KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

OMOTOLA ATUNUKIWA TUZO YA BEFFTA


LONDON, Uingereza
MCHEZA filamu Omotola Jalade amesema anaona fahari kubwa kwa kushinda tuzo ya BEFFTA kutokana na kufanya kwake vizuri katika fani ya filamu.
Omotola alisema wiki hii mjini hapa kuwa, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwake kwa vile hajawahi kupokea tuzo yenye hadhi kubwa katika kipindi cha miaka 16, ambacho amekuwa akijihusisha na uigizaji.
Mwanadada huyo, ambaye ni mama wa watoto wanne, alimshukuru mumewe Kepteni Mathew Ekeinde na mashabiki wake kwa kumuwezesha kuwepo kwenye chati ya juu katika fani hiyo.
"Hii ni tuzo bora niliyowahi kupokea katika ngazi ya kimataifa, ni heshima kubwa kwangu na nimefurahi kwamba katika kipindi cha miaka 16 cha kazi yangu, nimeweza kutambulika kimataifa,"alisema.
Aliongeza: "Kuna watu wengi wa kuwashukuru kutokana na kunifikisha hapa nilipo. Shukurani za pekee zimwendee mume wangu kwa kuwa karibu nami muda wote na kila niliyewahi kufanya naye kazi, lakini watu muhimu zaidi ni mashabiki wangu."
Malkia huyo wa Nollywood alisema anawapenda mno mashabiki wake kwa sababu siku zote wamekuwa wakimuunga mkono kwa kila analolifanya.
Omotola amekuwa mcheza filamu wa kwanza wa Nollywood kupewa tuzo ya BEFFTA. Alikabidhiwa tuzo hiyo ni mcheza filamu nyota wa kike mwenye maskani yake mjini London, Theodora Ibekwe.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali pamoja na wageni waalikwa.

No comments:

Post a Comment