KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeamua kuipokonya Simba pointi tatu ilizopewa na Kamati ya Saa 72, baada ya kubainika kuwa, Kagera Sugar ilimchezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Akisoma maamuzi ya kamati hiyo leo, Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa, amesema Kamati ya Saa 72 ilikosa uhalali wa kusikiliza rufani ya Simba kutokana na kikao chake kuwashirikisha baadhi ya wajumbe wasiohusika.
Aidha, Mwesiga alisema Kamati ya Nidhamu imebaini kuwa, rufani ya Simba ilikosa uhalali wa kusikilizwa kutokana na walalamikaji kutokana rufani na pia kushindwa kulipia ada ya sh. 300,000.
Licha ya Simba kupokwa pointi hizo, bado inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 59, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56, lakini ikiwa na mechi mbili mkononi, hivyo kuwepo na uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa.
No comments:
Post a Comment