KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

EMPRESS NJAMA AJISAFISHA



LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu Empress Njama amesema si vizuri kukikosoa kitabu kwa sababu ya sura ya kava lake. Amesema ni vyema kukisoma kwanza ndipo msomaji aweze kupambanua uzuri na ubaya wake.
Empress amesema mfano huo unalingana na maisha yake halisi kwa vile amekuwa akizushiwa mambo mengi ya uongo, ambayo mengine hajawahi kuyafanya katika maisha yake.
Mwanadada huyo amesema kwa watu wasiomfahamu, wanaweza kumlinganisha na shetani kwa kudhani ni mtu mbaya kutokana na jinsi jina lake linavyochafuliwa na vyombo vya habari.
"Watu ambao wamesoma ama kusikia habari mbaya kuhusu mimi wanapokutana nami, hupatwa na mshtuko. Wengine huthubutu hata kuomba radhi wakisema, 'Empress, samahani, sikufikiria iwapo ni mtu mchangamfu kiasi hiki',"alisema.
Empress alisema kutokana na taswira mbaya iliyojengwa na vyombo vya habari juu yake, mtu yeyote ambaye hajawahi kukutana naye, anaweza kumfikiria kuwa ni shetani.
"Kazi ya vyombo vya habari katika jamii ni kuhabarisha, lakini nafasi yake hivi sasa ni kuwachafua watu kwa kutoa taarifa za uongo ili kutengeneza fedha. Kama utaamini kila kitu utakachokiona ama kusikia kwenye magazeti, unaweza pia kuamini kwamba Obama ni bibi,"alisema Empress.

No comments:

Post a Comment