KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, July 22, 2013

SIMBA, YANGA DIMBANI OKTOBA 20 LIGI KUU YA BARA


HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, ambayo inaonyesha kuwa, timu kongwe za Simba na Yanga zitakutana Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo iliyotolewa leo inaonyesha kuwa, mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kati ya mabingwa, Yanga na washindi wa pili msimu uliopita, Azam itapigwa Agosti 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kushuka dimbani katika miji saba tofauti.

Katika mechi hizo za ufunguzi,  Yanga itacheza na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro) na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- attached).

Sunday, July 21, 2013

YANGA CHUPUCHUPU KWA URA



Wachezaji wa URA wakishangilia bao lao la pili dhidi ya Yanga leo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya Jerry Tegete kusawazisha dakika ya 90. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto)

BAO lililofungwa na mshambuliaji Jerry Tegete dakika ya 90 leo limeinusuru Yanga kuadhiriwa na URA ya Uganda baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 2-2 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0. Bao hilo la kuongoza lilifungwa na Litumba Yayo dakika ya 42.

Litumba ndiye aliyeizamisha Simba katika mechi ya jana baada ya kuifungia URA mabao yote mawili ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Bao la pili la URA lilifungwa tena na Litumba dakika ya 61 kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililowapita mabeki wa Yanga na kipa Deogratius Munishi 'Dida' aliyejaribu kuupangua mpira, lakini ulimshinda nguvu.

Mrundi, Didier Kavumbagu aliifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 66 alipounganisha wavuni kwa kichwa krosi maridadi iliyopigwa na Juma Abdul kutoka pembeni ya uwanja.

Tegete aliisawazishia Yanga baada ya kuwazidi nguvu na mbio mabeki wawili wa URA pamoja na kipa wao, Yassin Mugabi.

Mrundi Didier Kavumbangu alianza dakika ya 66 akiunganisha krosi ya beki Juma Abdul kabla ya Tegete kusawazisha dakika ya 90 baada ya kuwazidi nguvu na maarifa kipa wa URA, Yassin Mugabi na mabeki wawili.

WABUKINI KUZICHEZESHA STARS NA UGANDA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Madagascar kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

Waamuzi wataongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official).

Kamishna wa mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.

Mechi hiyo namba 38 itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Taifa Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.

SIMBA HOI KWA URA



Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuifungia Simba bao la kuongoza katika mechi ya kimatifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. URA ilishinda 2-1. (Picha na Bin Zubeiry)

SIMBA jana ilipigwa mweleka wa mabao 2-1 na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na kupokea kichapo hicho, vijana wa Simba, ambao wengi ni wapya walionyesha kiwango cha juu cha soka, hasa kipindi cha kwanza na kuwafanya washangiliwe na mashabiki wao.

Iliwachukua Simba dakika saba kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake mpya, Betram Mwombeki kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Ramadhani Singano 'Messi'. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

URA ilisawazisha dakika ya 60 kwa bao lililofungwa na Lusimba Yayi baada ya mabeki wa Simba kuzubaa kuokoa shambulizi kwenye lango lao.

Simba ilipata pigo dakika ya 65 baada ya Mwombeki kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko beki, Jonathan Mugaba.

Pengo hilo liliiwezesha URA kupata bao la pili dakika ya 75 lililofungwa na Yayi baada ya kupokea pasi kutoka kwa Derick Walulya, aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi.

URA inatarajiwa kushuka tena dimbani leo kucheza na Yanga kwenye uwanja huo.

Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Rahim Juma/Sino Augustino, Samuel Ssenkoom, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Miraj Adam, William Lucian, Betram Mombeki, Zahor Pazi/Twaha Ibrahim na Marcel Boniventura.

Friday, July 19, 2013

ENTER THE DRAGON YATIMIZA MIAKA 40, MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU BRUCE LEE



Behind every great man is a great woman, and for martial arts legend Bruce Lee, that woman was Linda Emery, who married her dashing gongfu teacher in the mid-'60s. Linda and Bruce were husband and wife until July 20, 1973, when Bruce died of cerebral edema at the age of 32 ... just six days before the Hong Kong release of what many consider to be his greatest cinematic achievement, "Enter the Dragon."
Upon the 40-year anniversary of both the premiere of "Enter the Dragon" (which is now available in a 40th Anniversary Edition Blu-ray) and the untimely death of its star, we spoke with Linda Lee Cadwell (who has since remarried) about her late husband's legacy and how his abilities and philosophies have inspired countless others to reach their full potential — and beyond.
BRYAN ENK: Does it feel like 40 years have passed since "Enter the Dragon" was first released?
LINDA LEE CADWELL: [Laughs] No, I was actually quite shocked when I realized, "40 years?!" It's a lifetime, to be sure. And like you, a lot of the people who admire "Enter the Dragon" and Bruce were not even born at the time when he was alive. That does put it in perspective and makes it seem like 40 years have passed.
BE: "Enter the Dragon" is considered to be one of the best martial arts films of all time, if not the best. What do you feel have been the most influential aspects of the film over the past four decades and what has made it stand the test of time so well?
LLC: Well it certainly is the gold standard of martial arts films and certainly inspired the genre altogether. I think it's quite obvious really that the outstanding thing about "Enter the Dragon" was Bruce. The storyline is really nothing spectacular and the technical qualities are fine, but the thing that makes it really stand out is of course Bruce. And the parts of it that people admire so much are on different levels — a person can look at "Enter the Dragon" and admire the physicality of it, the combat, the choreography inspired and performed by Bruce, or they can take it a step further and see that there are bits of philosophical wisdom in it, also inspired by Bruce.
BE: Do you have a particularly good behind-the-scenes memory from when the film was in production, something that happened on or off the set?
LLC: Oh my, yes! Bruce had been wanting to do a Hong Kong/American co-production for a long time, that had been his goal when he first went to Hong Kong to make films, that one day the filmmakers in the West would realize his value and talent and would be ready to do something with him. So it was an important landmark for him and it was important for him that the film be a success. So he put his heart and soul in it, and he was very insistent on some changes to the script. Some people have made the comment that he was very nervous to start the film, that he was on the edge of a nervous breakdown because he was so uptight about the film and making sure it was a success but that was not really the case — he just had some very important things to say about the script and how he wanted the film to be and very insistent on some changes. And I must say that in light of 40 years and we're still looking at this movie that he was right, and it's because of Bruce and his insisting on doing certain things and adding certain parts to the film that it's been such a success for four decades.
BE: My favorite part of the film is the "Hall of Mirrors" scene. It's a terrific sequence — the choreography, the building tension and there's something truly iconic about the imagery of the bloody scratches on Bruce's chest. Do you have a favorite scene from the film?
LLC: Well, of course all the combat scenes are spectacular and unmatched over all these years, but my favorite parts of the film are the more philosophical points that Bruce brings to the picture. For instance, when he's talking to the young boy and teaching him — that kind of thing makes the film more than an adventure and a "violent film," it gives it more substance.
BE: How did you and Bruce first meet?
Linda Lee, Brandon Lee, and Bruce Lee, circa 1970 (Photo: Everett)LLC: [Laughs] It's a fun story, actually! I was a senior in high school in Seattle, Washington at Garfield High School. And Bruce used to come to my school, he was five years older and a student of Philosophy at the University of Washington, he was friends with the philosophy teacher at my high school. So he would come to my high school to give lectures on Chinese philosophy; I was not in that class but I can tell you that every girl at my school knew when Bruce Lee was in the house because he was so dashing and so handsome. And one of my girlfriends who happened to be Chinese was taking gongfu lessons from him. And so the summer after I graduated from high school she talked me into taking gongfu lessons with Bruce, so that's how we first met — I was his student and it wasn't long before I was more interested in the teacher than the martial art, though I continued to do it for quite a while. [Laughs]
BE: Bruce is known for founding a martial arts practice and philosophy known as Jeet Kune Do. How would you describe the basic fundamentals of that?
LLC: Well, Bruce would never have described it as a "system," because a "system" is an organization of certain rules and his way of martial arts did not have any set rules — it is what is best for the individual person who is learning it. There was an aura of just responding to what "is" in martial arts, so you would not have a particular set of movements in response to, say, an attack — like in some forms of karate it's like "Well, I will punch in a certain way, I will do this or that in certain sequence." Bruce's art was not like that — it flowed, like he often said, like water flows and can fit into any container, it flowed to fit into any situation that was presented. So that's why he called it his "way" of martial arts, not a "system" of martial arts.
There's a great deal more to it as well, and there are fundamentals to it so that it can be carried on for generations, as it is now. But it's also a way of personal growth, to learn more about yourself — as Bruce used to say, all knowledge is really self-knowledge, you learn more about yourself and how to fit into a variety of situations. So, in a nutshell, that's a way of describing it.
BE: Do you have a particularly good memory involving a fan of Bruce's, either an encounter with a fan or a story that a fan told about Bruce?
LLC: Actually, there are so many that I can lump them all into one person, in a way. [Laughs] I've received letters over the years and had personal acquaintance with so many people who have told me how they're truly so inspired by Bruce. And most of the time, especially after the passing of 40 years, it's because of a wanting to model Bruce as a way of life, in a way of improving their own lives. So not so much "Well, I want to be a martial artist" or "I want to learn how to beat up people" — I think many years ago that was the first thing that impressed people, his fighting ability, but I think after all these years people have discovered there were many more layers to Bruce and he was a person of great depth.
And he did an immense amount of writing, which we are blessed today to still have and has been reproduced a number of times in different forms and I think people use that as an inspiration to improve their own lives.
BE: The 1993 film "Dragon: The Bruce Lee Story" is mostly based on your 1975 book, "Bruce Lee: The Man Only I Knew." How do you feel about the film — was it a good adaptation or was it missing something?
LLC: I have mixed feelings about the film. On the good side I think it hit on the high points of Bruce's life, the turning points, you might say. For instance, when he hurt his back and then he was laid up for six months, in bed a lot of the time, unable to be his usual physical self -- the doctors told him he would be unable to ever do gongfu again and all this stuff. That was certainly a turning point in his life, though the injury did not happen in the way they showed it in the film — they felt they had to make it more dramatic. But the point is he hurt his back and he used that time, the six months or more that he was laid up, to produce most of his writings — the philosophical writings about his method of combat, all kinds of things.
So the film took some liberties, it changed some facts, it had a mythical figure in it that I would not have agreed with but that a person can view on different levels. So there were good things and there were some not so good things and I hope that some day a really wonderful film is made about Bruce.
BE: What are you dedicating your time to these days?
LLC: I have a wonderful life going on. I have a great husband named Bruce Cadwell, I live in Idaho, and between us we have nine grandchildren; I have one grandchild, my daughter's daughter who is ten years old and I like to spend a lot of time with her.
Actually, you know, my daughter Shannon has taken over the role of perpetuating and preserving her father's legacy, so I just show up at certain times and of course I'm interested in that goal as well and we have larger goals of some day wanting to build the Bruce Lee Action Museum and people in Seattle are very interested in sponsoring that. It's a long-term project and that's what we're aiming at in the long run.

MKUTANO MKUU SIMBA LEO, INAKIPIGA NA URA JIONI U/TAIFA



MWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, anawakaribisha wanachama wote wa Simba katika Mkutano Mkuu wa Wanachama utakaofanyika kesho katika bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ni wa kawaida wa kila mwaka na unaendeleza utaratibu wa uongozi wa Alhaji Rage kufanya mikutano kama hiyo kwa kadri Katiba ya klabu inavyotaka.
Ikumbukwe kuwa katika miaka ya nyuma, kuna kipindi klabu haikuwa ikifanya mikutano kama hii kwa kipindi kirefu na hivyo huu ni utaratibu mwafaka katika kuendeleza klabu ya SIMBA.
Kwa mwaliko huu, Mwenyekiti anawataka wanachama wote walio hai kuhudhuria mkutano huo na KLABU INASISITIZA KWAMBA WANACHAMA AMBAO HAWATAKUWA HAI HADI ASUBUHI YA SIKU YA MKUTANO HAWATARUHUSIWA KUINGIA MKUTANONI. HII MAANA YAKE NI KWAMBA WANACHAMA HAWARUHUSIWI KULIPIA KADI ZAO KWENYE ENEO LA MKUTANO SIKU YA MKUTANO.
Mkutano unatarajiwa kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama wote wanaombwa kujali muda.
Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utapokea na kujadili Ripoti ya Mapato na Matumizi ya Klabu kwa mwaka ulioisha kama ilivyokaguliwa na wakaguzi wa hesabu, kupokea taarifa ya Mpango Mkakati wa Klabu (Strategic Plan) ulioandaliwa na maprofesa wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT).
MECHI YA SIMBA NA URA
TIMU za Simba na URA ya Uganda zimewasili jijini Dar es Salaam tayari kabisa kwa pambano la kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa Simba kucheza kwenye uwanja huo tangu kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania na ikiwa imetoka katika ziara ya mafanikio ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.
URA imewasili jijini jana ikiwa na msafara wa wachezaji 23 na viongozi sita. Baadhi ya wachezaji maarufu waliokuja na timu hiyo ni Derick Walulya, George Owino na Musa Doca.
Pambano hilo litaanza majira ya saa kumi kamili jioni.
MSIBA
KWA niaba ya Kamati ya Utendaji ya Simba, Wanachama na Wapenzi wa klabu, Mhe; Rag anatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Juma Urongo aliyefariki dunia asubuhi ya leo na kutarajiwa kuzikwa leo jioni huko Tandika jijini Dar es Salaam.
Mzee Urongo alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wazee la Simba na ni miongoni mwa kizazi cha wazee walioanza kuishabikia klabu tangu ikiitwa Sunderland.
Rage amesema binafsi atakosa sana busara, ushauri na maelekezo yam zee huyo ambaye alikuwa shabiki wa Simba katika nyakati nzuri na mbaya.
Mungu na aiweke mahali pema roho ya marehemu Juma Urongo.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

LYATTO AAGA RASMI TFF



MAELEZO YA SHUKURANI YA MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF - KWA VIONGOZI NA WADAU WA SOKA NCHINI


1.                   Kama wote tunavyofahamu jana uongozi wangu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulifikia tamati kama mlivyotangaziwa na Rais wa TFF. Kwa heshima kubwa naomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na wadau wa soka kwa ushirikiano mkubwa nilioupata kutoka kwao wakati nikitekeleza majukumu mbalimbali ya TFF.

2.                   Kwa kushirikiana na viongozi wa mpira wa miguu katika TFF na mikoa yote Tanzania Bara, pamoja na wadau wa soka, nimepata fursa kulitumikia soka la nchi yetu kwa nafasi mbalimbali. Kwa pamoja tumetekeleza majukumu ya ujenzi wa misingi ya uongozi bora katika TFF na wanachama wake.

3.                   Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF:

(i)             kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, (Jan 2005 - Jan 2007). Nawashukuru pia wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mhe. Said El-Maamry kwa kunichagua kuwa Katibu wa Kamati hiyo. Ushirikiano mlionipatia ulioniwezesha kulitumikia taifa katika soka na kwa pamoja kurejesha nidhamu kwa kiwango kikubwa.

(ii)           kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu, iliyochunguza mkasa wa timu yetu ya Taifa ya wachezaji wa umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) mwezi Juni 2005. Nawashukuru wajumbe wa kamati  hiyo chini ya Dr. Hamad Ndee Mkuu wa Idara ya Michezo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, kwa kunichagua kuwa Katibu wa kamati hiyo iliyoandaa taratibu za mashindano ya vijana  ambazo ni msingi  wa mashindano ya vijana wa umri chini ya miaka 17  hapa nchini.

(iii)          kwa kuniteua kuwa Mjumbe wa Kamati Maalumu iliyotayarisha Programu ya kuendeleza Timu ya Taifa kwa kipindi cha miezi 15 (April 2006 hadi Juni 2007). Progamu iliyochangia Tanzania kiinua kiwango cha ubora wa soka kutoka nafasi ya 165 duniani mwezi Februari 2006 hadi nafasi ya 89 mwezi Desemba 2007.

(iv)         kwa kunipa fursa ya kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu ya kuboresha mapato ya TFF mwaka 2009. Nikiwa mjumbe na Katibu wa Kamati hiyo nilipata ushurikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini  na nje ya nchi.  Nina imani kuwa TFF itakamilisha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati na ya wadau wa soka ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia tiketi za elektroniki.

(v)           kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kwa  vipindi viwili; Februari 2009 - Machi 2011 na kuniteua tena kuiongoza Kamati hiyo kwa kipindi cha pili Machi 2011 hadi jana tarehe 18 Julai 2013. Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF kwa imani kubwa iliyoonyesha kwangu na wanakamati wenzangu.
4.                   Nawashukuru wajumbe wote wa wa Mkutano Mkuu wa TFF, kwa ushirikiano mkubwa mliotoa kwangu na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kushiriki kwa amani na utulivu na kuzingatia Katiba za vyama vyenu, Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi na hivyo kufanikisha zoezi la chaguzi za viongozi katika wilaya zote na Mikoa yote ya Tanzania Bara na hivyo kuwezesha kuwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu, ambao  katika kikao chake cha kwanza baada ya chaguzi hizo kimefanya jambo la kihistoria kuweka nguzo za  Mwenendo, Maadili  na Miiko ya uongozi wa soka la nchi yetu. Nilifarijika kuwa sehemu ya Mkutano Mkuu huo nikiwa mwalikwa.

5.                   Nawashukuru viongozi na wafanyakazi wote wa Sekretarieti ya TFF, wajumbe wa Kamati zote za TFF, Wajumbe wa Kamati zote za Uchaguzi za wanachama wa TFF na wanachama wao, kwa ushirikiano mkubwa na wa dhati uliowezesha kuwatumikia wadau wa soka kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

6.                   Nawashukuru sana wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ushirikiano niliopata kutoka kwao kwa muda tuliofanya kazi pamoja. Si jambo rahisi kusimamia chaguzi za mikoa yote na klabu zenye wanachama za Ligi Kuu, hata hivyo kwa kushirikiana na wadau mbalimali wa soka ambao nachukua fursa hii kuwashukuru, kwa pamoja tumeweza kutimiza jukumu hilo kikamilifu. 

7.                   Nawashukuru sana Wandishi na Wahariri wa habari za michezo na pia Wahariri Watendaji wa vyombo vya habari, kwa ushirikiano mzuri nanyi, ushirikiano na uhusiano wa uwazi ambao haukuwa na mikwaruzo ya aina yoyote kwa kipindi chote (Jan 2005-Jul 2013) tulichoshirikiana kwa pamoja kulitumikia soka la nchi yetu.

8.                   Namshukuru sana Rais wa TFF Ndg. Leodegar Tenga kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na kwa wanakamati niliokuwa nao katika kutekeleza majukumu ya umma. Miaka ishirini na tisa (29) iliyopita nilipata fursa ya kufanya kazi ya mpira miguu kwa mara ya kwanza na Ndg. Tenga, nikiwa nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Desemba 1984, wakati Ndg. Tenga alipojitolea kuifundisha timu ya Chuo Kikuu cha DSM. Tangu wakati huo hadi sasa imani  na  ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya umma niliopata kutoka kwa Ndg. Tenga haujawai kutetereka hata kwa siku moja. Ni faraja kubwa kwangu kufanya kazi hizi za umma chini ya kiongozi anayeheshimika na kuaminika na wadau wa soka hapa nchini, Afrika Mashariki na Kati, Afrika na familia ya soka Duniani kwa ujumla.

9.                   Mwisho, kwa viongozi na wadau wote wa mpira wa miguu, nawashukuru na nawatakia kheri, baraka  na mafanikio katika Uchaguzi Mkuu wa TFF na  ujenzi wa  soka la nchi yetu..

Asanteni.
 Deogratias J. Lyatto
19 Julai 2013, Dar es salaam, Tanzania.

Thursday, July 18, 2013

TFF YAFUMUA KAMATI ZAKE



JAJI Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto wataongoza kamati muhimu za za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoundwa baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa TFF Leodegar C. Tenga alitangaza jana.

Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa za Nidhamu na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.

Rais Tenga alisema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kikatiba kina jukumu la kuunda Kamati Ndogo za TFF na vyombo vya maamuzi.

“Tulitaka tuwe na watu solid (imara) na makini ambao watatuhakikishia tunakwenda vyema,” alisema Tenga akizungumzia uteuzi huo ambao unahitimisha mchakato wa mageuzi kwenye Shirikisho baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika mwezi Februari kusimamishwa kutokana na baadhi ya wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda FIFA.

Katika kumaliza tatizo hilo, FIFA ilituma ujumbe wake kusikiliza walalamikaji na watu wengine na baadaye kuagiza kuundwa kwa Kamati za Maadili na kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa TFF kwa ajili ya kuingiza vyombo hivyo kwenye katiba kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Tumezingatia pia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao walitaka kamati ziwe na majaji... lakini si rahisi kupata seating judges (majaji walio kazini) ndio maana tunawashukuru wale waliotuambia kuwa wako tayari kutusaidia.

“Tumetafuta majaji na mawakili waandamizi ambao tunaamini watatuhakikishia haki inatendeka na inaonekana inatendeka,” alisema Tenga na kuongeza kuwa pia walizingatia maombi ya wajumbe wengine watatu ambao walitaka kupumzika, akiwataja kuwa ni Deo Lyatto, Sylvester Faya na Idd Mtiginjollah.

Alisema kutokana na mfumo huo mpya, mambo yote yanayohusu masuala ya ndani ya uwanja sasa yatashughulikiwa na Kamati ya Nidhamu, wakati yale ya nje ya uwanja, ambayo yanawahusu viongozi na wanafamilia ya mpira wa miguu kwa ujumla, yatashughulikiwa na Kamati za Maadili.

Tenga alisema mabadiliko hayo pia yamegusa kamati nyingine mbili, yaani Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi ambayo sasa itaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni

Jaji Ihema ataongoza Kamati ya Rufaa za Maadili akisaidiwa na mwanasheria mwingine mwandamizi, Victoria Makani, huku Bi. Mguto, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza vyombo vya vya maamuzi ataongoza Kamati ya Maadili akisaidiwa na makamu wake Francis Kabwe, ambaye Msajili wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi huo, baadhi ya wajumbe wamehamishwa kutoka kamati moja hadi nyingine. Mhe. Murtaza Mangungu, ambaye awali alikuwa Kamati ya Rufaa za Uchaguzi, sasa ataingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili; Kamanda Mohamed Mpinga na Prof Madundo Mtambo wamehamishwa kutoka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi kwenda Kamati ya Maadili.

Wajumbe wapya kwenye Kamati hizo ni pamoja na kocha wa zamani wa Taifa Stars na Reli ya Morogoro, Mshindo Msolla na Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow wanaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; mwanasheria maarufu Evodi Mmanda anaingia kwenye Kamati ya Maadili; mwanasheria mwandamizi Mustapha Kambona ambaye anaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; Mhe. Mohamed Misanga ambaye anaingia kwenye Kamati ya Maadili na Kanali Iddi Kipingu, ambaye anasifika kwa kuendesha soka la vijana, anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Nidhamu.

Pia Mwanasheria Anne Steven Marealle anakuwa mjumbe kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi; Yohane Masale (Rufaa za Uchaguzi), Allen Kasamala (Rufaa za Uchaguzi);  Francis Kiwanga ambaye pia aningia kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi na mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau ambaye anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili.

Kamati ya Utendaji pia imefanya mabadiliko kwenye Kamati ya Waamuzi ambako mwenyekiti Said Nassoro na katibu Charles Ndagala wa Chama cha Waamuzi wanaingia kwenye kamati hiyo kushika nafasi ya Joan Minja na Riziki Majala.

Wajumbe wa Kamati hizo ni kama ifuatavyo:

Kamati ya Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani (m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza Mangungu.

Kamati ya Maadili: Bi Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod mmanda.

Kamati ya Rufaa za Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo, Ong’wanuhama Kibuta (m/mwenyekiti), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla, ACP Jamal Rwambow.

Kamati ya Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona (m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa na Mohamed Msomali.

Kamati ya Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga (m/mwenyekiti), A. Steven Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala.

Kamati ya Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Kamati ya Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde (m/mwenyekiti), Said Nassoro, Charles Ndagala na Mohamed Nyama.

HUMUD AISHUKIA AZAM



LICHA ya kiungo Abdulhalim Humud  ‘Gaucho’  wa Azam kufuzu majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini, ameshindwa kwenda huko kutokana na kufanyiwa kitu mbaya na Azam.

Humud alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, viongozi wa Azam wamekuwa wakimkwamisha kwenda Afrika Kusini kujiunga na Jomo Cosmos na anashindwa kuelewa ni kwa nini.

Kiungo huyo wa zamani wa Simba alisema, viongozi wa Azam walitakiwa kufanya mazungumzo na wenzao wa Jomo Cosmos kwa ajili ya uhamisho wake, lakini hadi sasa wameshindwa kufikia makubaliano kuhusu malipo ya ada ya uhamisho.

"Ni kama vile naelea katikati ya bahari, sielewi la kufanya,"alisema kiungo huyo, ambaye jina lake limeachwa katika usajili wa timu hiyo msimu ujao.

Humud alikwenda Afrika Kusini, Aprili mwaka huu na kufanya majaribio hayo Jomo Cosmos kwa wiki mbili na kufaulu. Baada ya majaribio hayo, viongozi wa Jomo Cosmos walimruhusu arudi nyumbani ili waweze kuwasiliana na Azam.

"Namshukuru Mungu kwamba nimeshayafanya ya kwangu na kufanikiwa, sasa nashindwa kuelewa kwa nini viongozi wa Azam wameamua kunikwamisha wakati walitakiwa kujua lini napaswa kwenda Afrika Kusini,"alisema kiungo huyo.

Humud alisema anayo barua aliyopewa na Azam, inayoeleza kwamba yeye ni mchezaji halali wa Jomo Cosmos ndiyo sababu waliamua kumwacha kwenye usajili wa msimu ujao wa ligi.

Kiungo huyo alisema kila anapowafuata viongozi wa Azam na kuwataka wamweleze hatma yake, wamekuwa wakimpiga chenga na hivyo kumweka kwenye wakati mgumu.

Alisema hata nauli ya kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio hayo, alijigharamia mwenyewe wakati alipaswa kulipiwa fedha hizo na Azam. Alisema alitumia dola 800 za Marekani kwa ajili ya safari ya kwenda na kurudi.

"Kila mmoja anasema lake. Hali hii inanipa hasira, napatwa na uchungu. Wanatupigia kelele tunashindwa kwenda nje, kumbe kikwazo ni wao wenyewe,"alisema mchezaji huyo.

Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrisa hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa vile kila alipokuwa akipigiwa simu, hakupokea wakati msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Iddi simu yake ilikuwa haipatikani.

Wednesday, July 17, 2013

BABA WA KIEMBA AILIPUA SIMBA



BABA wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Simba, Amri Kiemba ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumuuza mtoto wake kwa bei ya chini kwa klabu za nje zinazomuhitaji.

Akizungumza na Burudani mjini Dar es Salaam jana, baba huyo mdogo wa Kiemba, aliyejitambulisha kwa jina la Tano Ramadhani alisema, kitendo wanachokifanya Simba kutaka kumuuza mchezaji huyo kwa bei ya juu si halali.

Ramadhani alisema kwa vile mtoto wake amepata bahati ya kuitwa na Raja Casablanca ya Morocco kwenda kucheza soka ya kulipwa, aachwe aende akatafute maisha mapya.

"Viongozi wa Simba wanataka dau kubwa kutokana na kumfanya mchezaji huyo aonekane kama vile ana umri mdogo wakati umri halisi wa Kiemba ni miaka 29," alisema.

Ramadhani alisema viongozi wa Raja Casablanca wameshafika nchini mara kadhaa kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa Simba, lakini wamekuwa wakikwamishwa bila ya sababu za msingi.

Baba huyo alisema kinachotokea hivi sasa ni kama vile viongozi wa Simba wameamua kumuwekea ngumu Kiemba kuondoka baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili na kumlipa sh. milioni 35.

Amewataka viongozi wa Simba kuacha kuweka mbele maslahi yao binafsi, badala yake watazame mustakabali wa maisha ya mtoto wake, ambaye bado anataka kujiendeleza zaidi kisoka.

"Hata kama Simba wamempa Kiemba shilingi milioni 35, si watazirejesha kutokana na malipo
watakayopewa na Raja Casablanca? Wamuache aende Morocco kutafuta maisha mapya kwa sababu mafanikio yake pia ni ya taifa,"alisisitiza.

Ramadhani alisema yeye kama mzazi, anasikitishwa na uamuzi huo wa Simba kwa vile kiwango cha soka nchini bado kipo chini na Tanzania inahitaji kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka ya kulipwa nje ya nchi.

KAPOMBE HUYOOO UHOLANZI


BEKI kiraka wa klabu ya Simba na timu ya Taifa, Taifa Stars, Shomari Kapombe anaondoka nchini kesho kwenda Uholanzi kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.

Kapombe anaondoka nchini baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Kim ameridhia Kapombe kuondoka licha ya timu yake kukabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Uganda.

Taifa Stars imeweka kambi mjini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Kombe la CHAN dhidi ya Uganda itakayochezwa kati ya Julai 26 na 28 mjini Kampala.

Katika mechi ya awali iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars ilichapwa bao 1-0 na hivyo kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu kucheza fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Angetile, Kim ameridhia mchezaji huyo kwenda Uholanzi kwa kuzingatia kuwa, mafanikio yake yatakuwa sifa kubwa kwa Tanzania.

Kapombe anatakiwa kufanya majaribio hayo katika klabu ya FC Twente ya Uholanzi, ambayo inashiriki katika ligi kuu ya nchi hiyo.

Awali, Kapombe alitakiwa kuondoka nchini Juni 28 na baadaye Julai 15 mwaka huu kwenda Uholanzi, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na mechi muhimu dhidi ya Ivory Coast na Algeria.

Mbali na FC Twente, Kapombe pia anatarajiwa kufanya majaribio katika klabu zingine za ligi kuu ya Uholanzi.

MNIGERIA AMTIMUA KIIZA




UONGOZI wa klabu ya Yanga umeshindwa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamis Kiiza baada ya mchezaji huyo kushinikiza alipwe sh. milioni 45.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, Kiiza alikuwa anataka alipwe fedha hizo zote ndipo atie saini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo kwa miaka miwili.

Kwa mujibu wa habari hizo, uongozi wa Yanga ulitaka kumpa mchezaji huyo sh. milioni 20 ili aweze kutia saini mkataba huo mpya na kumaliziwa fedha zilizobaki baadaye.

"Jambo hilo limewaudhi viongozi wa kamati ya usajili ya Yanga na wameamua kuachana naye na kuendelea na mipango ya kumsajili mshambuliaji mpya kutoka Nigeria," kilisema chanzo hicho cha habari.

Mshambuliaji huyo mpya kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi aliwasili nchini juzi usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya Airways na kupokewa kwa mbwembwe na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.

Chukwudi, ambaye alikuwa akichezea klabu ya Heartland ya Nigeria, alitarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake jana kwa ajili ya kupimwa uwezo wake na Kocha Ernie Brandts kabla ya kupewa mkataba.

"Upo kila uwezekano wa nafasi ya Kiiza kuchukuliwa na Mnigeria kwa sababu Kiiza ameonyesha jeuri na kutaka alipwe fedha nyingi kuliko wachezaji wenzake," kilieleza chanzo hicho cha habari.

Awali, mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Musa Katabalo alitumwa kwenda Uganda kwa ajili ya kuzungumza na Kiiza na kufanikiwa kuja naye Dar es Salaam kwa mazungumzo zaidi.

Kiiza, ambaye alikuja nchini na kikosi cha Uganda, kilichocheza mechi ya michuano ya Kombe la CHAN dhidi ya Taifa Stars, alifanya mazungumzo na viongozi wa kamati ya usajili ya Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini walishindwa kufikia mwafaka.

Akizungumza na Burudani mjini Dar es Salaam juzi, Kiiza alisema bado yeye ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na klabu yoyote kwa vile mkataba wake na Yanga ulishamalizika.

Kiiza alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa kamati ya usajili ya Yanga na kusisitiza kuwa, walishindwa kufikia mwafaka baada ya viongozi hao kugoma kumlipa sh. milioni 45 kwa mara moja.

Mchezaji huyo hakuwa tayari kuweka wazi iwapo ni kweli aliamua kurejea katika klabu yake ya awali ya Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) kama baadhi ya vyombo vya habari nchini vilivyoripoti wiki iliyopita.

Wakati huo huo, Yanga leo inatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na Three Pillare ya Nigeria katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

UNAMKUMBUKA MOHAMED SALIM?




UNAPOTAJA jina la Mohamed Salim, bila shaka unawakumbusha mbali mashabiki wa soka nchini, hasa waliowahi kumshuhudia mwanasoka huyo alipokuwa akisakata kabumbu miaka ya 1970 hadi 1980.

Ni mchezaji aliyekuwa na kipaji cha aina yake katika kucheza soka, akiwa na mwili uliojengeka vyema na hivyo kuwapa usumbufu mkubwa mabeki wa timu pinzani katika kumkaba.

Salim (52) alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani. Alipoanza kucheza soka, alikuwa akicheza nafasi ya beki wa pembeni, baadaye akacheza nafasi ya beki wa kati, kiungo mkabaji na mwishowe akahamia nafasi ya ushambuliaji, ambayo alidumu nayo hadi alipostaafu soka.

Mshambuliaji huyu ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Coastal Union na timu ya mkoa wa Tanga kung'ara na kutamba kisoka nchini miaka ya 1970 kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao.

Salim pia ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza 1980 zilipofanyika nchini Nigeria. Katika fainali hizo, Taifa Stars ilifungwa na Nigeria na Misri na kutoka sare na Ivory Coast.

Wachezaji wengine waliokuwa wakiunda kikosi hicho wakati huo ni Juma Pondamali, Leopard Tasso, Mohammed Kajole, Ahmed Amasha, Salim Amir, Jella Mtagwa, Leodegar Tenga, Hussein Ngulungu, Omari Hussein, Peter Tino na Thuweni Ally. Kikosi hicho kilikuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama.

Akizungumza na Burudani mjini Tanga hivi karibuni, Salim alisema alianza kucheza soka tangu akiwa mdogo kabla ya kujiunga na timu ya kiwanda cha CIC (sasa Afritex Limited).

Alilazimika kuihama timu hiyo 1970 na kujiunga na Coastal Union baada ya viongozi wa CIC kumfuma akiichezea timu hiyo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi ya Zanzibar. Wakati huo ilikuwa hairuhusiwi mchezaji wa timu ya kampuni kuchezea timu ya mtaani.

Kabla ya kuhama CIC, Salim alisema viongozi wa timu hiyo waliamua kumpa adhabu kwa kumuhamishia katika kitengo, ambacho asingeweza kupata nafasi ya kucheza soka. Aliamua kuwasilisha malalamiko kwa viongozi wa Coastal Union, ambao walimtafutia kazi katika Kiwanda cha Mbolea cha Tanga.

Akiwa kwenye kiwanda hicho, Salim alisema aliweza kupata nafasi ya kuichezea Coastal Union muda wote bila kupata kikwazo chochote. Wakati huo, Coastal Union ilikuwa chini ya kocha marehemu Rashid Moyo

Salim alisema sababu kubwa iliyomfanya ahamie kwenye nafasi ya ushambuliaji ni maajabu aliyoyaonyesha katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Mchakamchaka 1973. Katika mechi hiyo, alianza kucheza nafasi ya beki wa pembeni kulia kabla ya kubadili namba kipindi cha pili na kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati.

"Mechi ilikuwa ngumu na kali. Tulikwenda mapumziko tukiwa hatujafungana. Kipindi cha pili nilimuomba kocha anihamishie nafasi ya ushambuliaji na nikafanikiwa kuifungia Coastal Union mabao matano, yote kwa kichwa. Kuanzia wakati huo, kocha akawa ananichezesha nafasi ya ushambuliaji,"alisema.

Salim alianza kuichezea Taifa Stars 1975 katika michuano ya Kombe la Chalenji ilipofanyika visiwani Zanzibar. Anakiri kwamba, kuteuliwa kwake kwenye kikosi hicho, kilichokuwa chini ya marehemu Mansour Magram, kulimsaidia kukuza kiwango chake kisoka kutokana na kukutana na wachezaji mbalimbali.

Mechi pekee anayoikumbuka alipokuwa akiichezea Taifa Stars ni dhidi ya Nigeria, iliyochezwa 1981. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Lagos, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na ziliporudiana mjini Dar es Salaam, Taifa Stars ilichapwa mabao
2-0.

"Ni mechi iliyojaa ushindani mkali. Nakumbuka baada ya mechi ya marudiano, tulilipwa posho ya shilingi alfu saba kila mchezaji," alisema Salim, ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara katika mji wa Abudhabi nchini Oman.

Siku chache baada ya mechi hiyo, Salim aliondoka nchini kwenda Abudhabi kucheza soka ya kulipwa, akiwa amepata baraka zote kutoka kwa Chama cha Soka nchini (FAT) na serikali. Alikuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kwenda kucheza soka ya kulipwa Arabuni kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Akiwa Abudhabi, Salim alijiunga na klabu ya Al Wahida, ambayo aliichezea kwa miaka 16 hadi 1996 alipoamua kustaafu soka kwa hiari yake kutokana na kupatwa na maumivu ya mguu.

Akiwa katika klabu hiyo, Salim aliwahi kuzawadiwa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa ligi 1985 baada ya kufunga mabao 20. Pia aliwahi kuzawadiwa gari jipya aina ya Benz kwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka.

"Nililazimika kustaafu soka kutokana na kusumbuliwa sana na maumivu ya mguu. Nilipofanyiwa uchunguzi hospitali, ikabainika kwamba, mishipa yangu ya damu ya mguu wa kushoto ilikuwa ikiziba,"alisema Salim.

Baada ya kustafu soka, uongozi wa Al Wahida uliamua kumteua Salim kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha pili cha timu hiyo na baadaye kupelekwa kusomea fani hiyo barani Ulaya. Baada kumaliza masomo, aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya vijana.

Salim alidumu kwenye kazi hiyo kwa miaka kadhaa kabla ya kuamua kuachana kabisa na soka na kujikita zaidi katika masuala yake binafsi, zikiwemo biashara mbalimbali.

Mwanasoka huyo mwenye uraia wa Oman na ambaye amekuwa akifika Tanga mara kwa mara kwa ajili ya kusalimia ndugu na jamaa alisema, tatizo kubwa linalomwamisha maendeleo ya soka nchini ni wachezaji wa sasa kutocheza kwa ari na kujituma kama ilivyokuwa enzi zao.

Alilitaja tatizo lingine linalokwamisha maendeleo ya mchezo huo kuwa ni uchezeshaji mbovu wa waamuzi, kukosa umakini katika kutekeleza majukumu yao na hivyo kuchangia kuwafanya wachezaji wawe wazembe.

"Kama kweli Tanzania imedhamiria kupiga hatua kimaendeleo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kuongeza umakini katika utendaji wake wa kazi, ikiwa ni pamoja na kuyafanyiakazi mapungufu yaliyopo sasa,"alisema.

Salim alisema ni vyema shirikisho hilo liandae utaratibu wa kuwashirikisha wadau wa mchezo huo katika kujadili na kuamua masuala mbalimbali muhimu kuhusu mchezo huo badala ya kuwatumia watu, ambao hawana ufahamu wa soka.

Alisema mapenzi waliyonayo baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo kwa klabu kubwa na kongwe nchini, yamechangia kudumaza maendeleo ya mchezo huo kwa sababu baadhi ya maamuzi yamekuwa yakitolewa kwa upendeleo.

Salim ametoa mwito kwa wachezaji chipukizi wenye vipaji kufanya jitihada binafsi za kutafuta nafasi za kucheza soka ya kulipwa nje ya nchi ili waweze kuinua maisha yao badala ya kuridhika na soka ya Bongo.

"Nawashauri wachezaji wetu wasibweteke na kuridhika na mafanikio madogo wanayoyapata hapa nchini. Waongeze bidii zaidi na ikiwezekana wapiganie nafasi ya kwenda kucheza nje ili kuongeza ujuzi na mapato yao,"alisema mkongwe huyo.

Mwanasoka huyo pia amewataka wachezaji wa Tanzania kuzingatia maelekezo ya makocha wao na kujipangia muda wa ziada wa kufanya mazoezi binafsi kwa lengo la kujiweka fiti zaidi kiafya.

"Kuna baadhi ya wachezaji huwa wanafanya vitu tofauti uwanjani na vile wanavyoelekezwa na walimu wao. Hili ni tatizo kubwa lililopo kwa wanasoka wa Tanzania. Wanapaswa kubadilika kwa kufanya kile wanachoelekezwa, sio kufanya wanavyotaka wao,"alisema.

Salim alisema mchezo wa soka kwa sasa umekuwa ukitoa ajira kubwa kwa vijana sehemu mbalimbali duniani, hivyo vijana wa Tanzania wanapaswa kuichangamkia ili waweze kunufaika kimaisha.

"Binafsi naipongeza sana serikali kwa kudhamiria kwa dhati kukuza kiwango cha soka nchini, kuajiri makocha wa kigeni na kuboresha miundombinu. Wanasoka wetu nao wanapaswa kuunga mkono jitihada hizi za serikali kwa kujituma zaidi uwanjani,"alisema.

KAJALA ATOA YA MOYONI



MSANII nyota wa filamu nchini, Kajala Masanja amewatahadharisha wasanii wenzake wa kike wawe makini wanapoanzisha uhusiano wa kimapenzi na wanaume.

Kajala amesema kutokuwa kwake makini kumchunguza mumewe, Faraja Chambo kabla ya kufunga naye ndoa, ndiko kulikomponza na kujikuta akijumuishwa katika kesi ya kutakatisha pesa.

Msanii huyo aliyenusurika kufungwa jela miaka saba, alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Mboni Show, kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha East Africa.

"Tusikurupuke, tuwachunguze wanaume zetu kabla ya kuanzisha nao uhusiano wa kimapenzi. Hapa nilipo sitaki tena mwanaume,"alisema.

Kajala alikiri kuwa, baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani, P Funky Majani, ambaye alidumu naye kwa zaidi ya miaka sita, alichanganyikiwa na kujitosa kimapenzi kwa mumewe bila kumchunguza.

"Nilichojua ni kwamba alikuwa anafanyakazi benki, mambo mengine muhimu sikuyachunguza,"alisema.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ilimtia hatiani Kajala katika makosa mawili na kumuhukumu kwenda jela miaka saba ama kulipa faini ya sh. milioni 13. Kajala alilipiwa faini hiyo na msanii mwenzake wa filamu Wema Sepetu.

Mumewe, Faraja alipatikana na hatia katika makosa matatu na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela ama kulipa faini ya sh. milioni 200. Tayari Faraja ameshaanza kutumikia kifungo hicho.

Kajala alisema hakutarajia katika maisha yake iwapo ingetokea siku Wema angejitolea kumlipia faini ya sh. milioni 13 ili kumnusuru kwenda jela.

"Mimi na Wema tulikuwa marafiki, lakini wakati napelekwa Segerea, hatukuwa tukizungumza, tulikuwa tumegombana. Lakini wakati nikiwa mahabusu, alikuja kunitembelea, tukazungumza na kumaliza tofauti zetu,"alisema Kajala.

"Wema ni mmoja wa wasanii waliokuwa wakija mara kwa mara kunitembelea Segerea. Wakati mwingine alipokuwa akija, askari wa magereza walikuwa wakimzuia kuniona, sielewi kwa nini,"aliongeza.

Kajala alisema siku alipohukumiwa kwenda jela ama kulipa faini, alilia kwa uchungu kwa sababu aliamini mwisho wake umefika. Alisema alianza kupata faraja baada ya wasanii, Mahsen Awadh 'Dk. Cheni' na Elizabeth Michael 'Lulu' walipomfuata na kumueleza kwamba, Wema amekwenda benki kuchukua fedha za kumlipia faini.

Msanii huyo alisema si kweli kwamba fedha alizozitoa Wema zilitoka kwa watu wengine. Alisema anachoamini ni kwamba, fedha zile zilikuwa za Wema na alikwenda kuzitoa katika akaunti yake benki.

Kajala alisema pia kuwa, si kweli kwamba amepewa masharti na Wema ya kulipa fedha hizo kupitia filamu mbalimbali atakazozicheza. Alisema hakuna masharti hayo kati yake na Wema.

Kutokana na kuthamini msaada huo wa Wema, Kajala alisema ameamua kuchora tattoo yenye jina la msanii huyo kwenye bega lake la mkono wa kiume. Alisema hatarajii kuifuta tattoo hiyo hata kama atagombana na Wema katika siku zijazo.

"Nimechora tattoo ya Wema kwa sababu namuonyesha jinsi gani namshukuru na kukithamini kitu alichonifanyia,"alisema Kajala na kusisitiza kuwa, tattoo hiyo itabaki daima kwenye bega lake vyovyote itakavyokuwa.

Kajala alisema amejifunza mengi kutokana na kuishi jela kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kurekebisha mwenendo wa maisha yake. Alisema Kajala wa sasa si yule wa zamani.

"Kabla ya kupatwa na matatizo haya, nilikuwa nikichukulia kila kitu rahisi rahisi. Nilikuwa natoka matembezini hovyo na kufanya lolote ninalotaka. Kwa sasa sifanyi tena mambo hayo. Nimeamua kutulia na familia yangu kwa sababu ndiyo iliyonithamini wakati wa matatizo,"alisema Kajala.

Kwa mujibu wa Kajala, alikuwa karibu na Lulu walipokuwa pamoja gereza la Segerea, ikiwa ni pamoja na kushiriki kufanya ibada kwa lengo la kumuomba Mungu awanusuru katika kesi zilizokuwa zikiwakabili.

Alisema kamwe hakuwahi kupata nafasi ya kutoka gerezani nyakati za usiku na kwenda kutanua kwenye klabu za burudani kama ilivyowahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari. Alisema habari hizo zilikuwa za uzushi.

Kajala alimtaja mfungwa mwenzake aliyekuwa akimsisimua kwa stori zake kuwa ni Mama Rama, ambaye pamoja na mwanawe, Rama walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya mtoto wa kike.

Tayari Mama Rama na mwanawe wameshaachiwa huru na mahakama baada ya 
kuonekana hawana hatia, lakini Rama amepelekwa hospitali ya Mirembe ya mkoani Dodoma kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi. Mirembe ni hospitali maalumu ya wagonjwa wa akili.

Alipoulizwa ni kesi zipi zinazowakabili wanawake wengi waliofungwa jela, Kajala alisema nyingi zinatokana na makosa ya kutupa watoto na zingine chanzo chake ni wanaume. Alisema wapo wanawake waliohukumiwa vifungo vya miaka 30 jela baada ya wanaume zao kukamatwa kwa ujambazi.

"Wanawake wengi walikamatwa wakiwa na wanaume zao kwa makosa ya ujambazi, lakini si kweli kwamba walishiriki katika matukio hayo,"alisema Kajala.

Akizungumzia mazingira ya jela, Kajala alisema walikuwa wakifunguliwa saa 10 alfajiri kwa ajili ya kuhesabiwa na kunywa uji kabla ya kupangiwa kazi za kufanya. Alisema kila ilipofika saa 10 jioni, walitakiwa kwenda kulala na ilipofika saa tatu usiku kengele ya kuwazuia kuzungumza ilikuwa ikipigwa.

Alikanusha madai ya kuwepo kwa vitendo vya usagaji jela kwa kusema kuwa, wafungwa na mahabusu wanalala taa zikiwa zinawaka na wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa kike.

Kajala anakumbuka siku moja akiwa kwenye karandinga la polisi, akitoka mahakama ya Kisutu kurudishwa Segerea, alimuona msanii Barnaba Elias maeneo ya Mnazi Mmoja na kila mmoja alitamani kuzungumza na mwenzake, lakini ilishindikana.

Msanii huyo mwenye sura na umbo lenye mvuto alisema baada ya kunusurika kwenda jela, alifanyiwa tambiko na baba yake kwa kummwagia maji mwilini kabla ya kuingia nyumbani. Alisema siku hiyo alikesha akimzungumzisha mdogo wake usiku kucha. 

Pamoja na kukumbwa na matatizo hayo na mumewe, Kajala alisema ataendelea kumuheshimu kwa vile walifunga ndoa kanisani na kwa mujibu wa sheria za dini ya kikristo, hawapaswi kuachana.

"Siwezi kumshiti mume wangu, akitoka jela salama, atanikuta. Ndoa za kikristo hakuna kuachana,"alisisitiza.

Alisema pia kuwa, hawezi kuwachukia watu wake wa karibu waliomtelekeza wakati wa matatizo kwa vile kila kitu kinatokea kutokana na mipango ya Mungu.

Akizungumzia matarajio yake katika fani ya filamu, Kajala alisema anatarajia kutengeneza filamu itakayozungumzia maisha yake, ikiwa ni pamoja na matatizo aliyoyapata.

"Nimeandaa stori ya maisha yangu kupitia movi. Itazungumzia mambo yote yanayonihusu, tangu nilipokuwa na P Funky hadi nilipokamatwa na polisi na kufunguliwa mashtaka na maisha yangu ya jela,"alisema.

Kajala alisema katika filamu hiyo, atawatumia baadhi ya wasanii maarufu na chipukizi
kwa lengo la kuwapa uzoefu na kukuza vipaji vyao.

WACHEZAJI SIMBA WATEMBELEA KABURI LA BABA WA TAIFA



WACHEZAJI wa timu ya soka ya Simba juzi walitembelea kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere lililopo nyumbani kwake kijiji cha Mwitongo kilichopo Butiama mkoani Mara.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana kuwa, mbali na kutembelea kaburi hilo, wachezaji wa timu hiyo pia walipata nafasi ya kuzungumza na familia ya Nyerere.

Kamwaga alisema ziara hiyo nyumbani kwa Baba wa Taifa, ilikuwa ni sehemu ya ziara ya Simba katika mkoa wa Mara, ambako inatarajiwa kucheza mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya timu za mkoa huo.

Kwa mujibu wa Kamwaga, Simba ilitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza jana dhidi ya Kombaini ya mkoa wa Mara kabla ya kuvaana na timu ya Polisi, ambayo ni mabingwa wa mkoa huo.

Ofisa huyo wa Simba alisema kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho kwa ajili ya pambano lao la kimataifa la kirafiki dhidi ya URA ya Uganda litakalofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika hatua nyingine, Kamwaga amesema maandalizi ya mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika keshokutwa yanaendelea vizuri.

Kamwaga alisema jana kuwa, mkutano huo utafanyika kwenye bwalo la maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam na amewataka wanachama wa Simba kujitokeza kwa wingi kuhudhuria.

Alisema wanachama watakaoruhusiwa kuhudhuria mkutano huo ni wale waliolipia kadi zao na kuonya kuwa, wanachama watakaothubutu kufanya fujo, watachukuliwa hatua za kisheria.

Monday, July 15, 2013

TBL YAIKABIDHI SIMBA MIL 20/- ZA MKUTANO MKUU



KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake maridadi ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 20, 2013 jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi hundi hiyo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Tunakabidhi fedha hizi ikiwa ni mwendelezo kutekeleza majukumu yetu kama mdhamini mkuu wa Simba SC. Kwa kuzingatia hilo tungependa kuona maendeleo ya klabu ya Simba uwanjani na nje ya uwanja,”.
“Tunaiunga mkono klabu hii katika mkutano wake mkuu tukiamini kuwa mkutano huu utaimarisha uhusiano uliopo kati ya klabu na wanachama wake kwa kuwapa fursa ya kuhakiki mwelekeo wa klabu yao waipendayo,”alisema.
“Ikiwa na mamilioni ya mashabiki nchini, klabu hii imejengeka kutokana na rekodi nzuri ya mafanikio kwa muda mrefu – na Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa sehemu ya klabu hii,”.
“Tunaamini kwamba mbali na wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba kuona timu yao ikishinda lakini pia tunatambua kwamba ni haki yao ya msingi kuwasiliana na klabu na kupata taarifa mbalimbali za mwenendo wa klabu,”.
“Kutokana na sababu hizi, sisi kama wadhamini wakuu wa klabu hii tunatoa mchango wa shilingi milioni ishirini ili kuunga mkono jitihada za klabu kuendelea kuwajibika kwa wanachama wake,”.
“Tunatambua wajibu wetu kama wadhamini wakuu wa Simba katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio huku tukiwaburudisha na bia yenu muipendayo Kilimanjaro Premium Lager – Bonge la Kiburudisho”.

TENGA AWASHUKURU WAJUMBE WA MKUTANO MKUU TFF



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa michango yao, na utulivu waliouonesha katika kupitisha marekebisho ya Katiba ya TFF ya 2013.

Amesema marekebisho hayo yatawasilishwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kupitishwa ili mchakato wa uchaguzi uweze kuanza mara moja.

“Tutamuomba Msajili atusaidie kusajili haraka Katiba yetu ya 2013 ili tuingie katika mchakato wa uchaguzi. Kama tulivyotangaza awali tumepanga kufanya uchaguzi Septemba 29 mwaka huu, na tusingependa tarehe hiyo ipite,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji.

Katika kikao chake, Kamati ya Utendaji  imepitisha Kanuni za Maadili, Kanuni za Nidhamu, na marekebisho kwenye Kanuni za Uchaguzi yanayotokana na kuundwa kwa Kamati ya Maadili.

STARS KAMBINI MWANZA



Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka leo asubuhi (Julai 14 mwaka huu) kwenda Mwanza ambapo itapiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Uganda (The Cranes) kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeondoka kwa ndege ya PrecisionAir na itafikia hoteli ya La Kairo wakati mazoezi yatafanyika Uwanja wa CCM Kirumba kulingana na programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.

Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala. Tarehe rasmi itapangwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Uganda (FUFA) siku kumi kabla ya mechi.

STARS, UGANDA ZAINGIZA MILIONI 113



Mechi ya kwanza mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) imeingiza sh. 113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 17,278,169.49 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 13,227,108.98, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 17,636,145.30 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,409,036.33.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 52,908,435.91 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,645,421.80 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Sunday, July 14, 2013

WAJUMBE WAPITISHA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF

MKUTANO TFF WAPITISHA MAREKEBISHO YA KATIBA




Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliofanyika leo (Julai 13 mwaka huu) umepitisha marekebisho ya Katiba yake, hivyo mchakato wa uchaguzi unatarajia kuanza wakati wowote.

Wajumbe zaidi ya 100 walihudhuria Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa NSSF Waterfron, Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aliyewataka wajumbe kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini kinakuwa.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga umefanya marekebisho ya Katiba kutokana na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). James Johnson kutoka Idara ya Wanachama ndiye aliyeiwakilisha FIFA katika mkutano huo.

Aprili mwaka huu FIFA ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF, na kuagiza kwanza yafanyike marekebisho ya Katiba ili kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili ambavyo ndivyo watashughulikia matatizo ya kimaadili kwa familia ya mpira wa miguu nchini.

Mbali ya kamati hizo, mabadiliko hayo pia yametengeneza ngazi mbili za kushughulikia masuala ya kinidhamu ambazo ni; Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Rufani ya Nidhamu.

Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais Tenga itakutana kesho (Julai 14 mwaka huu) kwa ajili ya kuteua wajumbe watakaounda Kamati hizo ili kuruhusu kuanza mchakato wa uchaguzi ambao FIFA iliusimamisha hadi vitakapoundwa vyombo hivyo.