'
Tuesday, August 9, 2016
DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA, YANGA, COASTAL UNION ZASHINDWA KUREJESHA FOMU KWA WAKATI
Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.
Hadi dirisha linafungwa, timu kadhaa hazikuwasilisha kabisa usajili wake licha ya kukumbushwa kwa njia mbalimbali na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Usajili wa msimu huu ni kama msimu uliopita kwamba unafanyika kwa njia au mfumo wa mtandao unaoitwa Transfer Matching System (TMS) ambao (server) yake au chombo chake cha kutunza kumbukumbu kipo Makao Makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) - Uswisi.
Kwa kawaida mfumo huu upo chini ya FIFA na TFF hutoa taarifa kwa FIFA tarehe ya kufungua dirisha la usajili na kufunga.
Mfumo huu uhusisha pande tatu ambazo ni klabu, shirikisho (TFF) na FIFA. Kimsingi kazi ya usajili hufanywa na klabu ambako inajaza fomu kwa njia ya mtandao na hupakia viambatanisho kama vile mikataba ya wachezaji na picha za wachezaji.
Zoezi hili hufanywa na Meneja Usajili wa klabu husika wakati shirikisho hufanya kazi ya kuhakiki na kuidhinisha tu na FIFA huratibu na kuusimamia mfumo mzima.
Kabla ya kutangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili hapo Juni 15, 2016 Shirikisho liliandaa kozi ya mafunzo ya usajili kwa klabu zote 64 zikiwa ni 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara; 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na timu 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.
Baadhi ya timu hazikutuma wawakilishi, lakini ziko zilizofanya jitihada za kuomba usaidizi kwa kufika ofisini TFF kuomba usaidizi wa kufanya usajili na zilifanikiwa. Kwa Young Africans, licha ya kuwa hapa Dar es Salaam, haikuomba usaidizi wowote na hata walipokumbushwa kuhusu suala la usajili, hawakujibu kitu.
Young Africans ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo msimu wa 2014/2015 na 2015/2016, ni moja ya vilabu ambavyo havikutuma mwakilishi kwenye kozi iliyofanyika Uwanja wa Taifa kwa siku tatu mfululizo ikigusa wawakilishi wa madaraja ya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.
Meneja wa TMS wa Young Africans ni Katibu Mkuu hakuwahi kupata mafunzo ya TMS.
Hivyo sasa klabu zote ambazo hakuzituma usajili wake, hazina budi kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.
TFF kwa sasa inasuburi barua ya utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume FIFA. Sambamba na hilo TFF inatathimini mwenendo mzima kisha itatoa taarifa kwa FIFA ili kuangalia namna gani ya kushughulikia maeneo yaliyokuwa na upungufu kwa sasa na baadaye.
TFF YAIPONGEZA SIMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii kuipongeza Klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa kufikisha umri wa miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kama ambavyo inaelezwa na viongozi wa sasa wa klabu hiyo.
Uongozi wa Simba SC kwa takribani miaka saba sasa, wamekuwa wakiazimisha siku ya Agosti 8, kila mwaka wamekuwa na wiki maalumu ya kuweka kumbukumbu ya kuanzishwa klabu hiyo ambako wanachama wao wanafahamu historia ya timu yao.
TFF tunasema kwamba hicho ni kitu kizuri, ambacho hakina budi kuenziwa kama ambavyo Simba hufanya kwa kushirikiana na jamii hasa kwa kufanya usafi katika mazingira mbalimbali, kutoa zawadi na kufanya ibada za kumbukumbu za waasisi wa klabu hiyo, wachezaji walioichezea Simba na kuipa mafanikio makubwa hususani kwa wale waliotangaulia mbele za haki.
Wito wetu ni kwamba Uongozi na wanachama wa Klabu ya Simba kuendeleze utamaduni huo wa kuadhikmisha wiki hadi siku ya Simba katika kuenzi historia ya klabu hiyo ambayo ina mchango wake mkubwa kwa soka la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Kila la kheri Simba Sports Club.
Sunday, August 7, 2016
YANGA WAMKABIDHI MANJI TIMU KWA MIAKA 10
WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.
Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo ukumbi wa Diamond jubilee, Dar es Salaam.
Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.
Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji. Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji

SERENGETI BOYS YAIDINDIA AFRIKA KUSINI
Ikicheza mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys leo imegoma kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji Afrika Kusini baada ya kuibana Amajimbos na kutoka sare bya bao 1-1.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini –Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini walianza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Linamandlia Mchilizeli kabla ya Ally Msingi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.
Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari.
Afrika Kusini iliyoanza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
Kubanwa katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendelea kuwabana Afrika Kusini waliokuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
Shukrani za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi akishirikiana na Dickson Job.
Shime maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya. Si mabaya kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”
Kwa upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi. Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”
Katika mchezo huo, Kikosi cha Serengeti kilikuwa: Ramadhani Kbawili, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Shaban Ada, Kelvin Naftal, Ally Ng’anzi, Ibrahim Abdallah/Muhsin Makame (Dakika ya 72), Asad Juma na Mohammed Rashid.
Afrika Kusini: Glen Tumelo, Mswati Mavuso, Luke Donn, Sechaba Makoena, Kwenzokuhle Shinga, Mjabulise Mkhize, Bonga Dladla, Linamandla Mchilizeli, Luke Gareth, James Monyane na Siphamandla Ntuli.
Saturday, August 6, 2016
KILA LA HERI SERENGETI BOYS LEO
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inajitupa dimbani kumenyana na timu ya vijana wa umri huo ya Afrika Kusini.
Pambano hilo limepangwa kuanza saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Kusini, sawa na saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, aliyefuatana na timu hiyo nchini Afrika Kusini, amesema mapema leo asubuhi kuwa, vijana wamejiandaa vyema kwa mechi hiyo na wanauhakika mkubwa wa kuibuka na ushindi.

Wednesday, August 3, 2016
KLABU ZAKUMBUSHWA KUWASILISHA MIKATABA YA WACHEZAJI VPL, FDL
Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 68(8) inataka kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Ni matarajio yetu kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.
Kadhalika, kwa mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linakumbusha kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili.
Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji mtakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 67(8) inataka kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Pia katika hili tunategemea kila timu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu.

PONDAMALI, MANYIKA DARASANI TFF
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limeipa nafasi Tanzania kuwapa mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping Coach Course), ikiandika historia kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa makocha wa nafasi hiyo baada ya Botswana.
Makocha wa makipa 25 hususani wa wa timu za taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanahudhuria kozi hiyo inayoongozwa na Alejandro Heredia ambaye ni Mkufunzi kutoka FIFA.
Makocha hao ni Peter Manyika (Taifa Stars ya Tanzania), Saleh Ahmed (Zanzibar Heroes); Muharami Mohammed (Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys); Mohammed Silima (Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar) na Elyutery Mhoery (Timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars) na msaidizi wake ambaye pia anachezea JKT Queens, Fatuma Omary.
Wengine ni makocha maarufu wa makipa wakiwamo Juma Pondamali (Young Africans); John Bosco (Majimaji ya Songea); Salimu Tupa (Tanga); Bakari Ali Hamadi (Wete Pemba – Zanzibar); Hafidh Muhidin Mcha (Mkoani Pemba – Zanzibar); Mussa Wanena (Kagera Sugar); Juma Bomba (African Lyon), Adam Abdallah Moshi (Simba SC), Idd Mwinchumu (Azam FC) na Hussein Tade (Seeb Club-Oman/Toto African)
Pia wamo Khalid Adams (Mwadui FC); Josia Steven (Mbeya City); Herry Boymanda (Tanzania Prisons); Emmanuel Mwansile (Polisi Morogoro); Ben Kalama (Stand United); Abdallah Said (JKT Ruvu); Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar); Augustin Malindi (Mkoa wa Kigoma); Raphael Mpangala (Ndanda FC); Salimu Tupa (Tanga) na Abdul Mgude (Coastal Union ya Tanga).
“Mjione kwamba mmepewa kipaumbele,” alisema Heredia akiwanoa makocha hao na kuongeza: “Kinachohitajika sasa ni juhudi tu. Kozi hii haijafanyika pengine hapa barani Afrika zaidi ya Botswana. Mjue kuwa mna bahati.”
Akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia aliishukuru FIFA na CAF kwa namna inavyoshirikiana na TFF katika kuwapa kozio nyingi za makocha wa timu kwa wachezaji wa mbele, makocha wa makipa na waamuzi wa madaraja tofauti.
“Hakuna kipindi TFF imepata kozi za makocha nyingi za makocha kama kipindi hiki cha uongozi wa Jamal Malinzi,” anasema Karia na kuongeza: “Tumetoka kwenye kozi ya makocha wa Daraja A sasa tuko kwenu. Lengo ni Tanzania kuwe na makipa wazuri. Ninyi mtaleta makipa wazuri. Na hii ni kwa manufaa ya sasa na baadaye kwa upende wetu, timu zetu na taifa kwa ujumla.”
Karia aliwatia hamasa makocha hao wanaoshiriki kozi hiyo kuwa, mara baada ya kozi hiyo ipo siku watakwenda kuwa wakufunzi nje ya mipaka ya nchi kadhalika makocha ambao wanaweza kupata kazi mahala popote duniani hasa ukizingatia walimu wa daraja lao wako Tanzania na Botswana tu.
Kadhalika, Makamu huyo wa Rais wa TFF alielezea kuwa mpira wa miguu una changamoto nyingi na nyingine husababishwa na watalaamu hao kubweteka kwa mafanikio. “Hili ni tatizo. Tubadilike kifikra na kivitendo. Msilaze damu, kuweni active (mahiri).”
TIMU YA OLIMPIKI YA TANZANIA YAENDA BRAZIL
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi bendera kwa timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1, 2016.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Zikiwa zimebaki siku chache kabla kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini Brazil inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya Agosti 4, 2016 katika mji wa Sao Paulo na Rio De Jeneiro nchini Brazil wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo wamepata baraka zote kutoka kwa Serikali na kukabidhiwa bendera ya Taifa kabla ya kwenda kuipeperusha nchini Brazil.
Akikabidhi bendera kwa timu hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura aliwataka washiriki wanaokwenda kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu huko Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili warudi na medali.
Mhe. Annastazia Wambura alisema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao.
” Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zenu kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi”.
Aidha Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi alisema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo limefanikisha kuweza kujifua vyema na kujiandaa ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani.
Akizungumzia mara baada ya kukabidhiwa bendera Kocha wa timu ya kuogelea Bw. Alexandra Mwaipasi alisema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni walikuwa na changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na mashindano hayo ili kwa matayarisho aliyowapatia wachezaji wake anahakika watarudi na medali.
Moja ya washiriki wa mchezo wa kuogelea katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 Magdalena Mosha alisema kuwa amejiandaa vizuri na anaamini kwa miaka aliyoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing na London yamempa uelewa zaidi wa nini anatakiwa kufanya na kuyafanyia kazi mazoezi aliyoyapata nchini Australia ili kurudi na ushindi.
Naye mmoja wa wawakilishi katika mchezo wa Judo, Adrew Thomas alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na yuko tayari kuiwakilisha Tanzania na kuleta ushindi na pia kuitangaza Tanzania katika michezo na utalii uliopo kwa kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini.
Kwa upande wake Sara Ramadhani ambaye ni mwakilishi mwanamke pekee katika mshindano hayo kwa wakimbiaji wa Marathon alisema yuko vizuri kuipeperusha bendera ya taifa na kuitangaza Tanzania kimataifa kwa kushindana na kushinda medali hivyo kuiletea sifa nchini.
Mmoja wa wadhamini wa safari hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.
Katika mchango wao kwa wawakilishi hao Kampuni ya ving’amuzi ya Dstv imetoa mchango wa kuwakutanisha pamoja kwa kuandaa hafla ya kuwaaga wawakilishi hao ikiwa ni moja ya kuwatia moyo waende kupambana na kushinda katika michezo mbalimbali na kuliletea sifa taifa.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yakioneshwa moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
Bodi ya Utalii nayo haikuwa nyuma kuwapa nguvu na morali wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa mataifa mbalimbali yanayoshiriki mashindano hayo kwa kuwapatia vifurushi kwa ajili ya kusambaza ujumbe kuhusu utalii wa Tanzania.
Akitoa nasaha zake kwa wawakilishi hao Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey Tengeneza aliwaasa wawakilishi hao kujituma kwa bidii na kutangaza nchi kupitia michezo na pia watumie fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania kwa kueneza habari kuhusu utalii Tanzania.
“Mtakapokuwa huko mbali na kushiriki katika michezo muitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili tuzidi kupata watalii wengi kutoka duniani kote”.
Timu ya Tanzania inayoenda kushiriki mashindano ya 31 ya Olimpiki nchini Brazil inawakilishwa na wachezaji saba ambao ni waogeleaji wawili Magdalena Mosha anayeenda kwa mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku Hilal Hilal akienda kwa mara ya kwanza kwa upande wa wanaume na wote watakuwa ni waogeleaji kwa umbali wa mita 50.
Wengine ni Fabian Joseph, Said Juma Makula na Alphonce Felix Simbu watakaokimbia marathon kwa wanaume na Sara Ramadhani ambaye ni mwanamke pekee anayeiwakilisha Tanzania katika mbio za marathon.
Na kwa upande wa mchezo wa Judo Tanzania itawakilishwa na Adrew Thomas Mulugu katika uzito wa kilogramu 73.
Katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu takribani M yanatarajiwa kushindana katika michezo mbalimbali huku Marekani ikiongoza kuwa na wachezaji wengi zaidi katika mashindano hayo ikiwa na wachezaji 550 ikifuatiwa na Brazil iliyo na wachezaji 450 na China inayowakilishwa na wachezaji 380.
MO DEWJI AMWAGA MILIONI 100 SIMBA KWA AJILI YA USAJILI
Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.
Chanzo Mo Blog

Monday, August 1, 2016
SIMBA YARIDHIA MO DEWJI KUKABIDHIWA TIMU KUIENDESHA
Hatimaye ile ndoto ya mashabiki wa klabu ya Simba kuona klabu yao ikibadili mfumo unaotumika sasa wa wanachama ndiyo kuwa wamiliki wa klabu na kuingia katika mfumo wa kampuni imekamilika.
Hilo limethibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva katika mkutano mkuu wa Simba ambao ulikuwa unafunga msimu wa 2015/2016 kwa kutolewa taarifa na kuweka mipango mipya kwa msimu ujao.
Hatua hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO” kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20 kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi katika makali ya kushinda mataji.
Sunday, July 31, 2016
WADAU WA SANAA WAHAMASISHWA KUDHAMINI MASHINDANO YA UREMBO
Miss Dar Indian Ocean aliyemaliza muda wake, Camilla John (katikati) akimvisha skafu Mshindi wa Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (kushoto) mara baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzie ambaye ni Mshindi wa pili na wa tatu mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuregenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro (kulia) akimpongeza Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
Wadau wanaojishughulisha na masuala ya Sanaa nchini wamehamishwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia maendeleo ya Sanaa kwa kudhamini na kufadhili mashindano ya urembo bila kubagua.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Anastazia Wambura ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 yaliyofanyika katika Ukumbi wa MRC uliopo Mikocheni jijini hapa.
Akiwasilisha hotuba hiyo, Songoro amesema kwamba kazi inayofanywa na wadau wa sanaa ni hatua ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ambayo inasisitiza jamii na wakuzaji sanaa kuendeleza ubunifu katika kazi za kiutamaduni.
Ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inathamini na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau hao hasa katika kukuza na kuviendeleza vipaji vya vijana nchini, hivyo amewapongeza wadau hao kwa moyo wao wa kujitoa na kuwataka kuendeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 katika Sura ya 9 kifungu cha 9:5:8 ambacho kinasisitiza na kuhimiza watu binafsi pamoja na Mashirika kuwekeza rasilimali katika sekta ya utamaduni.
‘’Maonyesho haya ni ishara tosha kuwa sanaa ni kazi, ajira, biashara na burudani, hivyo kipekee nawapongeza sana’’, alisema Songoro.
Aliongeza kuwa, Warembo ambao wameshiriki katika mashindano hayo wanautangaza utalii wa ndani na nje ya nchi na kwa kufanya hivyo wanaiwakilisha vyema Tanzania Duniani katika mashindano ya Miss World na pia kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, amewataka warembo ambao hawakubahatika kuibuka washindi katika mashindano hayo kutokata tamaa, bali waitumie fursa hiyo hususani ya elimu waliyoipata wakiwa kambini kwa kuisadia jamii inayowazunguka na kuwa wanawake wa mfano wa kuigwa katika kujitambua na kujiamini.
‘’Mtambue kwamba, siyo wote mtakaoibuka washindi na kuendelea mbele katika mashindano haya, niwaombe wale ambao hamtashinda msivunjike moyo, bali mkaitumie elimu mliyoipata na yale ambayo mmejifunza mkiwa kambini kwa kuisaidia jamii inayowazunguka na muwe wanawake wa mfano wa kuigwa’’, alisema Songoro.
Katika mashindano hayo, Mshindi wa Kwanza aliyeibuka na kunyakua taji hilo ni Jackline Kimambo ambaye alipatikana kati ya tano bora na kuvikwa taji la Miss Tanzania Indian Ocean 2016 na Mshindi wa pili ni Regina Ndimbo huku wengine waliobaki kwenye tano bora wamepata fursa ya kuingia katika mashindano ya Miss Kinondoni.
Shindano hilo lilihusisha jumla ya washiriki wapatao 20 ambapo mmoja kati yao ndiyo aliyeibuka mshindi na lilidhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo Mikocheni Resort Centre, Mlimani TV, Channel Ten, Darling, Helmic, Tanzania Breast Cancer Foundation, Magic FM, Jozi Lounge, Kiss Printers pamoja na NTS.

Saturday, July 30, 2016
MSIWE WACHOYO WA ELIMU – WALLACE KARIA
Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amewaagiza waamuzi wenye Beji kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kadhalika waamuzi waandamizi waliohitimu kozi leo Julai 29, 2016 kutokuwa wachoyo wa kutoa elimu waliyopata kwa wenzao wa madaraja ya kwanza, pili na tatu.
Karia aliyefunga kozi hiyo na kugawa vyeti kutoka FIFA kwa wahitimu 48, alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kufunga kozi hiyo iliyochukua takribani siku tano ambako sehemu ya mafunzo hayo ilikuwa ni kusoma baadhi ya marekebisho kwa msimu wa 2016/17.
“Tuna matagemeo makubwa kutoka kwenu, lakini nasema mfikirie kusaidia wenzenu ili kama si kumaliza matatizo kwenye soka basi yapungue, nasisitiza msiwe wachoyo, fundisheni wengine na muwape hamasa,” alisema Karia kwa niaba ya Rais Jamal Malinzi ambaye kwa sababu za majukumu, hakudhuria hafla hiyo.
Karia ambaye aliishukuru FIFA kuendelea kutoa kozi nyingi nchini, alisema kwamba tayari Tanzania imefaidika kwa kozi za makocha na makamishna, lakini akaagiza Idara ya Ufundi ya TFF chini ya Kocha Mkongwe, Salum Madadi kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa klabu na waandishi wa habari ambao ni sehemu kubwa ya familia ya mpira wa miguu.
Alisema kwamba umahiri wa makocha utakuwa chachu ya mafanikio ya soka la Tanzania kwa kutoa waamuzi bora watakaokuwa wakipata nafasi kubwa ya kuchezesha michezo mbalimbali ya mpira wa miguu.
“Mkifanya vibaya kwenye mashindano, mtakuwa mmejiharibia wenyewe na pia kupoteza sifa ya nchi,” alisisitiza.
Kozi za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania ilianza Julai 25, 2016 ambako iliendeshwa na wakufunzi Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe.
Leo Julai 29, 2016 limeanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017
TFF YAELEZA SABABU YA KUIBUA VIPAJI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amesema kutimia kwa malengo ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imesukuma kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano ya soka kwa vijana – wavulana na wasichana.
Selestine alisema hayo kwenye hafla ya kukabidhiana vifaa kwa Airtel kwenda TFF kabla ya kwenda kwa klabu shiriki iliyofanyika Ukumbi wa TFF, Dar es Salaam. Vifaa vilivyotolewa kwa timu jezi kamili ikiwa ni pamoja na jezi za waamuzi, viatu, mipira na vizuia ugoko kutopata madhara.
Alisema sababu hizo ni uhusiano mzuri kati ya TFF na Airtel inayotoa bora za mawasiliano kwa miaka sita sasa sambamba na kuendeleza vipaji kwani nusu ya wachezaji wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, wanatoka katika michuano hiyo ya mwaka jana.
Wachezaji hao ni Ramadhani Awm Kabwili, Nickson Clement Kibabage, Dickson Nickson Job, Ally Hamisi Ng’anzi, Syprian Benedictor Mtesigwa, Mohammed Abdallah Rashid na Muhsin Malima Makame na Katibu Mkuu alisema: “Hawa wamepita Airtel. Tunashukuru Airtel kwa kuingia katika zonal (ukanda) ambao wengi hawapendi kuingia.”
Selestine alisifu Airtel akisema imejitofautisha na taasisi nyingine na kuamua kwenda shambani au jikoni kulima au kupika chakula ambacho leo tunajivunia kuwa na kikosi bora na imara cha Serengeti Boys ambayo wiki ijayo itakuwa na mtihani dhidi ya Afrika Kusini.
Rai wa Karibu Mkuu, Selestine ni kwa viongozi kuratibu vema mashindano ya Aitel msimu huu kwa kufuata kanuni ambazo zilijadiliwa na kupitishwa mara baada ya kuzindua mashindano hayo. “Kama viongozi mmeingia kwenye mashindano haya na hujafuata au hujui kanuni ujue tu umejiandaliwa kushindwa.”
