'
Thursday, February 25, 2016
YANGA YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO
YANGA jana ilisonga mbele katika michuano ya soka ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuilaza JKT Mlale mabao 2-1.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hizo mbili zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Kocha Hans van der Pluijm wa Yanga alilazimika kupangua kikosi kilichocheza jana kwa kuwapanga baadhi ya wachezaji wapya, wakiwemo Matheo Anthony, Paul Nonga na Saidi Juma 'Makapu' huku akimrejesha dimbani nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyekuwa nje kwa miezi kadhaa kutokana na kuwa majeruhi.
Baada ya kosakosa kadhaa kwa kila upande, JKT Mlale kutoka Ruvuma, inayoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza, ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 21 lililofungwa na Mgandila Shaaban baada ya kupokea krosi kutoka kwa Edward Songo.
Nonga aliifungia Yanga bao la kusawazisha dakika ya 42, akiunganisha wavuni krosi kutoka kwa Godfrey Mwashiua.
Mabadiliko yaliyofanywa na Yanga katika kipindi cha pili, yaliiwezesha kubadili sura ya mchezo dakika ya 58 kwa kufunga bao lililopachikwa kimiani na Thabani Kamusoko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment