KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 28, 2013

COASTAL UNION YAIWEKEA NGUMU YANGA



UONGOZI wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, umesema hauna mpango wa kumuuza mchezaji wao nyota, Abdul Banda.
Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka Tanga, Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Aurora hawako tayari kumuuza mchezaji huyo kwa gharama yoyote.
Aurora alisema hayo baada ya kuwepo na taarifa kwamba, Banda amejiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.
"Hatuwezi kumuuza mchezaji wetu yeyote kwa sababu hatuko kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi na bado tunapigana kuhakikisha tunafanya vizuri katika mzunguko wa pili,"alisema.
Aurora alisema taarifa za Banda kusajiliwa na Yanga, zimeleta mtafaruku kubwa kwa mashabiki wa Coastal Union na kuwaweka kwenye wakati mgumu viongozi wa klabu hiyo.
"Mashabiki wetu wamekuwa wakitusumbua kupiga simu kuulizia hatma ya Banda. Ninachoweza kuwahakikishia ni kwamba, Banda hauzwi na wasubiri watamuona tena katika mechi za mzunguko wa pili,"alisema.
Banda ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa Yanga, kutokana na staili yake ya uchezaji na pia kupanda mbele kusaidia mashambulizi na kurudi nyuma kuongeza nguvu kwenye ulinzi.
Beki huyo kisiki, amesajiliwa na Coastal Union msimu huu baada ya kupandishwa daraja kutoka kikosi cha pili cha timu hiyo.

No comments:

Post a Comment