'
Thursday, February 12, 2015
BOBBI KRISTINA AFUNGUA MACHO
NEW YORK, Marekani
HALI ya mtayarishaji wa vipindi vya televisheni na mwanamuziki nchini Marekani, Bobbi Kristina Brown imeanza kutia matumaini.
Bobbi Kristina jana alifumbua macho, baada ya kulazwa kwa zaidi ya wiki moja kwenye chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU).
Taarifa hizo bila shaka ni njema kwa Wamarekani ambao kwa takribani wiki moja wako katika maombezi maalumu ya kumuombea nyota huyo ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa muziki, Bobby Brown.
Kinda huyo alikutwa ameanguka bafuni na chanzo cha tukio hilo kinafanyiwa uchunguzi na Polisi nchini humo ingawa mumewe, Nick Gordon, anatajwa kuhusika.
Shangazi wa Bobbi, Leolah Brown, amethibitisha taarifa za maendeleo mazuri ya mgonjwa huyo ambaye aliyekuwa mahututi tangu Januari 31 mwaka huu.
Alisema jana alikwenda kumuona katika Hospitali ya Emory University ambapo Bobbi alifumbua macho kwa mara ya kwanza.
Leolah alisema hali yake inaridhisha na familia ina imani nduyu yao atapona ingawa bado wanaendelea na maombi.
“Bado tuna majonzi makubwa lakini, Bobbi anaendelea vizuri na hali yake inatia matumaini kuwa huenda akapona na kurejea katika hali ya kawaida,” alisema shangazi huyo.
Juzi familia ya Bobbi iliwataka madaktari kuzima mashine inayomsaidia kupumua ili aweze kufa katika tarehe kama marehemu mama yake Whitney Houston.
Whitney alifariki dunia Februari 11, 2012 baada ya kukutwa ameanguka bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton na pembeni kukiwa na pakiti za dawa za kulevya.
MAZITO YAIBUKA SAKATA LA MSANII BOBBI KRISTINA
Mumewe apandishwa kizimbani, Yadaiwa alimpiga kabla ya tukio
NEW YORK, MarekaniMUME wa msanii Bobby Kristina, Nick Gordon, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu shitaka la makosa ya uzembe barabarani.
Pia mamalaka nchini hapa zinamchunguza kwa tuhuma za kumjeruhi, Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa mwanamuziki nguli wa zamani, Whitney Houston.
Marehemu Whiyney alizaa mtoto huyo na mwanamuziki mwingine mahiri, Boby Brown, ambaye ni gwiji wa kutumia dawa za kulevya.
Mahakama ya Fulton County State, leo inatarajia kutoa kibali cha kukamaktwa kwa Gordon iwapo atashindwa kuhudhuria kesi ya awali inayomkabili.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa kibali hicho ikiwa ni wiki moja tangu Bobbi Kristina, alipokutwa amepoteza fahamu bafuni huku kichwa chake kikiwa ndani ya sinki lililokuwa limejaa maji.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, polisi wa mjini hapa wamesema wana imani Gordon alimjeruhi mkewe kabla ya kutokea tukio hilo.
Tayari polisi wameanza kuchunguza mienendo ya uhusiano wa wawili hao, kabla ya Bobbi Kristina, kukutwa na tukio hilo, Jumamosi wiki iliyopita.
Aidha, mamlaka ya kiuchunguzi zimedai wanandoa hao wamekuwa na historia ya kushambuliana ambapo dakika 15 kabla ya tukio hilo walinaswa wakiwa kwenye malumbano makali.
Max Lomas ambaye ni rafiki wa Bobbi Kristina, alidai Gordon alifuta damu katika eneo la tukio zinazosadikiwa kuwa za mkewe.
Lomas alidokeza kuwa alilazimika kuingia nyumbani kwa Bobbi Kristina, baada ya kugonga mlango kwa muda kabla ya kuingia ndani baada ya kukosa mtu wa kumfungulia na kumkuta rafiki yake akiwa amepoteza fahamu bafuni.
Waaguzi katika hospitali aliyolazwa msanii huyo wa vipindi vya televisheni, wanasema hali yake sio nzuri na mjomba wake ameandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa hali ya mpwa wake haileti matumaini.
Mjomba huyo alisema madaktari walimwambia ajiandae kupokea taarifa yoyote kwa kuwa hakuna matumaini Bobbi Kristina, kuokoa uhai wake.
Hatua ya kupoteza fahamu, Bobbi Kristina, limeushtua ulimwengu kwa kuwa linafanana na tukio la kifo cha Whitney aliyefariki Februari 12, 2012.
Whitney alikutwa amefariki bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton huku kichwa chake kikiwa ndani ya maji.
Katika tukio hilo, polisi walikuta chupa za pombe, vyeti vya hospitali vilivyokuwa vikionyesha kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na matumizi ya dawa za kulevya aina ya kokein.
Gordon na Bobby Kristina, walifunga ndoa Januari, mwaka jana licha ya ndoa hiyo kupingwa vikali na Bobby Brown kwa kuwa Godon ni mtoto wa kuasili wa Whitney.
Wednesday, February 11, 2015
AZAM YAIPA MTIBWA KIPIGO CHA PAKA MWIZI
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam wamerejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.
Matokeo hayo yameiwezesha Azam kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Yanga, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Washambuliaji Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na kiungo Frank Domayo ndio walioiwezesha Azam kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele baada ya kuifungia mabao hayo matatu. Bao la Mtibwa lilifungwa na Mussa Nampaka.
Mabao mengine ya Azam katika kipindi cha pili yalifungwa na Domayo na Tchetche wakati bao la pili la Mtibwa lilifungwa na Abdalla Juma.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.
Matokeo hayo yameiwezesha Azam kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Yanga, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Washambuliaji Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na kiungo Frank Domayo ndio walioiwezesha Azam kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele baada ya kuifungia mabao hayo matatu. Bao la Mtibwa lilifungwa na Mussa Nampaka.
Mabao mengine ya Azam katika kipindi cha pili yalifungwa na Domayo na Tchetche wakati bao la pili la Mtibwa lilifungwa na Abdalla Juma.
Tuesday, February 10, 2015
TFF YAFANYA MAREKEBISHO KAMATI NDOGO ZA KISHERIA
JUDICIAL AND STANDING COMMITTEES.
Kamati ya Utendaji iliyoketi tarehe 19 Disemba 2014, ilifanya mabadiliko katika kamati ndogo ndogo na zile za kisheria. Kamati hizo ni kama ifuatavyo
KAMATI YA NIDHAMU
1. Tarimba Abbas (Mwenyekiti)
2. Advocate Jerome Msemwa ( Makamu mwenyekiti)
3. Kassim Dau
4. Nassoro Duduma
5. Kitwana Manara
KAMATI YA RUFANI YA NIDHAMU
1. Advocate Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti)
2. Advocate Revocatus Kuuli (Makamu mwenyekiti)
3. Abdala Mkumbura
4. Dr. Franics Michael
5. Advocate Twaha Mtengela
KAMATI YA MAADILI
1. Advocate Wilson Ogunde (Mwenyekiti)
2. Advocate Juma Nassoro (Makamu mwenyekiti)
3. Advocate Ebenezer Mshana
4. Geroge Rupia
5. Mh. Said Mtanda
KAMATI YA RUFANI YA MAADILI
1. Advocate Walter Chipeta (Mwenyekiti)
2. Magistrate George Kisagenta (Makamu mwenyekiti)
3. Lilian Kitomari
4. Advocate Abdala Gonzi
KAMATI YA UCHAGUZI
1. Advocate Melchesedeck Lutema
2. Advocate Adamu Mambi (Makamu mwenyekiti)
3. Hamidu Mahmoud Omar
4. Jeremiah John Wambura
5. John Jembele
KAMATI YA RUFANI TA UCHAGUZI
1. Advocate Julius Lugaziya (Mwneyekiti)
2. Advocate Machare Suguta (Makamu Mwenyekiti)
3. Idrisa Nassor
4. Paschal Kihanga
5. Benister Lugora
KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1. Wallace Karia (Mwenyekiti)
2. Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti)
3. Goodluck Moshi
4. Omar Walii
5. Ellie Mbise
6. Deo Lubuva
KAMATI YA MASHINDANO
1. Geofrey Nyange (Mwenyekiti)
2. Ahmed Mgoyi (Makamu mwenyekiti)
3. James Mhagama
4. Stewart Masima
5. Steven Njowoka
6. Said Mohamed
KAMATI YA UFUNDI
1. Kidao Wilfred (Mwenyekiti)
2. Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti)
3. Vedastus Rufano
4. Dan Korosso
5. Pelegriunius Rutahyugwa
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU YA VIJANA
1. Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti)
2. Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti)
3. Ali Mayay
4. Mulamu Ngh’ambi
5. Said Tully
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE
1. Blassy Kiondo (Mwenyekiti)
2. Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti)
3. Zena Chande
4. Amina Karuma
5. Zafarani Damoder
6. Beatrice Mgaya
7. Sofia Tigalyoma
8. Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati)
KAMATI YA WAAMUZI
1. Saloum Umande Chama (Mwenyekiti)
2. Nassoro Said (Makamu mwenyekiti)
3. Charles Ndagala (Katibu)
4. Kanali Issaro Chacha
5. Soud Abdi
KAMATI YA HABARI NA MASOKO
1. Athuman Kambi (Mwenyekiti)
2. Alms Kasongo (Makamu Mwenyekiti)
3. Rose Mwakitangwe
4. Amir Mhando
5. Haroub Selemani
KAMATI YA UKAGUZI WA FEDHA
1. Ramdhan Nassib (Mwenyekiti)
2. Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti)
3. Jackson Songora
4. Golden Sanga
5. Francis Ndulane
6. Cyprian Kwiyava
KAMATI YA TIBA
1. Dr. Paul Marealle (Mwenyekiti)
2. Dr. Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti)
3. Dr. Mwanandi Mwankewa
4. Dr. Eliezer Ndelema
5. Asha Mecky Sadik
KAMATI YA FUTSAL NA BEACH SOCCER
1. Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2. Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti)
3. Samson Kaliro
4. Shaffih Dauda
5. Boniface Pawassa
6. Apollo Kayugi
PRESIDENTIAL COMMISSION FOR AFFAIRS
1. Omar Abdulkadir (Mwenyekiti)
2. Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti)
3. Victor Mwandiki
4. Riziki Majala
5. Zahra Mohamed
6. David Nyandu
PRESIDENTIAL COMMISSION ON BUSINESS AND INVESTMENTS
1. William Erio (Mwenyekiti)
2. Mbaraka Igangula
3. Advocate Iman Madega
4. Lt. Col Charles Mbuge
5. Philemon Ntalihaja
KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI 600,000/-
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad, Mbarouk Kassanda kwa kuhusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao haukufuata kanuni za usajili.
Villa Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.
JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.
Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi
BEKI ALIYEMKABA KOO TAMBWE AFUNGIWA MECHI TATU
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.
Osei ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa kwa kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Mlalamikiwa alifika mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili ya Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia Ibara ya 96(3) ya Kanuni ya Nidhamu ya TFF Toleo la 2012.
Katika uamuzi wake, Kamati imesema kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni dhaifu, hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo, imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona, na Katibu wa Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.
Kwa upande wa Sorogo, Kamati imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa upande mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.
Badala yake aliyehusika ni Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua hatua dhidi yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya SIFA.
Pia barua ya kumsimamisha kocha huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa Mashindano. Kamati imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo maana hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi na yametupwa.
Kwa upande wa Galibona ambaye ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa alishiriki kuhamasisha marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa aliwasilisha vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.
Kamati imesema licha ya ripoti ya Saleh Mang'ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya refa huyo na msaidizi wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada ya tukio hilo hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.
Pia barua ya FAM kwenda TFF kuhusu matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa, hivyo Kamati imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na yametupiliwa mbali.
KLABU ZATAKIWA KUOMBA LESENI TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi jana Jumapili tarehe 08 Februari, 2015 katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na kujadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 na 15 mjini Singida, Kamati ilijadili na kuamua yafuatayo:-
1.Zoezi la utoaji leseni kwa vilabu litaanza kabla ya msimu wa ligi 2015/16. Vilabu vitatumiwa fomu za maombi mapema iwezekanavyo ili viweke nyumba zao sawa na kuleta maombi. Leseni za vilabu (club licence) ni agizo la CAF na FIFA katika kuhakikisha vilabu vinaendeshwa kwa weledi. Baadhi ya maeneo yanayoagaliwa katika utoaji wa leseni ni pamoja na kuwepo kwa Sekretarieti, miundo mbinu ya mazoezi na mashindano, hadhi za kisheria (legal status) mikataba ya ajira n.k.
2. Kamati ya Utendaji imeazimia kufanyika kwa mashindano ya Taifa Cup kwa upande wa
wanaume. Sekretarieti ya TFF imetakiwa kufanya juhudi ili mashindao hayo yaweze kufanyika.
3. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetoa pongezi kwa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii
(NSSF) kwa juhudi zake za kukuza soka la vijana kupitia mradi wake wa kuanzisha shule ya soka
(Academy) kwa ushirikiano na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Aidha Kamati ya Utendaji ya
TFF imeipongeza Kampuni ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa juhudi zao za
kuchangia maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu kwa ujumla ikiwa ni kupitia mpango
wa kujenga shule ya soka (academy) uwezeshaji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 13
(U-13) yatakayofanyika mwezi April, 2015 mjini Mwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya soka na
michezo kwa ujumla.
Kamati ya Utendaji imewaomba wadau wengine kufuata mifano hiyo na kuchangia maendeleo ya
soka kwani kazi hii inategemeana ni kwa faida ya wadau mbali mbali.
4. Kamati ya Utendaji ilipokea mabadiliko ya uwakilishi wa Chama cha Soka la Wanawake nchini (TWFA) yaliyotokana na kuondoka kwa Bi. Lina Kessy aliyekuwa Mwenyekiti wake. Bi. Lina ameajiriwa kama Afisa michezo wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia. Nafasi ya Mwenyekiti inachukuliwa na Bi. Rose Kisiwa ambaye hapo kabla alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TWFA ataendelea kuwa Mwenyekiti mpaka hapo utakapokaa Mkutano Mkuu wa kawaida wa TWFA.
5. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo kwa vitendo vya vurugu na utovu wa nidhamu katika mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini. TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu hususani viongozi wa vilabu kutilia mkazo elimu ya kujitambua ili wachezaji wajue kuwa wao ni hazina ya Taifa na kioo (taswira) cha jamii, hivyo waepuke vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja. Vitendo hivi si tu vinakwamisha maendeleo, bali pia vinawadharirisha wao, mpira wa miguu na jamii kwa ujumla.
Kufuatia matukio ya hivi karibuni na kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu
kwa haraka na weredi, Kamati ya Utendaji imeteua ya Kamati ya kuangalia na kusimamia kanuni
za uendeshaji Ligi. Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Bodi ya Ligi, Kurugenzi ya
mashindano, Kamati ya mashindano na kamati ya waamuzi.
TFF YATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA FIF
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF, Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la soka nchini Ivory Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
Katika salam zake Bw. Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika
yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa
huo wa Afrika kwa mara pili.
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za
rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha mpira wa miguu nchnii Misri (EFA ),kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha Zamalek na ENPPI.
Mashabiki wapatao ishirini na moja (22) wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo
zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kupelekea Shirikisho la Soka nchini Misri
kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.
Katika salam zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.
TFF YAIPONGEZA CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Bw Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika nchini Equatorial Guinea bila ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
Katika salamu hizo kwenda kwa Bw Haytou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Bw Hicham El Amrani, Bw Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.
RATIBA YA MECHI ZIJAZO ZA LIGI KUU
MECHI ZIJAZO LIGI KUU
Feb 11, 2P15
Azam vs Mtibwa Sugar
Feb 14, 2015
Ndanda vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs Mbeya City
Stand United vs Mgambo Shooting
Feb 15, 2015
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Feb 21, 2015
Mbeya City vs Yanga
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Ndanda vs Coastal Union
Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
Feb 22, 2015
Stand United vs Simba
Azam vs Tanzania Prisons
Feb 25, 2015
Mbeya City vs Ruvu Shooting
BARCELONA NAO KUTUA BONGO, KUCHEZA NA MAGWIJI WA BONGO
KIKOSI cha magwiji wa Barcelona kitazuru Dar es Salaa Machi 28 mwaka huu kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya wachezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, maarufu Tanzania Eleven.
Almasi Kasongo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wanaoandaa ziara hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya Prime Time Promotions amesema hayo leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam.
Mkutano huo, ulihudhuriwa na mkali wa zamani wa mabao wa Barcelona, Mholanzi Patrick Kluviert ambaye amethibitisha ujio wa nyota waliotaka Camp Nou miaka ya nyuma kidogo.
Ziara hiyo ni matunda ya ziara ya magwiji wa wapinzani wa Barcelona, Real Madrid Agosti mwaka jana, ambao pia walicheza na magwiji wa Tanzania na kushinda 3-1 Dar es Salaam.
WARUNDI, WASOMALI KUZICHEZESHA YANGA, AZAM
MAREFA kutoka nchi jirani za Burundi na Somalia, ndio watachezesha mechi za kwanza za Raundi ya Awali ya michuano ya Afrika za timu za Tanzania mwishoni mwa wiki.
Yanga SC itamenyana na BDF XI Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC watakuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji.
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Azam na El Merreikh refa atakuwa Hassan Mohamed Hagi, wasaidizi wake namba moja Bashir Sh Abdi Sule na namba mbili Salah Omar Abubakar wakati mezani atakuwa Kidane Melles Terfe, wote wa Somalia.Kamisaa wa mchezo huo atakuwa M.CHaileyesus Bazezew Beleti kutoka Ethiopia.
Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga SC na BDF XI, refa atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.
Monday, February 9, 2015
IVORY COAST MABINGWA WAPYA AFRIKA
IVORY Coast jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa soka barani Afrika baada ya kuichapa Ghana kwa penalti 9-8 katika mechi ya fainali iliyochezwa mjini Malabo, Equatorial Guinea.
Mshindi wa pambano hilo ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa suluhu.
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ivory Coast kutwaa taji hilo tangu 1992, ilipoishinda Ghana kwa staili hiyo hiyo ya penalti tano tano.
Kipa Boubacar Barry aliibuka shujaa wa Ivory Coast baada ya kufunga penalti ya mwisho na kisha kuokoa shuti la kipa mwenzake wa Ghana, Razak Braimah.
Pambano hilo lilikuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kucheza kwa kasi na
nguvu, kila moja ikipania kutoka uwanjani na ushindi.
Sunday, February 8, 2015
YANGA MWENDO MDUNDO
MSHAMBULIAJI Mrisho Ngasa jana aliibuka shujaa wa Yanga baada ya kuifungia mabao mawili katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga iliichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 na kurejea kileleni mwa ligi hiyo.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Ngasa tangu aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini, alikokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
Ngasa alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kpah Sherman.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuzichezea Azam na Simba, alifunga bao la kwanza dakika ya 55 baada ya kupokea pasi maridhawa kutoka kwa Simon Msuva.
Nyota huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars, aliongeza bao la pili dakika ya 62 baada ya kuwachambua mabeki wa Mtibwa kabla ya kufumua shuti lililompita kipa Said Mohamed.
Ushindi huo wa Yanga ni wa pili mfululizo na umekuja siku chache baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 wiki iliyopita mjini Tanga.
Saturday, February 7, 2015
SIMBA YALE YALE DROO KWA KWENDA MBELE AU KUFUNGWA
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Simba ya Dar es Salaam leo imegawana pointi na Mbwa Mwitu wa Tanga, Coast Union katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana.
Wanyama hao wa mwituni wamemaliza dakika 90 za kusukuma gozi la ng'ombe bila goli hata la kuotea. Coast Union siku kadhaa zilizopita iliambulia kichapo cha goli moja kutoka kwa Yanga ya Dar es Salaam.
Kikosi cha Simba SC kiliwakilishwa dimbani na: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.
Kikosi cha Coastal Union wao ilikuwa: Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.
DRFA YATAJA RATIBA 18 BORA
Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA,kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beirahotspurs na Pan Africa.
Katika kundi (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,imeingia katika hatua ya pili,ambayo itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali ,ambapo kwa upande wa kundi (A)
Simba U20 vs Red Coast (Karume)
Sifa UTD vs Shababi (Mwl/Nyerere)
Ukonga UTD vs Zakhem (Airwing)
Ugimbi vs Beirahospurs (Bandari)
KATIKA KUNDI (B) Februari 12
Yanga U20 vs Stakishari (Karume)
FFU vs New Kunduchi (Benjamini Mkapa)
Sinza Stars vs Changanyikeni (Kines)
Tuamoyo vs Sifapolitan (Bandari)
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.
NYOSO, MORRIS WAPEWA ADHABU KALI
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City
na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya
wakiwa uwanjani.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji
mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya
11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi
mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa
alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa
mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa
kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye
mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri
kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea
mgongano huo.
Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT
scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani
akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video
uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.
Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya
Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na
kumpa onyo kali.
Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000
Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa
kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui
iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa
kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John
Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa
kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.
Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na
viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza
kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza
upande wa walalamikaji pekee.
Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa kumchezea
ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya mlalamikiwa
kupata udhuru uliosababisha asiwepo.
Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers
kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa,
kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya
Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.
Wednesday, February 4, 2015
YANGA YAISULUBU COASTAL UNION MKWAKWANI
BAO lililofungwa na beki wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' jana liliiwezesha Yanga kukata ngebe za wapinzani wao Coastal Union baada ya kuichapa bao 1-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Cannavaro alifunga bao hilo dakika ya 11 kwa kichwa, akiunganisha mpira uliorushwa na beki mwenzake, Mbuyu Twite kutoka pembeni ya uwanja.
Kwa ushindi huo, Yanga sasa imetwaa uongozi wa ligi kuu, ikiwa na pointi 22 na kuwashusha waliokuwa wakiongoza Azam. Timu mbili hizo zinatofautiana kwa pointi moja huku Azam ikiwa na mchezo mmoja kibindoni.
Ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wake, Coastal Union ililianza pambano hilo kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Yanga, lakini umaliziaji mbovu ulikuwa kikwazo kupata bao.
Monday, February 2, 2015
USAJILI WA DIRISHA DOGO LIGI KUU YA ENGLAND HUU HAPA
Arsenal yamnyakua kiungo mkabaji kinda wa miaka 17, Krystian Bielik na beki wa kati, Gabriel Paulista
Manchester United yamsajili kipa Victor Valdes
Sunderland yaimarisha kikosi chake kwa kumsajili Jermain Defoe
Liverpool haijafanya usajili wowote wa dirisha dogo
West Brom yamnyakua Callum McManaman kutoka Wigan
Yaya Sanogo ajiunga na Crystal Palace
ARSENAL
WALIOSAJILIWA
Gabriel Paulista (Villarreal, £11.2m)
Krystian Bielik (Legia Warsaw, £2.5m)
WALIOONDOKA
Benik Afobe (Wolves, ada haikutajwa)
Lukas Podolski (Inter Milan, mkopo)
Yaya Sanogo (Crystal Palace, mkopo)
Joel Campbell (Villarreal, mkopo)
ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA
Carles Gil (Valencia, £3.25m)
Scott Sinclair (Manchester City, mkopo)
WALIOONDOKA
Darren Bent (Derby, mkopo)
Gary Gardner (Nottingham Forest, mkopo)
Chris Herd (Wigan, mkopo)
Callum Robinson (Preston, mkopo)
BURNLEY
WAlIOSAJILIWA
Michael Keane (Manchester United, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Hakuna
CHELSEA
WALIOSAJILIWA
Juan Cuadrado (Fiorentina, £27m)
WALIOONDOKA
Andre Schurrle (Wolfsburg, £24m)
Ryan Bertrand (Southampton, £10m)
Mark Schwarzer (Leicester, huru)
Thomas Kalas (Middlesbrough, mkopo)
John Swift (Swindon, mkopo)
Lewis Baker (Sheffield Wednesday, mkopo)
Marko Marin (Anderlecht, mkopo)
Mohamed Salah (Fiorentina, mkopo)
CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA
Wilfried Zaha (Manchester United £6m)
Jordon Mutch (QPR, £5.75m)
Lee Chung-yong (Bolton, ada haikutajwa)
Keshi Anderson (Barton Rovers, £35,000)
Shola Ameobi (Gaziantep, huru)
Pape Souare (Lille, ada haikutajwa)
Yaya Sanogo (Arsenal, mkopo)
WALIOONDOKA
Stuart O'Keefe (Cardiff, ada haikutajwa)
Alex Wynter (Colchester, ada haikutajwa)
Zeki Fryers (Rotherham, mkopo)
Lewis Price (Crawley, mkopo)
Jake Gray (Cheltenham, mkopo)
Barry Bannan (Bolton, mkopo)
Jimmy Kebe (huru)
EVERTON
WALIOSAJILIWA
Aaron Lennon (Tottenham, mkopo)
WALIOONDOKA
Samuel Eto'o (Sampdoria, huru)
Chris Long (Brentford, mkopo)
Conor McAleny (Cardiff, mkopo)
HULL CITY
WALIOSAJILIWA
Dame N'Doye (Lokomotov Moscow, £3m)
WALIOONDOKA
Tom Ince (Derby County, mkopo)
LEICESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Andrej Kramaric (Rijeka, £9.5m)
Mark Schwarzer (Chelsea, huru)
Robert Huth (Stoke City, mkopo)
WALIOONDOKA
Tom Hopper (Scunthorpe, mkopo)
LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Oussama Assaidi (Al Ahli, £4.7m)
Suso (AC Milan, £1m)
MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Wilfried Bony (Swansea, £28m)
WALIOONDOKA
Matija Nastasic (Schalke, mkopo)
Scott Sinclair (Aston Villa, mkopo)
MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA
Victor Valdes ( huru)
Sadiq El Fitouri (Salford City, huru)
Andy Kellett (Bolton, mkopo)
WALIOONDOKA
Wilfried Zaha (Manchester United, £6m)
Michael Keane (Burnley, £3m)
Darren Fletcher (West Brom, huru)
Will Keane (Sheffield Wednesday, mkopo)
Ben Amos (Bolton, mkopo)
Jesse Lingard (Derby County, mkopo)
NEWCASTLE UNITED
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Mapou Yanga-Mbiwa (Roma, £5.2m)
Hatem Ben Arfa (huru)
Gael Bigirimana (Rangers, mkopo)
Haris Vuckic (Rangers, mkopo)
Shane Ferguson (Rangers, mkopo)
Davide Santon (Inter Milan, mkopo)
QUEENS PARK RANGERS
WALIOSAJILIWA
Mauro Zarate (West Ham, mkopo)
Ryan Manning (Galway United, huru)
WALIOONDOKA
Jordon Mutch (Crystal Palace, £5.75m)
Bruno Andrade (Stevenage, mkopo)
SOUTHAMPTON
WALIOSAJILIWA
Ryan Bertrand (Chelsea, £10m)
Eljero Elia (Werder Bremen, mkopo)
Filip Djuricic (Benfica, mkopo)
WALIOONDOKA
Jack Cork (Swansea, £3m)
Jos Hooiveld (Millwall, mkopo)
Artur Boruc (Bournemouth, mkopo)
STOKE CITY
WALIOSAJILIWA
Philipp Wollscheid (Bayer Leverkusen, mkopo)
WALIOONDOKA
Ryan Shotton (Derby, ada haikutajwa)
Maurice Edu (Philadelphia Union, ada haikutajwa)
Robert Huth (Leicester City, mkopo)
SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA
Jermain Defoe (Toronto, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Jozy Altidore (Toronto, ada haikutajwa)
Mikael Mandron (Shrewsbury, mkopo)
Charis Mavrias (Panathinaikos, mkopo)
Cabral (huru)
SWANSEA CITY
WALIOSAJILIWA
Kyle Naughton (Tottenham, £5m)
Jack Cork (Southampton, £3m)
Matt Grimes (Exeter City, £1.75m)
Nelson Oliveira (Benfica, mkopo)
WALIOONDOKA
Wilfried Bony (Manchester City, £28m)
Rory Donnelly (Tranmere, mkopo)
Jazz Richards (Fulham, mkopo)
TOTTENHAM HOTSPUR
WALIOSAJILIWA
Dele Alli (MK Dons, £5m)
WALIOONDOKA
Kyle Naughton (Swansea, £5m)
Aaron Lennon (Everton, mkopo)
Milos Veljkovic (Charlton, mkopo)
Benoit Assou-Ekotto (huru)
Dele Alli (MK Dons, mkopo)
WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA
Callum McManaman (Wigan, £4.75m)
Darren Fletcher (Manchester United, huru)
WALIOONDOKA
Luke Daniels (Scunthorpe, ada haikutajwa)
WEST HAM UNITED
WALIOSAJILIWA
Doneil Henry (Apollon Limassol, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Mauro Zarate (QPR, mkopo)
Ricardo Vaz Te (huru)
FRANCIS CHEKA AFUNGWA JELA
NA LATIFA GANZEL, MOROGORO,
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, imemhukumu bondia nguli nchini, Francis Cheka, kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la shambulio na kudhuru mwili.
Cheka alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya Hakimu Mkazi, Said Msuya, kumtia hatiani kwa kosa la kumshambulia na kumdhuru mwili aliyekuwa Meneja wa baa yake, Bahati Kabanda.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana, katika eneo la kata ya Uwanja wa Taifa, Manispaa ya Morogoro.
Bondia huyo anadaiwa kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake ilijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall na kusababisha kumdhuru sehemu mbalimbali za mwili.
Akisoma hukumu hiyo, Hakima Msuya alisema mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo, atatakiwa kumlipa mlalamikaji gharama ya sh. milioni moja ya matibabu alizojitibia baada ya kupigwa na bondia huyo.
Akizungumza baada ya kupewa adhabu hiyo, Cheka alidai kuna mkono wa watu wenye lengo la kutaka kuchafua jina lake na maisha yake .
Cheka alidai kushangazwa kusomewa kuwa alikiri kosa la kumpiga mlalamikaji wakati yeye katika maelezo yake alikana shitaka.
"Ni wazi kesi yangu ilipangwa kuvurugwa ili nifungwe na kunipoteza katika ulimwengu wa masumbwi," alidai.
Kocha wa bondia huyo, Abdallah Komando, alidai kuwa kifungo cha bondia wake kimemtia simanzi kubwa, kwa kuwa kesi hiyo ingeweza kumalizika mezani.
Komando alisema kifungo cha bondia wake ni matokeo ya fitna za kimichezo.
MANJI AONYESHA JEURI YA FEDHA, KUDHAMINI KOMBE LA EBOLA KWA DOLA 500,000 ZA MAREKANI
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji ametenga kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya michuano ya Ebola Cup itakayoshirikisha timu 108 za Afrika.
Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwa na Yanga pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Jonas Tibohora alisema hatua za kuanza michuano hizo zipo kwenye hatua nzuri.
Alisema michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazowasaidia waafrika walioathirika na ugonjwa wa Ebola.
Alisema michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Soka Afrika (CAF), na kwamba kwa sasa kamati ya michuano hiyo yenye wajumbe mchanganyiko kutoka nchi wanachama wa CAF itakaa na kupanga tarehe ya michuano hiyo.
Alisema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu kati ya nne na saba.
Alisema michuano hiyo itashirikisha timu zote kutoka Afrika ambazo ni mwanachama wa CAF ambapo kila nchi itatoa timu mbili na michuano itachezwa nyumbani na ugenini.
Alisema kila timu zitachangia kiasi cha dola 100,000 kama ada ya ushiriki ambazo zitaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa kusaidia waathirika hao.
"Mpango huu yatari umepitishwa na kinachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya michuano ambapo kamati ya mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti wake Machache Shipanda kutoka Zambia itakutana na kutoa ratiba,"alisema Tibohora.
Alisema pia mpango huo umeungwa mkona na umoja wa Afrika (AU) ambao watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa manufaa makubwa.
Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwa na Yanga pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Jonas Tibohora alisema hatua za kuanza michuano hizo zipo kwenye hatua nzuri.
Alisema michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazowasaidia waafrika walioathirika na ugonjwa wa Ebola.
Alisema michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Soka Afrika (CAF), na kwamba kwa sasa kamati ya michuano hiyo yenye wajumbe mchanganyiko kutoka nchi wanachama wa CAF itakaa na kupanga tarehe ya michuano hiyo.
Alisema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu kati ya nne na saba.
Alisema michuano hiyo itashirikisha timu zote kutoka Afrika ambazo ni mwanachama wa CAF ambapo kila nchi itatoa timu mbili na michuano itachezwa nyumbani na ugenini.
Alisema kila timu zitachangia kiasi cha dola 100,000 kama ada ya ushiriki ambazo zitaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa kusaidia waathirika hao.
"Mpango huu yatari umepitishwa na kinachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya michuano ambapo kamati ya mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti wake Machache Shipanda kutoka Zambia itakutana na kutoa ratiba,"alisema Tibohora.
Alisema pia mpango huo umeungwa mkona na umoja wa Afrika (AU) ambao watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa manufaa makubwa.
DRFA YAIFAGILIA TEMEKE KUTWAA KOMBE LA TAIFA LA WANAWAKE
Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimeipongeza timu ya Temeke kwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake,baada ya kuifunga Pwani kwa bao 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complez, Chamazi.
Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa na Waziri mwenye dhamana ya michezo Dk.Fenella Mukangara,Temeke ilijipatia bao lake dakika ya 66 kupitia kwa mchezaji wao Neema Paul.
Temeke walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuwafunga ndugu zao Ilala kwa mabao 4-0,huku Pwani wakitinga hatua hiyo kwa kuifunga Kigoma mabao 3-2.
Mshindi amejinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili, wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja.
Mbali na Temeke kubeba ubingwa,pia imefanikiwa kutoa mlinda mlango bora, Belina Julius aliyezawadiwa kitita cha shilingi 500,000/-.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliwakutanisha, Ilala dhidi ya Kigoma, ambapo Ilala ilifanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kushinda mabao 3-0.
Uongozi wa DRFA,unatoa shukurani kwa mashabiki wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani,ambao wamejitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)


