Kadhalika aliwataka wazazi na walezi kuwatia shime wachezaji ili wafanye vema kwenye michuano hii ili siku moja waingie kwenye ajira ya soka wakitokea mashindano ya kuibua vipaji ya Airtel. Pia alitaka wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo yatayosimamiwa na kuendeshwa na TFF katika mikoa mbalimbali.
Mikoa ambayo itazindua Mashindano hayo ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Morogoro, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa upande wa wavulana wakati wasichana mikoa iliyoteuliwa ni Lindi, Zanzibar, Arusha na Ilala, Kinondoni na Temeke.

Thursday, July 28, 2016
SERENGETI BOYS YATUA SALAMA MADAGASCAR
Msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es Salaam, Tanzania imetua salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba mshindi atakuwa amejiwekea mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew.
Pia yumo Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.

MAAGIZO KWA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa Wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha, madaktari na wachezaji kabla ya kuingia kandarasi.
Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa ya kuishi nchini, vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji na Serikali, lakini wakati huohuo kwa wachezaji nao kukatiwa leseni ya kucheza kutoka TFF.
“Mchezaji au mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yo yote anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu Mkuu nimepata taarifa kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa kuwa sisi ndio waratibu soka nchini, natakiwa kufuatilia,” amesema Selestine.
“Vilabu vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. Inawezekana hawahitajiki. Ni vema wakafanya uratatibu wa kuhakiki,” amesema.
Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, 2016 ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.

Wednesday, July 27, 2016
NAY WA MITEGO AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA KAZI ZA SANAA KWA MUDA USIOJULIKANA, ATOZWA FAINI YA TSH. MILIONI MOJA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.
Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.
Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.
Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.
Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake.
Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA
YANGA YAPIGWA THALATHA NA MEDEAMA YA GHANA
JAHAZI la Yanga limeendelea kuzama katika michuano ya soka ya Kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Medeama ya Ghana.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa imeshafungwa idadi hiyo ya mabao.
Hiyo ni mechi ya nne mfululizo kwa Yanga kushindwa kutoka uwanjani na kishindo katika hatua ya makundi ya michuano hiyo, ikiwa imefungwa mechi tatu na kutoka sare moja.
Mabingwa hao wa soka nchini walianza michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na Mo Bejaia nchini Algeria, kabla ya kufungwa bao 1-0 na TP Mazembe na kutoka sare ya 1-1 na Medeama mjini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Medeama ilijipatia mabao yake kupitia kwa Daniel Amoah dakika ya saba, aliyemalizia kona ya Enock Atta Agyei.
Bao la pili lilifungwa na Abbas Mohammed, dakika ya 23 kabla ya kuongeza la tatu dakika ya 37.
Yanga ilijipatia bao lake la pekee dakika ya 25 lililofungwa kwa njia ya penalti na Simon Msuva baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo lahatari.
Kipa Deo Munishi 'Dida' aliiokoa Yanga isiadhirike zaidi baada ya kuokoa penalti dakika ya 10 iliyopigwa na Malik Akowuah.
SERENGETI BOYS YAENDA KUWEKA KAMBI MADAGASCAR
Dua na sala za Watanzania zielekezwe pia kwa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, iliyoondoka leo saa 12.00 Uwanja wa Ndege ya Mwalimu Julius K. Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania kwenda Antananarivo, Madagascar kupitia Uwanja wa Ndege wa Ndege ya Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Serengeti Boys inayokwenda kuweka kambi huko Antananarivo, Madagascar inatarajiwa kufika huko saa 8.10 mchana. Timu hiyo inajiandaa kucheza na Afrika Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Serengeti ipo kwenye ushindani wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Wakati mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew pamoja na Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.
“Najua mchezo utakuwa mgumu, lakini nakiamini kikosi change. Kiko imara,” amesema Shime, maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
Serengeti Boys inayokwenda kuweka kambi huko Antananarivo, Madagascar inatarajiwa kufika huko saa 8.10 mchana. Timu hiyo inajiandaa kucheza na Afrika Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Serengeti ipo kwenye ushindani wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Wakati mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew pamoja na Juma Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.
“Najua mchezo utakuwa mgumu, lakini nakiamini kikosi change. Kiko imara,” amesema Shime, maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
Subscribe to:
Posts (Atom)