'
Friday, January 29, 2016
MWESIGWA AFUNGUA KOZI YA MAKOCHA WA SOKA YA WANAWAKE
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level Coaching Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia vyema fursa hiyo adimu waliyoipata.
Mwesigwa amewataka washiriki kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na kwenda kuwa walimu wa mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko kwa wanawake wengi kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.
Aidha Mwesigwa, amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya mkufunzi, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri kwao kupata nafasi ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema atatumia uwezo wake wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza na kuelewa vizuri mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri watakapokwenda kuanza kufundisha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike kutaongeza mwamko wa wanawake kuucheza mpira wa miguu.
Jumla ya washiriki 25 wanashiriki kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni Fatuma Omary, Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo John, Berlina Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia Mkumba, Marry Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.
Wengine ni Veneranda Mbano, Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid, Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu Malogo, Komba Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy Kimaro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment