa wagombea wote wana haki sawa na sanduku la kura ndilo litaamua nani ataongoza mpira wetu kwa kipindi cha 2017-2021.


Wagombea wote ninawatakia kila la kheri na Mola awabariki na kuwaongoza.


Ahsanteni

Jamal Emil Malinzi

Rais wa TFF

TFF YARAHISISHA UPATIKANAJI FOMU ZA UCHAGUZI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia wanafamilia wote wa mpira wa miguu wenye nia ya kuwania uongozi kuwa limewarahisishia namna ya kupata fomu baada ya tovuti ya TFF: www.tff.or.tz kuwa kwenye marekebisho.


Kwa wanafamilia ambao wapo nje ya Dar es Salaam, wanaotaka fomu hizo kwa sasa hawana budi kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwenye anwani ya info@tff.or.tz na moja kwa moja atajibiwa kwa kupata fomu hizo ziliazoanza kutolewa leo Juni 16, mwaka huu. Kwa walioko Dar es Salaam, wanaweza kupata fomu hizo katika ofisi za TFF zilizo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.


Mwanafamilia wa mpira wa miguu mwenye nia ya kugombea ataweza kufungua fomu hizo na kuzijaza huku akifuata utaratibu wa kulipia kwenye nambari ya akaunti 01J1019956700 katika Benki ya CRDB.


Zoezi hili kuchukua fomu na kuzirejesha fomu lililoanza leo Juni 16, litafikia kikomo Juni 20, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya 10.8 ya Uchaguzi kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya TFF.


Mara baada ya kulipia, Mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na kupewa fomu ya nafasi husika.


Gharama za kuchukulia fomu ni.

1.   Rais TSHS 500,000/=

2.   Makamu wa Rais TSHS 300,000/=

3.   Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/=


RAIS MALINZI AMSHUKURU MGOYI


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi amempongeza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ahmed Mgoyi kwa utumushi mara baada ya kutangaza kutowania nafasi yoyote ya uongozi.


Mjumbe Mgoyi anayewakilisha Mikoa ya Kigoma na Tabora aliandika waraka jana Juni 15, 2017 akielezea kutogombea tena katika Uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.


“Nimefanya kazi na Wajumbe wangu wote wa Kamati ya Utendaji. Tumefanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Wakati Tukielekea kwenye uchaguzi, mwenzetu ametangaza kutogombea tena, lakini kwa namna nilivyofanya naye kazi, kwangu mimi naamini anahitajika mno, lakini uamuzi wake ni mwisho unakuwa ni wa kwao.


“Naamini kwamba bado ni mwanafamilia wa mpira wa miguu na pindi atakapohitajika kwa lolote lile kama vile ushauri na masuala mengine, basi hatutasita kuwafuata kwa sababu lengo ni kujenga na kuendeleza mpira wetu,” amesema Malinzi.


Katika ujumbe wake, Rais Malinzi amesema kwamba hadhani kama Mgoyi hao atasita au kukataa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa shirikisho pindi akihitajika kutoa msaada wao wa mawazo na ushauri.


Rais Malinzi amemtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine aliyojipangia kuyafanya huku akiwa bado mwanafamilia wa mpira wa miguu.

PONGEZI KWA FRANCIS AMIN MICHAEL


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, amempongeza Francis Amin Michael kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Sudan Kusini (SSFA).


Amin - Mfanyabiashara aliyepata kuwa Mjumbe wa Bodi ya timu Atlabara FC, alishinda nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Juba ambako aliwashinda Lual Maluk Lual na Arop Joh Aguer baada ya kuvuna kura 22 kati ya 34.


Amin anamrithi Chabur Goc Alei, ambaye hakutetea nafasi hiyo.


Katika salamu za pongezi, Rais Jamal Malinzi amesema kwamba ana imani na Amin katika nafasi hiyo kwa kuwatumikia vema Wana Sudan Kusini kama alivyoahidi mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.


Rais Malinzi anaamini kwamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Serikali ya Sudan Kusini, ataendeleza mpira wa miguu hususani katika Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ambako Tanzania na Sudan Kusini ni nchi wanachama.

MGOYI ASEMA HATARAJII KUGOMBEA TENA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TFF



Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na mwenye Ukarimu
 
TFF inaelekea kwenye Uchaguzi wake mwingine  ambao tunategemea kuundwa kwa safu nyingine ya Uongozi itakayoendeleza Gurudumu la Soka nchini.

Binafsi naomba kuchangia muda nanyi kuwasilisha *SHUKRANI* zangu za dhati kabisa kwa Wadau wote wa soka tulioshirikiana kwa njia moja ama nyingine katika kipindi chote cha miaka 13 ambacho nilichaguliwa na kuhudumu kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwenye chaguzi zote tatu nilizoshiriki ambapo kwa mara ya kwanza nikiingia nikiwa Mjumbe mwenye umri mdogo zaidi kuliko wote. Aidha kuomba radhi kwa mapungufu yoyote na yaliyotokana nayo kwa kipindi chote hicho:

Nawashukuru sana wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF katika Chaguzi tatu za TFF kuonyesha Imani na mimi na kunichagua kwa kishindo cha kura nyingi sana kwa nyakati zote hizo.

Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake chini ya Rais Jamal Malinzi kwa ushirikiano uliotukuka na nitawakumbuka sana kwa mengi mchanganyiko.

Namshkuru binafsi Leodegar Chilla Tenga aliyenijenga kuwa Kiongozi imara wa Mpira.

Nawashukuru ma-Rais wote wawili niliofanya nao kazi (Tenga na Malinzi) makamu wao na Kamati zao za Utendaji kwa kuniamini kwa nyakati tofauti kunifanya kuwa msimamizi wa shughuli kadhaa miongoni mwa shughuli za TFF.

Navishukuru vyombo vya habari na wanahabari kwa ushirikiano wakati wote.

Naishukuru klabu mashuhuri, Wana Kinyamtula, Never say Die, The Uncolonized, Watoto wa Jiji,  *Ashanti United* niliyoingoza kama Meneja wa timu mpaka Rais wake kwa zaidi ya miaka 20 kwa kunisaidia sana kunijenga kiUongozi na kuniongezea Uthubutu.

Nawashkuru wadau wa Mpira wa Kigoma kwa kuniamini na kunifanya kuwa sehemu ya Uongozi wa Mpira.

Nawashukuru Vilabu vyote vya VPL, FDL, SDL na RCL kwa ushirikiano navyo kwa nyakati tofauti tofauti.

Nawashkuru wafanyakati wote wa TFF na timu za Taifa nilioshirikiana nao kwa nyakati tofauti.

Naishukuru sana Serikali na watendaji wa serikali kwa ushirikiano wakati wote.

Nawashkuru wadhamini na watendaji wa wadhamini wa TFF niliofanya nao kazi kwa nyakati tofauti.

Shukrani zangu zinatokana na yaliyopita na bado naendelea kuamini nitaendelea kushirikiana na nyanja zote kama sehemu ya familia ya Mpira wa Miguu.

Najisikia Fahari sana kuwa sehemu ya Ujenzi wa TFF katika mifumo thabiti na kuwa sehemu ya Usimamizi wa Mafanikio ya Mabadiliko Chanya ya Shuguli za TFF  bila ya kujali na kuthamini Changamoto za Utii na Uendeshaji zinazosababishwa na kutokana nazo.

Naomba kwa dhati kabisa na nikiendelea kuamini kwenye kuhuishwa na kuendelezwa na kufanywa kwa weledi zaidi kwa mema  yaliyopangwa na kufanywa na TFF kwa vipindi vyote nilivyokuwepo na wakati mwingine ikiwemo Ulinzi kwa Mifumo na Misingi ya kiTaasisi iliyowekwa,  Matumizi sahihi ya Vyombo vya TFF, Uthubutu na Mafanikio kwa Uendelezaji wa Soka la Vijana na Wanawake, Muundo wa Uendeshaji wa Mashindano yetu na Mafunzo.

Pamoja na kuwa bado nina nguvu uwezo na sifa za kuendelea kugombea, lakini pia nimeamini ni wakati wa kutoa nafasi pana zaidi kwa wengine kugombea na kuwa badala yangu na heshima kwa fikra nyinginezo. Na ninaondoka nikiwa mjumbe wa muda mrefu zaidi ya wote kwenye Kamati ya Utendaji inayokamilisha kipindi cha kikatiba na kwa dhati kabisa naamini kwenye kutoa nafasi kwa wengine.

Nawaomba radhi wale wote ambao wangependa au kutarajia ningekuwa miongoni au wakiendelea kuamini kuwa nilistahili kuwa sehemu ya wagombea.. nawashukuru kwa imani yao kwangu na bado nipo nao pamoja, pamoja na wale ambao hawaamini hivyo kama sehemu ya familia ya Mpira wa Miguu Tanzania na kwingineko.

Nawatakia kila la kheri wagombea wote na kwa nafasi na uzoefu wangu najishawishi kuamini kwamba wagombea wote watakuwa wamejipima vya kutosha na kuzihakiki dhamira zao, wamejiridhisha na wanavyoijua TFF, ukubwa wake na shughuli zake, wamefuatilia na kutambua vema mahitaji ya mpira wetu, wametathmini changamoto, madhaifu na makusudi ya kiuongozi na wapo tayari kwa mabadiliko, wametambua maeneo TFF inayofeli au hayajafanywa vema zaidi na wanaamini kwenye kuwa sehemu ya ufumbuzi, wamezikataza nafsi zao kufuata matamanio ya mapenzi ya timu zao, wanafahamu nguzo kuu za mpira wa miguu na changamoto zinazozikabili na namna ya kuzitatua, utayari wao kujitolea kwa hali na mali, kuheshimu miiko ya kiUongozi na kuimarisha nidhamu na Uadilifu.

Nimesukumwa kutoa Ushauri wangu huu kwa kuendelea kuathiriwa na kutoamini sana kwenye Utekelezaji na Udhibiti wa  kimfumo wa kupatikana kwa Viongozi wa Mpira hasa katika ngazi za juu kama hizi zinazokwenda kugombewa.

Kila la kheri Wagombea.
Ramadhani Kareem
Nawashukuru sana.
Ahmed Iddi Mgoyi
Mjumbe Kamati ya Utendaji TFF (Kigoma na Tabora 2004-2017)
13 Juni 2017.

Thursday, June 15, 2017

SIMBA WAMSAJILI KIPA WA MBAO FC



Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kufanya fujo za kuwasainisha mikataba wachezaji kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa VPL pamoja na mashindano ya kimataifa (CAF Confederation Cup).

Simba imemtambulisha golikipa wa Mbao FC Emanuel Elius Mseja baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Golikipa huyo alikuwa ni namba tatu katika klabu ya Mbao akiwa nyuma ya Musa Ngwegwe ambaye badae alisimamishwa akituhumiwa kwa upangaji matokeo baada ya timu yake kupoteza mchezo dhidi ya Yanga na huku golikipa namba mbili akiwa ni Benedict Haule ambaye amesaini mkataba wa kujiunga na Azam FC.

Kusajiliwa kwa golikipa huyo kunaifanya Simba kuwa na magolikipa watano (Daniel Agyei, Peter Manyika, Denis Richard, Emanuel Elius Mseja pamoja na Aishi Manula ambaye ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Kwa maana hiyo, lazima baadhi ya wachezaji wa nafasi hiyo waonde kwenye ili kupisha ujio wa Aishi Manula na  Emanuel Elius Mseja.

YANGA YAANZA KUFURU,YASAJILI BEKI KISIKI WA ZANZIBAR

Mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ‘VPL’, Yanga SC, wameanza kufuru ya usajili baada ya kunasa beki kisiki toka visiwani Zanzibar

Mlinzi mahiri wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar, Abdallah Haji Shaibu maarufu kwa jina la “Ninja” amesaini mkataba wa miaka miwili (2) kuichezea Yanga.

MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA STARS CHA COSAFA



Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga, leo Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi  Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania – mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki.

Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

Kwa mujibu wa Mayanga, kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).

 Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.

Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC)

UTARATIBU MPYA WA USAJILI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI WAJA

Baada ya kufutwa utaratibu wa mawakala ‘agents’ wa wachezaji wa kulipwa, Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), lilitangaza utaratibu mpya wa kukasimu majukumu hayo kwenye ngazi ya mashirikisho kwa kila taifa.

Hivyo kwa mwaka 2016/2017, hakuna usajili wala uhamisho uliofanywa na watu wa kati yaani intermediaries wanaotambulika na TFF.

TFF – Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, linakwenda sambamba na utaratibu huo wa mabadiliko na kwa sasa linakamilisha mipango ya kusajili watu wa kati wa usajili watakaofahamika kama intermediaries.

Usahili wa kati utatangazwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kitakachojadili kanuni za watu wa kati hapo baadaye.

AZAM FC WATHIBITISHA KUONDOKA KWA MANULA NA KAPOMBE


Uongozi wa timu ya Azam FC umethibitisha taarifa ya wachezaji wake Aishi Manula na Shomari Kapombe kusajiliwa na mabingwa wa michuano ya FA timu ya Simba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Mwenyekiti wa klabu ya Azam Iddrisa Nassoro alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi wa klabu hiyo hawana kinyongo na wachezaji hao katika harakati za kuondoka kwao kwani ni moja ya kuendelea kusaka mafanikio kwa upande kwao.

Aidha Nassoro alisema kwamba uongozi unawashukuru wachezaji hao kwa ushirikiano wao ambao wameuonyesha tangu walipojiunga na Azam kwani kwa njia moja walifanikiwa kuipa maendeleo timu hiyo.

Alisema kwamba kwa sasa kwao wanaendelea kuifanyia kazi taarifa ya mwalimu mkuu kuhakikisha wanatimiza matakwa yake ikiwemo kusajili wachezaji ambao watakuwa na chachu ya mafanikio kwa klabu.
Kapombe-Azam

Kapombe na Manula wamejiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili kwa kila mmoja huku ikielezwa kila mmoja amesajiliwa kwa dau la shilingi milioni 50.

MZEE AKILIMALI ATANGAZA KUWANIA NAFASI YA MWENYEKITI YANGA

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
 

Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache zilizopotia.
Lakini pia maamuzi hayo ya Manji  yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.
Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.
Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.
“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.
“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.

“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,” alisema Akilimali.

Tuesday, June 13, 2017

KUGOMBEA URAIS TFF SHILINGI 500,000, UCHAGUZI KUFANYIKA AGOSTI 12- DODOMA


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.

Akitangaza tarehe hiyo mbele ya wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli, amesema kwamba kamati yake haitakuwa na huruma kwa ishara yoyote ya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
 
“Napenda kuwatangazia wadau wote wa mpira wa miguu kuwa mnakaribishwa kugombea nafasi zilizo orodheshwa hapo chini kwa kuchukua fomu Ofisi za TFF Karume Ilala na pia unaweza kuzipata katika tovuti ya TFF: www.tff.or.tz,” amesema Kuuli.

Wakili Kuuli amesema kamati yake itandesha uchaguzi huo kwa Uhuru na Haki na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zote zilizopo.

Kuuli, amesema Kamati yake itafanya kazi na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na jeshi la Polisi kuhakikisha uchaguzi huo hautakuwa na vitendo vya rushwa.

“Tunawatahadharisha wagombea woye kukaa mbali na vitendo vya rushwa…, kamati yetu haitakubali vitendo hivyo na tutafanya kazi na mamlaka za Serikali kuhakikisha yeyote atakayehusika na vitendo hivi anachukuliwa hatua, Takukuru wataufuatilia kwa karibu uchaguzi huu,” alisema Kuuli.

Akizungumzia mchakato mzima, Kuuli anasema, mchakato wa kuchukua fomu na kuzirejesha ni Juni 16 mpaka 20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mkapa Juni 23.

Juni 24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.

Kwa mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai 4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya kimaadili.

Julai 15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya  masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29 mpaka Agosti 2.

Wagombea watajulishwa matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.

Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita;

Mara na Mwanza;

Shinyanga na Simiyu;

Arusha na Manyara;

Kigoma na Tabora;

Katavi na Rukwa;

Mbeya na Iringa;

Njombe na Ruvuma;

Lindi na Mtwara;

Dodoma na Singida;

Pwani na Morogoro;

Kilimanjaro na Tanga na

Dar es Salaam ambayo ni kanda pekee.

Sifa za wagombea

GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.

1.   Rais TSHS 500,000/=

2.   Makamu wa Rais TSHS 300,000/=

3.   Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-


SIFA ZA WAGOMBEA.

        1. Awe raia wa Tanzania.
        2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha   Elimu ya Sekondari).
        3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
        4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
        5. Awe na umri angalau miaka 25.
        6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
        7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
        8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni.

TAIFA STARS SASA YAJIANDAA NA COSAFA


Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Afrika Kusini, Juni 20, mwaka huu.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo.

Kocha kesho atafanya uteuzi wa wachezaji wengine atakaowajumuisha kwenye kikosi chake, atafanya mabadiliko kidogo hivyo  kesho atatangaza majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kujiandaa na michuano hii ya Cosafa inayoanza Juni 25 huko Afrika Kusini.

Wakati huo huo, awamu ya pili ya kozi ya Daraja A inayoendeshwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeanza leo kwenye ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Kozi hiyo inahusisha makocha 20 ambao walishiriki kwenye kozi hiyo ya awamu ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba, mwaka jana.

Mkufunzi wa kozi hiyo ni Mtanzania Sunday Kayuni ambaye pia atakuwa na wataalam wa masuala ya Lishe, Masoko, Tiba, Habari, Bima pamoja na mtaalam wa masuala ya upingaji wa matumizi ya utumiaji wa dawa ả kuongeza nguvu michezoni.

Monday, June 12, 2017

GOR MAHIA YATWAA UBINGWA KOMBE LA SPORTPESA, SASA KUCHEZA NA EVERTON JULAI 13- DAR


SportPesa imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa Uingereza, Everton. 

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.

Tangazo hil limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Muu wa masoko wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi wa Everton FC, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Murugenzi wa Michezo Yusuph Singo, Rais wa TFF Jamal Malinzi na wanahabari. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SportPesa ilitangaza Mei 24 kwamba michuano ya SportPesa Super Cup itafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikishirikisha timu nne (4) za Tanzania dhidi ya timu nne (4) kutoka Kenya. Timu sita (6) kati ya zitakazoshiriki michuano hiyo ni klabu washirika rasmi wa SportPesa. Simba SC, Young Africans SC na Singida United FC ni washirika wa SportPesa Tanzania wakati Nakuru All Stars, AFC Leopards na Gor Mahia ni washirika wa SportPesa kutoka Kenya. 

Tusker FC ndiomabingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa ya Kenya wakati Jang’ombe Boys FC ni vinara katika Ligi Kuu ya Zanzibar.

Akifurahia ujuio wa Everton, Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov alisema; “Tunafuraha kuwakaribisha Everton nchini Tanzania, ziara yao itakuwa na manufaa siyo tu kwa klabu za hapa zitakazopata fursa ya kucheza na mabingwa hao mara 9 wa Ligi Kuu ya England, bali pia na taifa zima kwa ujumla.

“Katika ziara hiyo tutashirikiana kufanya shughuli kadhaa za kurudisha kwa jamii.

“Tanzania inapaswa kujiandaa kupata uzoefu  mkubwa kutokana na uwepo wa Everton mjini hapa.”

Robert Elstone, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton alisema: “Maandaizi ya mwanzo wa msimu mpya ni kipindi muhimu sana kwetu kwani kwa kocha Ronald Koeman na benchi lake la ufundi wakiwaandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mkubwa ujao. Kuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kuja kucheza Tanzania itakuwa ni sehemu muhimu ya maandalizi hayo.

“Tunafungua milango mipya na hatuna shaka kwamba tutapata marafiki na kuongeza mashabiki wetu kkmataifa tutakapokuja Julai.

“Najua Ronald Koeman na wachezaji wanajiandaa kuja kucheza mechi nzuri dhidi ya moja ya klabu bora ya Afrika Mashariki.”

SportPesa tangu ilipozinduliwa Tanzania Mei 9, 2017, imethibitisha nia yake ya kufanya mapinduzi ya soka nchini hapa kwa kuzidhamini klabu tatu za soka, ikichangia Sh. Milioni 50 za Kitanzania katika kuisapoti timu ya taifa ya vijana ya U-17 Serengeti Boys ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya AFCON ya vijana nchini  Gabon, imetangaza michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inaweza kuwakutanisha miamba wa soka wa Tanzania, Yanga na Simba katika nusu-fainali /au fainali, na pia kumshuhudia bingwa wa Kombe la SportPesa akiwavaa miamba hao wa Uingereza.

Sunday, June 11, 2017

SARE YA STARS DHIDI YA LESOTHO YAMKERA SAMATTA, ASEMA UWANJA WA AZAM HAUKUPASWA KUTUMIKA KWA MECHI HIYO





NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema amekerwa na matokeo ya sare waliyoyapata kutoka kwa Lesotho katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za 2019.

Samatta amesema haikuwapo kwenye akili yake Taifa Stars kupata sare katika mechi hiyo ndio sababu wachezaji wote walipatwa na hasira baada ya mechi hiyo kumalizika.

Katika mechi hiyo iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam, Taifa Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Lesotho, matokeo ambayo yaliwachukiza mashabiki wengi wa soka nchini.

“Kitu ambacho kimewasaidia Lesotho ni uwanja kuwa mdogo. Na kuhusu hasira, mimi sipendagi kushindwa, hata sare sijaifurahia kwa sababu tulikuwa tunacheza nyumbani na tulikuwa tunahitaji ushindi kwa lazima,” alisema Samatta, alipozungumza na waandishi wa habari baada ya pambano hilo kumalizika.

“Haikuwa katika akili yangu kupata sare, nafikiri wachezaji wote walikuwa na hasira, sio mimi peke yangu, labda kwa sababu nilishindwa kujizuia kuionyesha, lakini hakuna mtu aliyeyafurahia matokeo,” alisisitiza Samatta.

Samatta pia alilaani staili ya ukabaji wa mabeki wa Lesotho, akisema walikuwa wanamfuata watatu kwa wakati mmoja hadi kuna wakati akajikuta anakasirika.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema mabeki wake walifanya kosa kubwa kuruhusu goli la kusawazisha la Lesotho.

“Tumefanya makosa kuruhusu goli rahisi la Lesotho, lakini sare ya leo haitukatishi tamaa na tutaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya mechi zilizosalia. Naamini makosa ya leo tutayafanyia kazi na tutazinduka, tutafanya vizuri,”alisema Mayanga.

Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki wachache kutokana na kuchezwa usiku na pia umbali wa mahali uliko uwanja, Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao
dakika ya 27 kupitia kwa Samatta, kwa shuti la mpira wa adhabu, baada ya beki wa kushoto, Gardiel Michael kuangushwa nje ya boksi.

Lesotho, maarufu kwa jina la Mamba, walisawazisha dakika ya 34 kupitia kwa Thapelo Tale aliyeunganisha pasi nzuri ya Jane Thaba-Ntso baada ya mabeki wa Taifa Stars kujichanganya.

TFF YAJITETEA KUHUSU SAKATA LA KUWATELEKEZA VIJANA WA SERENGETI BOYS


Kuna taarifa zimekuwa zikienea na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatelekeza wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Wadai kwamba eti hawakulipwa posho na kushutumu viongozi wa juu wa shirikisho kuhusu jambo hilo. Hizi taarifa si za kweli.

Aidha, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwajulisha wazazi na umma kwa ujumla kwamba vijana wetu walilipwa posho zao zote wakiwa kambini Morocco na Cameroon na zile za mashindano ya AFCON nchini Gabon.

Vilevile, Shirikisho linafanya taratibu za kupeleka maombi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund FDF) ili kuweza kuwalipa vijana na benchi la ufundi sehemu ya posho zilizokuwa bado hazijakamilishwa wakati wa michuano ya kufuzu kwa AFCON 2017.

Tumeshtushwa na taarifa hizo ambazo tafsiri yake ni kuharibu uhusiano mwema kati ya shirikisho, wazazi na wachezaji ambao wanatarajiwa  kuitumikia timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka  20 maarufu kama Ngorongoro Heroes.

Shirikisho linaendelea kuwatambua vijana wa Serengeti Boys kwani bado ni sehemu ya kikosi cha Ngorongoro Heroes na hivyo ukifika wakati wataitwa kambini kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya U-20.

TFF inazidi kuushukuru umma ambao umeendelea kuchangia Mfuko wa FDF ambao kimsingi kazi yake ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira.

Tunaomba michango iendelee kwani bado tuna changamoto za mashindano mbalimbali kwa timu za wanawake na vijana ikiwemo fainali za wanawake Afrika zitakazofanyika Ghana hapo mwakani kwa timu ya Twiga Stars na AFCON 2019 kwa Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji.

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira – FDF ulianzishwa kwa lengo la kutafuta rasilimali za maendeleo ya mpira wa miguu hasa kwa wanawake na vijana pamoja na miundombinu ya mchezo huo.

Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando anayeongoza Bodi na Mtendaji Mkuu (CEO) ni Bw. Dereck Murusuri anayesimamia sekretarieti.

TFF YATANGAZA KUANZA KWA DIRISHA LA USAJILI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano wa 2017/2018.

Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15, mwaka huu na litafungwa Agosti 6, mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano tajawa hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa.

Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa.