KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 27, 2016

HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA TFFMKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amemuomba Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amsamehe Mkuu wa Idara hiyo wa Yanga, Jerry Muro aliyefungiwa mwaka mmoja Julai mwaka huu.
Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3 Julai mwaka huu baada ya Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde kumtia hatiani kwa mashitaka mawili kati ya matatu.
Makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo.
Kwa kosa hilo alihukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja- wakati shitaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.
Katika shitaka hilo, Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Manara amemuomba Rais wa TFF kumsamahe Muro baada ya kutumikia karibu nusu ya adhabu yake.
"Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari amekwishatumikia karibia nusu ya kifungo chake,"alisema Manara.
"Nnajua kwa kufanya hivyo atakuwa amekwishajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. Nafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yalikwishapita na binafsi amenihakikishia hatorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wana Simba,"aliongeza Manara.
Aidha, Manara amemuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Muro, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru, hususan ikizingatiwa Muro si mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA TFFMKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amemuomba Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amsamehe Mkuu wa Idara hiyo wa Yanga, Jerry Muro aliyefungiwa mwaka mmoja Julai mwaka huu.
Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3 Julai mwaka huu baada ya Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde kumtia hatiani kwa mashitaka mawili kati ya matatu.
Makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo.
Kwa kosa hilo alihukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja- wakati shitaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.
Katika shitaka hilo, Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Manara amemuomba Rais wa TFF kumsamahe Muro baada ya kutumikia karibu nusu ya adhabu yake.
"Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari amekwishatumikia karibia nusu ya kifungo chake,"alisema Manara.
"Nnajua kwa kufanya hivyo atakuwa amekwishajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. Nafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yalikwishapita na binafsi amenihakikishia hatorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wana Simba,"aliongeza Manara.
Aidha, Manara amemuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Muro, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru, hususan ikizingatiwa Muro si mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

Monday, December 26, 2016

SIMBA YAIONYESHA UNDAVA JKT RUVU


SIMBA jana iliendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuichapa JKT Ruvu bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi la Simba lilifungwa na kiunga Muzamil Yassin dakika ya 45 baada ya kaz nzuri iliyofanywa na Pastory Athanas.

Kutokana na ushindi huo, Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 baada ya kucheza mechi 17, ikiwa mbele ya watani wao wa jadi Yanga, kwa tofauti ya pointi nne.

Timu hizo zilikianza kipindi cha kwanza kwa kushambuliana kwa zamu, huku safu za viungo za pande zote mbili zikionyeshana umahiri wa kutawala idara hiyo.

YANGA YABANWA MBAVU NA AFRICAN LYONMABINGWA watetezi Yanga jana walilazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na African Lyon katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Sare hiyo imeifanya Yanga iendelee kukamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 17, sawa na Simba inayoongoza kwa kuwa na pointi 38.

Matokeo hayo yalipokelewa kwa hasira na mashabiki wa Yanga, kufuatia wachezaji wa timu hiyo kugomea mazoezi kwa siku mbili mfululizo, wakishinikiza kulipwa mshahara wa mwezi Novemba.

Timu ya timu zote mbili kushambuliana kwa zamu katika kipindi cha kwanza, hadi kilipomalizika hakuna iliyoweza kupata bao.

Lyon ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 67, lililofungwa na Ludovic Venance baada ya kupokea pasi kutoka kwa Abdalla Mguhi.

Bao hilo halikudumu kwa muda mrefu, kwani Yanga ilifanikiwa kusawazisha dakika ya 74, kupitia kwa Amisi Tambwe, aliyemalizia krosi ya Juma Abdul.

Tuesday, December 20, 2016

WACHEZAJI YANGA WAMGOMEA LWANDAMINA MAZOEZINI

WACHEZAJI wa Yanga, jana walifanya mgomo wa mazoezi  asubuhi wakiushinikiza uongozi wa timu yao kuwalipa mishahara yao ya mwezi Novemba.

Yanga walitakiwa kufanya mazoezi saa tatu asubuhi. katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya African Lyon, utakaopigwa kwenye uwanja huo.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa vigogo wa Yanga, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wachezaji wote walifika uwanjani hapo saa tatu na nusu asubuhi.

Alisema baada ya kuwasili kwenye uwanja huo, waligoma kubadili nguo na kuvaa za mazoezi huku wakisisitiza kuwa hawatafanya mazoezi hadi hapo uongozi utakapowalipa mishahara yao.

Alisema licha ya Kocha George Lwandamina kutoka Zambia, kuwasihi wafanye mazoezi angalau kwa muda wa nusu saa, wachezaji hao walimuwekea ngumu na kumwambia msimamo wao upo pale pale hadi hapo watakapolipwa mishahara yao.

“Jumatatu iliyopita waligoma kuingia kambini kwa sababu hii hii, lakini tuliwasihi wasitishe mgomo ili wajiandae na mchezo wetu dhidi ya JKT Ruvu  walikubali.

“Tulicheza dhidi ya JKT Ruvu kwa morali ingawa tulikuwa na wasiwasi kuwa huenda  wakaharibu kwenye mchezo ule, lakini tulishukuru waliingia uwanjani na kucheza kwa moyo mmoja na ndio maana tulifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0,”alisema kiongozi huyo.

Alisema wachezaji walitegemea baada ya mchezo huo wangerekebishiwa madai yao, hali ambayo haijatekelezwa hadi sasa.

Alisema anadhani wachezaji hao wameona ufumbuzi wa suala hilo ni kutofanya mazoezi na kuendelea na mgomo wao.

Kutokana na mgomo huo, benchi la ufundi la Yanga lilifanya jitihada za kuwasiliana na uongozi ili kuona wanatatua vipi tatizo hilo ili wachezaji hao warejee kwenye morali ya kufanya mazoezi.

“Hadi sasa bado hatujajua suala hili litaisha muda gani, kama ni leo (jana) au kesho (leo), tunawasiliana na viongozi tujue tunafanyaje,”alisema.

Wachezaji wote wa Yanga walitimka uwanjani hapo ilipofika saa 4:30 na kurejea majumbani mwao kusubiri mustakabali wa madai yao.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikijikusanyia pointi 36 huku Simba ikiwa kileleni mwa ligi kwa kuwa na pointi 38.

Baada ya mchezo wao na African Lyon, Yanga itasafiri kwenda visiwani Zanzibar, kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo Yanga itaanza kurusha karata yake ya kwanza dhidi ya Jamhuri, mchezo utakaopigwa Januari 2 saa mbili usiku.

Monday, December 19, 2016

MREMBO WA PUETRO RICA ATWAA TAJI LA MREMBO WA DUNIA
MSANII DARASA APATA AJALI MBAYA YA GARI KAHAMASIMBA YAISHIKISHA ADABU NDANDA FCSIMBA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC jioni ya Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Ushindi huo, unaifanya Simba ifikishe pointi 38 baada ya kucheza mechi 16, ikiwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Josephat Bulali na Mohamed Mkono, dakika 45 za kwanza zilimalizika bila mabao.
Kiungo mpya wa Simba James Kotei kutoka Ghana alilazimika kumpisha Muzamil Yassin dakika ya 19 baada ya kuumia kufuatia kugongana na Nahodha wa Ndanda, Kiggi Makasi.
Kipa Mghana wa Simba alifanya kazi ya ziada dakika ya 20 kumzuia mshambuliaji chipukizi wa Ndanda, Riffat Khamis asifunge baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki.
Dakika saba kabla ya mapumziko, mshambuliaji wa Simba Ibrahim Hajib alipiga shuti zuri la mpira wa adhabu ambalo liliupita ukuta wa Ndanda, lakini likatoka nje sentimita chache.
Kipindi cha pili, Ndanda ilipata pigo dakika ya 52 baada ya beki wake Hemd Khoja kuumia na kushindwa kuendela na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Benito John.
Pengo la Khoja lilionekana wazi kuiathiri Ndanda, kwani baada ya hapo Simba wakaanza kuipenya ngome ya wenyeji wao kwa urahisi na kupata mabao mawili.
Mshambuliaji Muivory Coast wa Simba, Frederick Blagnon hakuamini macho yake dakika 59 baada ya mpira wa kichwa alioupiga kuunganisha krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuokolewa vizuri na kipa Jeremiah Kasubi.
Dakika moja baadaye, winga Shizza Kichuya akamdakisha kipa Kasubi shuti dhaifu la karibu ndani ya sita kufuatia pasi ya Mo Ibrahim.
Hatimaye Muzamil Yassin akaifungia Simba bao la kwanza kwa shuti kali dakika ya 63 akimalizia pasi ya Mo Ibrahim.
Baada ya bao hilo, Ndanda walionekana kupoteana na kuwaruhusu Simba kuuteka zaidi mchezo.
Hata hivyo. kuanzia dakika ya 80, Ndanda walitulia kidogo, ingawa Simba waliendelea kutawala mchezo.
Mo Ibrahim akaifungia Simba bao la pili dakika ya 91 akimalizia pasi ya kiufundi ya Muzamil.
Mechi nyingine za leo African Lyon imetoa sare ya 0-0 na Azam FC, Mbao FC imeilaza 1-0 Stand United na Mbeya wenyeji Prisons wameifunga 1-0 Maji Maji.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY

TFF YAPATA MKURUGENZI MPYA WA FEDHASHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemteua Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
Uteuzi huo umefanywa leo (Desemba 17, 2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
Aidha, Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili Richard Sinamtwa.
Wajumbe wengine walioongezwa kwenye Kamati hiyo ni Adam Mihayo na Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Joseph Mapunda ambaye ameomba kupumzika, wakati Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.

YANGA YAIENGUA SIMBA KILELENI MWA LIGI KUU BARAYANGA imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na kuishusha Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. Lakini Simba inaweza kurejea kileleni kesho ikishinda dhidi ya wenyeji, Ndanda FC mjini Mtwara.
Shujaa wa Yanga leo alikuwa ni winga Simon Happygod Msuva aliyefunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya kuseti moja kipindi cha kwanza.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Heri Sasii aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lililokuja baada ya muda mrefu wa timu zote kushambuliana kwa zamu, lilifungwa na beki Michael Aidan Pius aliyejifunga dakika ya 38 katika harakati za kuokoa krosi ya Simon Msuva iliyokuwa inafuatiliwa vizuri na winga Deus Kaseke. 
JKT Ruvu pamoja na kuondoka uwanjani baada ya nusu ya kwanza wakiwa nyuma, lakini walicheza vizuri na kupeleka mashambulizi mawili ya hatari langoni mwa Yanga ambayo yaliokolewa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.
Yanga nayo ilicheza vizuri pia, lakini wachezaji wake walishindwa kutengeneza nafasi nzuri za kufunga katika kipindi cha kwanza zaidi ya hiyo waliyotumia kupata bao la kwanza.
Dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili, kocha Mzambia wa Yanga, George Lwandamina alimtoa mshambuliaji Amissi Tambwe na kumuingiza kiungo Said Juma ‘Makapu’.
Mabadiliko hayo yaliifanya Yanga ianze kutawala sehemu ya kiungo na kupika mashambulizi yenye shibe hatimaye kupata mabao mawili zaidi.
Msuva alifunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 57 akimalizia krosi ya Kaseke baada ya kazi nzuri ya kiungo mwenzake Haruna Niyonzima. Msuva tena akafunga bao la tatu dakika ya 90 akimalizia pasi ya Niyonzima dakika ya 90.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm alikuwepo jukwaa kuu kufuatilia mchezo, wakati kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu alikuwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini.
Baada ya mchezo, kocha Lwandamina alisema timu haijaanza kucheza kwa kiwango chake kwa kuwa bao anajaribu wachezaji.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Mzima. Mwadui imeilaza 1-0 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City imelazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Ruvu Shooting imetoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY

U-23 SASA KUITWA KILIMANJARO WARRIORS


TIMU za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo hazikuwa na majina hatimaye zimepatiwa majina.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba kuanzia sasa U-23 ya wanaume itaitwa Kilimanjaro Warriors wakati ya wanawake itaitwa Kilimanjaro Starlets.
Uteuzi wa majina hayo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake kilichofanyika juzi (Desemba 17, 2016) mjini Dar es Salaam.
Timu hizo ambazo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki zitaanza maandalizi yake Januari mwakani, na wengi wa wachezaji watakaounda timu hizo zinazojiandaa kwa ajili ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020 watatoka katika timu za sasa za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20).
Mechi za mchujo (qualifiers) kwa ajili ya michuano ya Olimpiki ya 2020 zitaanza mapema mwaka 2019.

Thursday, December 15, 2016

NYOTA WATATU WAJIUNGA RASMI NA AZAM


UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha kuutarifu umma kuwa leo mchana imefanikiwa kuingia mkataba na wachezaji watatu, beki wa kati Yakubu Mohammed, kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo na winga Joseph Mahundi.

Zoezi hilo la kuingiana mikataba limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul Mohamed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Meneja wa timu, Phillip Alando.

Wakati Mohammed, 20, amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Aduana Stars ya Ghana, utakaomuweka kwenye viunga vya Azam Complex hadi Desemba 14, 2019 akiziba nafasi ya Pascal Wawa, huku Mpondo anayetokea Coton Sports ya Cameroon, kwa upande wake akisaini mwaka mmoja.

Nyota hao wawili wamepewa rasmi mikataba baada ya kulivutia benchi la ufundi la Azam FC kwenye majaribio waliyokuwa wakifanya ndani ya kikosi hicho.

Katika kuongeza makali kwenye eneo la ushambuliaji, Azam FC imemrejesha winga wake wa zamani aliyekulia Azam Academy, Mahundi, ambaye amesaini miaka miwili akitokea Mbeya City, alipomaliza mkataba baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Azam FC tunaamini ya kuwa ujio wa nyota hao, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajia kuanza wikiendi hii, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shirikisho Afrika (CC) mwakani.

Hivyo mashabiki wa Azam FC wasiwe na wasiwasi waendelee kuisapoti timu, kwani bado uongozi wa timu kwa kushirikiana na benchi la ufundi, una nia ya dhati ya kuipeleka mbele timu kufikia kwenye mafanikio yanayokusudiwa kwa kukiboresha kikosi kadiri inavyowezekana.

Wakati huo huo, Azam FC inapenda kuweka wazi taarifa ya kufikia makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji raia wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’, ambaye amepata timu nchini Vietnam na muda wowote kuanzia sasa atakwenda huko.

Azam FC inamtakia mafanikio mema Migi huko aendako na inapenda kumkaribisha muda wowote atakapojisikia kurejea tena hapa na katika kuziba nafasi yake tumeamua kumsajili Mpondo, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Cameroon kwenye kikosi kilichoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika nchini Rwanda mwanzoni mwa mwaka huu. 

MALINZI AWAPONGEZA VIONGOZI TOC

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), waliochaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika salamu zake za kuwapongeza viongozi hao, Rais Malinzi amesema huu ni wakati mwafaka wa kujipanga katika kufuzu michuano ya kimataifa tukianzia hii Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika Tokyo, Japan.

Kuonyesha namna TFF ilivyopjipanga kwa ajili ya maandalizi hayo, msimu huu imeendesha Ligi Kuu ya Soka Taifa kwa upande wa wanawake na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 23, lengo likiwa ni kupata timu ya kutafuta kufuzu.

Tumewaomba wanafamilia wa mpira wa miguu kupendekeza majina majina ya timu za taifa za wanawake na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 23 kabla ya timu hizo hazijaingia kwenye kalenda ya kutafuta timu za kufuzu kwa kushirikiana na TOC.

Kwa Malengo yote hayo na mengine, TFF inaahidi kushirikiana na TOC na vyama vingine vya michezo kikiwamo cha riadha ambacho pia kimepata viongozi wake hivi karibuni.

TFF inaamini itapata ushirikiano wa kutosha kutoka timu nzima ya Viongozi wa TOC watakaoongoza kwa miaka minne ijayo, kuanzia sasa hadi kipindi cha Olimpiki ya Tokyo 2020 ambao ni Rais Gulam Rashid aliyepata kura za ndiyo 48 na mbili za hapana na Makamu wa Rais, Henry Tandau aliyepata kura za ndiyo 44, tano zikimkataa na moja ikiharibika.

Wengine ni Katibu Mkuu, Filbert Bayi aliyetetea kwa kishindo nafasi yake hiyo baada ya kupata kura za ndiyo 49, huku hapana moja huku Katibu Msaidizi Suleiman Mohamed Jabir akichomoza kwa kura 49 huku moja ikimkataa na Mweka Hazina ni Charles Nyange kura za ndiyo 47 huku hapana ni tatu na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa Juma Khamis Zaidy kura 47, moja ikiharibika na hapana ni mbili.

Katika uchaguzi huo ulioendeshwa na kufanyika kwa utulivu mkubwa, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Uchaguzi, Wakili Lloyd Nchunga, aliwataja walioshinda nafasi tano za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Bara na kura zao kwenye mabano kuwa ni Irene Mwasanga (50), Noorelain Sharrif (48), Muharam Mchume (39), Amina Lyamaiga (32), na Donath Massawe (30).

Kwa upande wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Zanzibar walishinda ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Nasra Juma Mohamed (44), Katibu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Suleiman Ame Khamis (42), Mussa Abdulrabi Fadhi (37), Ramadhan Zimbwe Omar (33), na Sheha Mohammed Ali (30).

Kwa upande wa Wana Olimpiki, Mwanariadha wa kike, Zakia Mrisho alishinda kwa kura 49, Samuel Mwera kura 48 na Fabian Joseph kura 44. Nafasi za juu ambazo zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.

RFF SASA YAVALIA NJUGA TIBA YA MOYO KWA WACHEZAJIShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza mazungumzo na Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Muhimbili, Dar es Salaam.

TFF imeanza mazungumzo hayo, ili kwa pamoja waanze  kushiriana kutoa mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa afya kwa wanamichezo wa soka katika kushughulikia matatizo ya moyo.

Ni matumaini yetu kuwa mafunzo haya yataboresha uwezo wa madaktari wa mpira wa miguu sambamba na kusambazwa kwa vifaa maalumu vya tiba ya moyo kwenye klabu za soka nchini.

Hii ni hatua thabiti inayochukuliwa na uongozi wa TFF baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo kwa wachezaji ukiwamo ugonjwa wa ‘cardiac arrest’ ambao kwa taarifa za AWALI unaonyesha ndio uliosababisha kifo cha Mchezaji wa Mbao FC U20, Ismail Mrisho Khalfan.

Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.

 Kifo hicho kimegusa hisa za wanafamilia wengi wa mpira wa miguu akiwamo Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Bw. Gianni Infantino ambaye juzi alituma salamu za rambirambi kwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kilo cha ghafla cha Mchezaji.

Salaam Rais Infantino, zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Ndugu Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou.

Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya avijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.

Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.

Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza.

YAHAYA AJIWEKEA MALENGO CAF


MSHAMBULIAJI mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Yahaya Mohammed, ameweka wazi kuwa moja ya malengo yake makubwa ni kuisaidia timu hiyo kuingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Azam FC ndio wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano hiyo mwakani baada ya kuwa washindi wa pili katika Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) msimu uliopita ikifungwa na Yanga mabao 3-1 katika mchezo wa fainali.

Nyota huyo kwenye mechi yake tu ya kwanza kuichezea Azam FC alifanikiwa kufunga bao, lililokuwa la pili kwa mabingwa hao walipokuwa wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi iliyopita, ulioisha kwa sare ya 2-2, bao jingine likiwekwa kimiani na winga Enock Atta Agyei.

Mohammed aliyesajiliwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo akitokea Aduana Stars ya Ghana, ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa atahakikisha anafunga mabao kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili kuweza kutimiza hilo.

“Kombe la Shirikisho ni lengo langu kubwa, nataka kuisaidia Azam FC kuingia hatua ya makundi na mimi kuwemo kwenye kikosi kitakachoingia katika hatua hiyo, malengo yangu makubwa yapo huko,” alisema.

Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola kinachosisimua na kuburudisha koo pamoja na Benki ya NMB, imekuwa na kiu kubwa ya kufika hatua ya makundi ya michuano kwa miaka minne iliyoshiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika (mara moja Ligi ya Mabingwa na mara tatu Kombe la Shirikisho Afrika), ambapo mwaka huu iliishia raundi ya pili baada ya kutolewa na vigogo wa Tunisia kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2, ikishinda 2-1 nyumbani na kufungwa 3-0 ugenini.

Ujio wa VPL

Kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajia kuanza wikiendi hii, kwa Azam FC kuvaana na African Lyon katika Uwanja wa Uhuru Jumapili ijayo saa 10.00 jioni, Mohammed amesema kuwa atajitahidi kwa uwezo wake kama mshambuliaji kuweza kufunga mabao ili kutimiza malengo ya klabu.

“Mimi kama mshambuliaji kazi yangu ni kufunga, nimeanza vizuri kwa kufunga bao katika mechi yangu ya kwanza (Mtibwa Sugar), nimejipanga kuendeleza mazuri niliyoyaanza, japo haitakuwa kila siku lakini nitajitahidi kufanya mazuri kwa ajili ya Azam FC,” alisema.

Kupambana na vikombe

Mohammed aliongeza kuwa: “Nitajitahidi kufanya mazuri kama nilivyosema awali, nahitaji kujitoa kwa ajili ya Azam FC kushinda makombe na kufikia malengo ambayo walipanga kufikia.”

Upinzani VPL

Wakati Azam FC ikicheza na Mtibwa Sugar wikiendi iliyopita, Mohammed amejionea aina ya upinzani anaotarajia kukutana kwenye mechi za ligi, na kusema kuwa ameona viwango vya juu pamoja upinzani mkali.

“Unajua hili ni daraja la Ligi Kuu, hivyo lazima utegemee viwango vya hali ya juu, kwangu mimi nimejipanga vema na upinzani na sitaidharau timu yoyote, kitu cha kwanza kwangu kitakuwa ni kujitahidi kufanya mazuri kwa manufaa ya Azam FC,” alisema.

Alivovutiwa na Bocco

Wakati akisifu ushirikiano anaoonyeshwa na wachezaji wenzake wa Azam FC, nyota huyo wa zamani wa Aduana Stars na Asante Kotoko zote za Ghana, hakusita kumtaja Nahodha wa timu hiyo, John Bocco ‘Adebayor’, akisema kuwa ni mtu mzuri sana.

“Wachezaji wenzangu wote wako vizuri ni kama kaka zangu tokea niwasili hapa hasa Bocco (John) ni mtu mzuri sana, nawaheshimu wachezaji wenzangu wote wako vizuri sana,” alisema.

Rekodi zake

Mohammed amesajiliwa Azam FC akitoka kuwa mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana msimu uliopita, akitupia wavuni mabao 15 akizidiwa mawili na staa wa Liberty Proffesional, Latif Blessing, aliyefunga 17.

Staa huyo msimu uliopita aliweka rekodi ya aina yake ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya klabu ya Aduana kufunga mabao matatu kwenye mechi moja ‘hat-trick’ tokea timu hiyo ipande Ligi Kuu mwaka 2009, alifanya hivyo walipoichapa Sekondi Hasaacas 4-0.

Mbali na kuwahi kuichezea timu ya Taifa ya Ghana, mwaka juzi alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo waliochaguliwa kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

WALIOFUZU AZAM FC U17 DAR KUCHUJWA


MKUU wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, jana Jumatatu ameanza kazi jana ya kuwafanyia mchujo vijana wenye umri chini ya miaka 15 na 17 waliochaguliwa kwenye majaribio ya wazi ya mkoa wa Dar es Salaam katika mpango wa Kitaifa wa timu hiyo wa kutengeneza timu za vijana wa umri huo.

Ni vijana 34 tu waliohudhuria kati ya 46, kwenye siku hiyo ya kwanza, ambapo vijana hao waliweza kupimwa uzito na urefu kabla ya kuingia uwanjani kufanya mazoezi mepesi na kucheza mechi ndogo ndogo baina ya wao wenyewe.

Zoezi hilo litaendelea tena kesho Jumatano, ambapo Legg anatarajia kumalizia programu hiyo Alhamisi ijayo kwa kuwachuja vijana hao na kubakia na wale bora.

Vijana watakaochaguliwa kwenye orodha ya mwisho ya mkoa wa Dar es Salaam, wanatarajia kuungana na vijana wengine waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali katika zoezi hilo katika mchujo wa mwisho unaotarajia kufanyika hivi karibuni mwezi huu ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Tuesday, December 13, 2016

SIMBA HOI KWA MTIBWA SUGARMTIBWA Sugar imepata ushindi wa kufungia mwaka dhidi ya Simba SC, baada ya kuichapa mabao 2-1  jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog aliwaanzisha Waghana wote, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, lakini wakashindwa kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo.
Mtibwa Sugar ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza tu ya mchezo huo, mfungaji Stahmili Mbonde aliyefumua shuti kali lililompoita kipa mpya kutoka Ghana, Daniel Agyei baada ya kufanikiwa kuwapiga chenga mabeki wa Simba.
Simba ilicharuka na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar kutaka kusawaziha, hata hivyo safu ya ulinzi ya Wakata Miwa wa Manungu iliyokuwa ikiongozwa na Salim Mbonde ilisimama imara kuzuia hatari zote.
 Mtibwa Sugar ikafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 34 mfungaji Jaffari Salum aliyewapiga chenga mabeki wa Simba baada ya kupokea pasi nzuri ya Ally Shomary na kumchambua Agyei tena.
Dakika mbili baadae Simba wakapata bao, dakika ya 36 lililofungwa na kiungo wa zamani wa Mtibwa, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim kwa shuti la kushitukiza lililompita kwa urahisi, kipa Said Mohammed aliyekuw amezubaa.
Kipindi cha pili, Simba iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Mtibwa, lakini bado wapinzani wao hao waliendelea kuwa makini katika kujilinda.
Beki Janvier Besala Bokungu aliikosesha Simba SC bao la kusawazisha dakika ya 88 baada ya kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wa penalti kufuatia mshambuliaji Ibrahim Hajib kuangushwa na Nahodha na kiungo Shaaban Nditi.
Refa Michale Magoli aliwatoa kwa kadi nyekundu viungo Mohammed Ibrahim wa Simba na Mohammed Issa wa Mtibwa Sugar dakika ya 86 baada ya kupigana uwanjani.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY

SIMBA YATWAA UBINGWA KOMBE LA U20SIMBA SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Tanzania Bara, baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.

Katika mchezo huo ulifanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), timu zote zilionyesha kandanda safi.
 

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 mfungaji Moses Kitandu aliyemalizia pasi ya George Emmanuel, lakini Shaaban Iddi akaisawazishia Azam dakika ya 28.

Said Mohammed akaifungia Azam FC bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 57, kabla ya Said Hamisi kuisawazishia Simba dakika ya 83.


Katika dakika 30 za nyongeza baada ya 90 kukamilika kwa sare ya 2-2, si Simba ya kocha Nico Kiondo wala Azam ya kocha Iddi Nassor ‘Cheche’ iliyofanikiwa kuongeza bao.
 

Waliofunga penalti za Simba ni Calvin Faru, Said Hamisi, Mokiwa Perus, Vincent Costa na Moses Kitandu, wakati za Azam zilifungwa na Abbas Kapombe, Rajab Mohammed na Adolph Bitegeko huku ya Said Mohammed ikipanguliwa na kipa Ally Salum.

Sunday, December 11, 2016

LWANDAMINA AANZA KWA MAUMIVU YANGA


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABAO ya mawili mshambuliaji, Emanuel Martin yameipa ushindi wa 2-0 JKU ya Zanzibar dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jioni ya leo.
Mchezaji huyo wa zamani wa JKT Mlale, Martin alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akiunganisha kona iliyopigwa na Mbarouk Chande wakati la pili alifunga dakika ya 27 akimalizia pasi ya Nassor Mattar.
Baada ya mabao hayo, kocha Mzambia, George Lwandamina aliyejiunga na timu mwezi uliopita kutoka Zesco United ya kwao, alimtoa beki Pato Ngonyani na kumuingiza Andrew Vincent ‘Dante’.
Katika kipindi hicho, Yanga walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga, kwanza dakika ya 14 baada ya winga Geoffrey Mwashiuya kupiga mpira wa adhabu vizuri, lakini ukadakwa na kipa wa JKU Mohamed Abrahaman na ya pili dakika 21 winga Mmalawi, Obren Chirwa alipopiga shuti kali likatoka nje.
Kipindi cha pili, kocha mpya, Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila, wazalendo Juma Mwambusi na kocha wa makipa Juma Pondamali alibadilisha wachezaji 10.
Ally Mustafa 'Barthez' alimpisha Deogratius Munishi 'Dida', Hassan Kessy alimpisha Juma Abdul, Oscar Joshua alimpisha Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' alimpisha Vincent Bossou, Said Juma alimpisha Justin Zulu, Juma Mahadhi alimpisha Thabani Kamusoko, Matheo Antony alimpisha Donald Ngoma, Obrey Chirwa alimpisha Simon Msuva, Malimi Busungu alimpisha Amissi Tambwe na Geoffrey Mwashuiya alimpisha Deus Kaseke.
Pamoja na mabadiliko hayo, Yanga haikufanikiwa kupata japo bao la kufutia machozi mbele ya timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).
Lakini angalau jitihada zilionekana na lango la JKU lilitiwa misukosuko na kama si uhodari wa kipa wa timu hiyo ya Ligi Kuu ya Zanzibar, Yanga wangepata mabao.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez'/Deogratius Munishi 'Dida' dk46, Hassan Kessy/Juma Abdul dk46, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji Mngwali dk46, Pato Ngonyani/Andrew Vincent 'Dante' dk31, Nadir Haroub 'Cannavaro'/Vincent Bossou dk46, Said Juma/ Justin Zulu dk46, Juma Mahadhi/Thabani Kamusoko dk46, Matheo Antony/Donald Ngoma dk46, Obrey Chirwa/Simon Msuva dk46, Malimi Busungu/Amissi Tambwe dk46 na Geoffrey Mwashuiya/Deus Kaseke dk46.
JKU: Mohamed Abrahaman, Hafidhi Ally, Edward Mazunga, Khamis Abdallah, Issa Haidary, Fesail Salum, Mabrouk Chande, Is Haka Othumani, Nasoro Mattar, Emmanuel Martin na Mohammed Abdallah.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

SIMBA, AZAM KUKUTANA FAINALI YA KOMBE LA U20AZAM FC itakutana na Simba SC katika fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya usiku wa jana kuitoa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa penalti 4-2 katika mchezo wa Nusu fainali, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC U-20, kukata tiketi ya kuchuana na Simba kwenye mchezo wa fainali kesho Jumapili, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam saa 1.00 usiku.
Kama ilivyokuwa kwa Azam FC U-20, Simba nayo ililazimika kusubiri hadi changamoto ya kupigiana mikwaju ya penalti ili kuitoa Stand United, kufuatia muda wa kawaida wa mchezo na dakika 30 za nyongeza kuisha kwa sare ya bao 1-1 na hivyo wekundu hao kushinda 8-7.

Friday, December 9, 2016

AZAM KUJIPIMA NGUVU NA MTIBWA KESHOKATIKA kujiandaa vilivyo kuelekea mechi za raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kukipima kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi ijayo Desemba 10 saa 1.00 usiku.

Azam FC iliyoanza maandalizi ya mzunguko huo wa pili Jumatatu iliyopita, itautumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza mikikimikiki ya ligi, ambapo inatarajia kufungua pazia kwa kucheza na African Lyon Desemba 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Baadhi ya wachezaji wapya itakaowatumia katika mchezo huo ni washambuliaji Yahaya Mohammed (Aduana Stars) na Samuel Afful (Sekondi Hasaacas), ambao wametua nchini alfajiri ya leo Jumatano wakitokea nchini kwao Ghana sambamba na beki wa kati, Yakubu Mohammed (Aduana Stars) aliyekuja kufanya majaribio ya kujiunga na Azam FC.

Mabingwa hao wanawafanyia majaribio wachezaji wengine wawili kutoka Cameroon, beki wa kati Batetakang Flavius (Canon Yaoundé) na kiungo mkabaji Stephane Kingue (Coton Sport FC de Garoua), ambao nao wanatarajia kuwemo kwenye mtanange huo.

Hadi inamaliza raundi ya kwanza ya ligi, Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola kinachochangamsha mwili na kuburudisha koo pamoja na Benki bora kabisa nchini kwa sasa ya NMB, imejikusanyia jumla ya pointi 25 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa nyuma pointi 10 dhidi ya Simba (35).

Mbali na kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi, Azam FC pia inayatumia mazoezi hayo kujiandaa ipasavyo na michuano mingine ya Kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shiikisho Afrika (CC), ili iweze kufanya vizuri.

TFF YAMZAWADIA GARI MWAMUZI JONESIA RUKYAAWadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye hivi karibuni alichezesha vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika nchini Cameroon.

Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini miaka miwili iliyopita, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka, alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.

Umahiri wake, umevutia wengi wakiwamo wadau wa mpira wa miguu ambao hawakupenda kutajwa walioamua kumzawadia gari aina Toyota Vits ikiwa ni zawadi na kumbukumbu yake baada ya kuiwakilisha vema nchi.

Kwa upande wa TFF ilimtuza Mwamuzi Jonesia cheti cha kutambua uwezo na kufikia hatua ya kulitangaza shirikisho  na nchi kwa ujumla. Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ndiye aliyemkabidhi funguo za gari Jonasia.

Rais Malinzi alimsifu Jonesia kwa ujasiri na hatua aliyofikia na kumpa baraka za kumtakia mafanikio zaidi ya hapo ya kusonga mbele baada ya kufanya vema kwenye michuano ya Afrika Mashariki ya wanawake (CECAFA challange) na hiyo ya Wanawake Afrika.

“Ni Mtihani mkubwa to officiate (kuchezesha) mechi kubwa kama hiyo. Maana kila kosa linaweza kukuondoa na mafanikio ya kupata medali ya dhahabu kati ya waamuzi wanne ni hatua kubwa inayopaswa kutuzwa. Siwasemi FIFA, lakini itoshe kusema kuwa Jonasia unaweza kufika hatua ya kuchezesha fainali za kombe la dunia,” alisema Malinzi.

Rais Malinzi alipigia upatu kwa waamuzi wanaume nao kuandaliwa vema na kuchezesha michezo mikubwa ikiwamo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwani kinachohitajika ni mikakati tu na kuitekeleza.

“Kamati ya waamuzi nawaachia kazi hii. Maana kazi kubwa ya uamuzi ni kusoma na mazoezi,” alisema Malinzi mbele ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Waamuzi akiwamo Mwenyekiti wake, Saloum Chama.

Jonesia ambaye wakati wote alikuwa na faraja, alimshukuru Mungu kwa mafanikio aliyofikia pia wadau wote wakiwamo wazazi wake na bibi yake aliyemlea baada ya kufariki mama yake mzazi na viongozi mbalimbali ambao aliwaelezea kumtia moyo.

BEACH SOCCER: TANZANIA NA UGANDA KUCHEZA LEO


Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), leo Ijumaa Novemba 9, 2016 inatarajiwa kucheza na Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Viwanja vya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ni maandalizi kwa timu Tanzania na Uganda kujiandaa na michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la  CAF. TFF inatangaza kuwa mchezo huo hautakuwa na kiingilio.

Waamuzi wa mchezo huo watakuwa Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda anatarajiwa kuwa Idd Maganga.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu anatambia nyota wake 12 wakiwamo makipa Rajab Galla na Khalifa Mgaya.

Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.

Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya  kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa yAfrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.

NUSU FAINALI LIGI YA TFF U20 KUPIGWA LEO

Nusu fainali ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, inafanyika kesho Novemba 9, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala-nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Hatua hiyo itazikutanisha timu za Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Dar es Salaam katika mchezo utakaoanza saa 10.00 (16h00) kabla ya nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Simba ya Dar es Salaam na Stand United ya Shinyanga katika mchezo utakaofanyika kuanzia saa 1.00 )usiku (19h00).

Simba ilifikia hatua hiyo baada ya kuibuka kinara katika kundi A la michuano hiyo ambako ilifikisha pointi 17 na kuzishinda nyingine saba kama ilivyotokea kwa Azam FC ambayo pia ilifikisha pointi 17 katika kundi B ambalo kituo chake kilikuwa Kagera.

Michuano hiyo iliyochezwa kwa udhamini wa Azam Tv na Benki ya DTB yaani Diamond Trust Benk, iliziibuka Mtibwa Sugar ambayo ilishina nafasi ya pili kwa kituo cha Dar es Salaam kwa kujikusanyia pointi 14 kama ilivyotokea kwa Stand United ambayo pia ilishika nafasi ya pili katika kituo cha Dar es Salaam

HAYATOU ATUMA RAMBIRAMBI KWA MALINZI KIFO CHA KHALFAN
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (TFF), Bw. Issa Hayatou ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kifo cha ghafla cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan akiwa na umri mdogo wa miaka 19 baada ya kuzimia katika mchezo wa Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20,” ilisema sehemu ya barua hiyo ya Rais Hayatou kwenda kwa Rais Malinzi.

“Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF, familia nzima ya mpira wa Afrika na kwa niaba ya jina langu binafsi, tunapenda kupeleka rambirambi zetu kwa familia ya marehemu na familia ya mpira wa miguu katika Tanzania kwa ujumla wake kufuatia kifo hiki ambacho hakikutarajiwa,” ilisisitiza.

Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya vijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.

Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.

Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza. 

YANGA YATOZWA FAINI MILIONI 50 KWA KUMSAJILI HASSAN KESSY KABLA HAJAMALIZA MKATABA SIMBA
Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.

2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.

3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.

5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.

6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.

HATUA:

Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.

Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.

KIKOSI CHA TAIFA CHA U15 CHAMALIZA KAMBI MOROGORO, KINAKWENDA BURUNDITimu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 15, imemaliza ziara Morogoro kwa mafanikio baada ya jana Alhamsi Desemba 8, kuifunga Moro Kids mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kwa siku ya jana Ijumaa Desemba 9, mwaka huu timu hiyo ilijifua kwa mazoezi kwa mujibu wa programu ya Kocha Oscar Mirambo baada ya Morogoro kuleta timu ya wakubwa tofauti na vijana wenye umri wa chini ya miaka 15. Hivyo, mchezo huo wa pili haukufanyika.

Mazoezi na michezo hiyo ya kirafiki ambayo mingine wataifanya Zanzibar juma lijalo, ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi mchezo unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, mwaka huu kwenye Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Awali ilipangwa icheze na Shelisheli ambayo imetoa taarifa ya kuwa haijajiandaa.

Mara baada ya Morogoro, timu hiyo imerejea Dar es Salaam leo kujiandaa na safari ya kwenda Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.

Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana weeny umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.

Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.

Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma  Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.

Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.

Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.

Thursday, December 8, 2016

WAZEE WAZUIA MKUTANO SIMBASIMBA, YANGA KURUDIANA DESEMBA 18


MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unatarajiwa kuanza Desemba 17, mwaka huu wakati mchezo wa mahasimu wa jadi, Simba na Yanga utakuja Februari 18, mwakani.
Baada ya mapumziko ya tangu Novemba 10, kufuatia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza kitimutimu cha Ligi Kuu kinarejea Jumamosi ya Desemba 17, mabingwa watetezi, Yanga SC kufungua dimba na JKT Ruvu Stars Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mechi nyingine siku za siku hiyo, Mbeya City watamenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Mwadui na Toto Africans Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Vinara wa ligi hiyo, Simba wataanza kampeni ya kuwania taji la kwanza baada ya miaka minne Jumapili ya Desemba 18 watakapoifuata Ndanda Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, siku ambayo Mbao FC watamenyana na Stand United Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, African Lyon na Azam Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Prisons na Maji Maji Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

ZIARA YA TIMU YA TAIFA MPIRA WA MIGUU U15


Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 15, kesho Desemba 8, 2016 inaanza rasmi ziara ya mkoani Morogoro ambako watakuwa na mchezo wa kirafiki kesho jioni na keshokutwa asubuhi.

Vijana hao 22, walioko kambini kujiandaa Dar es Salaam wanajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha Bendera za Mataifa husika.

Mara baada ya Morogoro itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, timu hiyo itarejea Dar es Salaam jioni ya Desemba 9, 2016 kujiandaa na safari ya Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.

Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.

Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.

Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma  Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.

Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.

Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.

Wednesday, December 7, 2016

SAANYA, MPENZU WAPIGWA STOP KUCHEZESHA LIGI KUU
Waamuzi waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.

Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia daraja lengine la uamuzi.

Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.

Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.

Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake.

Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo kumalizika kwa vurugu.

Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.

kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.

Tuesday, December 6, 2016

HIVI NDIVYO MAUTI YALIVYOMKUTA MCHEZAJI WA MBAO FC

MAREHEMU Khalfan (kulia) akishangilia bao lake la kwanza
KHALFANI (kulia) akishangilia
Akipongezwa na mwenzake
AKIBEBWA kwa machela na kutolewa uwanjani

AKIPATIWA huduma ya kwanza
AKIWA na mchezaji mwenzake alipokwenda Ulaya

AKIPEWA huduma ya kwanza