Mabingwa watetezi wa michuano ya soka ya Kombe la Kagame, Yanga jana walianza vibaya utetezi wao baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico ya Burundi katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Katika mechi hiyo, Yanga inayonolewa na Kocha Tom Saintfiet, ilishindwa kuonyesha soka ya kuvutia, ikilinganishwa na wapinzani wao, ambao walicheza pasi za uhakika na kucheza kwa malengo.
Safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan na Ladslaus Mbogo haikucheza kwa uelewano na kukaribisha mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango lao.
Kupwaya kwa safu ya kiungo iliyokuwa chini ya Rashid Gumbo na Athumani Iddi 'Chuji' ndiko kulikochangia Atletico ifanye mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango la Yanga na hatimaye kupata mabao mawili yaliyofungwa na Didier Kavumbagu.
No comments:
Post a Comment