'
Sunday, April 16, 2017
SAFARI YA YANGA KIMATAIFA YAFIKIA TAMATI
UNAWEZA kusema kuwa safari ya Yanga katika michuano ya Afrika mwaka huu imefikia ukingoni baada ya kupigwa mweleka wa mabao 4-0 na MC Alger ya Algeria.
Kipigo hicho kwa Yanga, ilichokipata katika mechi ya marudiano iliyochezwa jana mjini Algiers, kimeifanya itolewe kwa jumla ya mabao 4-1, baada ya kushinda mechi ya awali mjini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Yanga iliangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa raundi ya pili na Zanaco ya Zambia kwa faida ya bao la ugenini, baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na waamuzi kutoka Guinea, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa imeshakubali kipigo cha mabao 2-0.
Dalili za Yanga kupoteza mchezo huo zilionekana mapema kutokana na kuibuka migogoro baina ya wachezaji na viongozi kabla ya safari ya kuanza safari ya Algeria
Wachezaji Vincent Bossou kutoka Togo na Obrey Chirwa kutoka Zambia, waligoma kusafiri na timu kwa sababu ya madai ya mishahara yao ya miezi mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment