KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, July 30, 2013

MAWAKALA WA WACHEZAJI KUTAHINIWA SEPT 26


Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI

Waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.

Mtihani huo utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika mtihani huo.

RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14

Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu.

Kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).

African Lyon (Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi B.

Timu za kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).

Tunapenda kukumbusha kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili ni Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TF

USAJILI WA WACHEZAJI LIGI KUU ENGLAND 2013/2014


 
Mshambuliaji Paulino aliyesajiliwa na klabu ya Tottenham akitokea Corinthians ya Brazil. Uhamisho wake umeigharimu Tottenham pauni milioni 17 za Uingereza.

ARSENAL
WAPYA
Yaya Sanogo (Auxerre, huru)
WALIOONDOKA
Andrey Arshavin (ameachwa), Denilson (Sao Paulo, huru) and Sebastien Squillaci (huru), Martin Angha (Nuremberg, ada haikutajwa), Craig Eastmond (Colchester, huru), Conor Henderson (ameachwa), Jernade Meade (Swansea, huru), Sanchez Watt (Colchester, huru), Johan Djourou (Hamburg, mkopo), Vito Mannone (Sunderland £2m), Francis Coquelin (Freiburg, mkopo), Junaid Meade (Swansea, huru)

ASTON VILLA
WAPYA
Aleksandar Tonev (Lech Poznan, £2.5m), Jores Okore (Nordsjaelland, ada haikutajwa), Leandro Bacuna (Groningen, ada haikutajwa), Nicklas Helenius (Aalborg, ada haikutajwa), Antonio Luna (Sevilla, ada haikutajwa), Jed Steer (Norwich, huru)
WALIOONDOKA
Richard Dunne (QPR, huru), Eric Lichaj (Nottingham Forest, huru), Jean Makoun (Rennes, ada haikutajwa), Andy Marshall (ameachwa), Derrick Williams (Bristol City, huru)

CARDIFF
WAPYA
Andreas Cornelius (FC Copenhagen, £8.5m)
WALIOONDOKA
Stephen McPhail (ameachwa), Heidar Helguson (ameachwa), Nat Jarvis (ameachwa)

CHELSEA
WAPYA
Andre Schurrle (Bayer Leverkusen, £18m), Marco van Ginkel (Vitesse Arnhem £9m), Mark Schwarzer (Chelsea, huru)
WALIOONDOKA
Jeffrey Bruma (PSV, £2.5m), Yossi Benayoun (ameachwa), Florent Malouda (ameachwa), Hilario (ameachwa), Ross Turnbull (ameachwa), Thibaut Courtois (Atletico Madrid,mkopo), Patrick van Aanholt (Vitesse Arnhem, mkopo), Oriol Romeu (Valencia, mkopo), Paulo Ferreira (amestaafu).

CRYSTAL PALACE
WAPYA
Dwight Gayle (Peterborough, £8.5m), Stephen Dobbie (Brighton, ada haikutajwa), Jerome Thomas (West Brom, huru), Jose Campana (Sevilla, £1.75m), Kevin Phillips (Blackpool, huru)
WALIOONDOKA
Jermaine Easter (Millwall, huru), Alex Marrow (Blackburn, ada haikutajwa), Jason Banton (MK Dons, mkopo)

EVERTON
WAPYA
Arouna Kone (Wigan, £5m), Antolin Alcaraz (Wigan, huru), Joel Robles (Atletico Madrid, ada haikutajwa), Gerard Deulofeu (Barcelona, mkopo)
WALIOONDOKA
Thomas Hitzlsperger (amachwa), Jan Mucha (ameachwa), Jake Bidwell (Brentford, ada haikutajwa), Phil Neville (amestaafu)

FULHAM
WAPYA
Sascha Riether (Cologne, £1.3m), Derek Boateng (Dnipro, ada haikutajwa), Fernando Amorebieta (Athletic Bilbao, huru), Maarten Stekelenburg (Roma, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Chris Baird (ameachwa), Simon Davies (ameachwa) Mahamadou Diarra (ameachwa), Mladen Petric (ameachwa), Mark Schwarzer (Chelsea, huru), Tom Donegan (ameachwa), Alex Smith (Swindon, huru), Dan Burn (Birmingham, mkopo)

HULL
WAPYA
George Boyd (Peterborough, huru), Maynor Figueroa (Wigan, huru), Curtis Davies (Birmingham, ada haikutajwa), Ahmed Elmohamady (Sunderland, £2m), Allan McGregor (Besiktas, £1.8m), Steve Harper (Newcastle, huru)
WALIOONDOKA
Sonny Bradley (Portsmouth, huru), Danny East (Portsmouth, huru), Mark Cullen (Luton, huru), Andy Dawson (Scunthorpe, huru), Jamie Devitt (ameachwa), Paul McKenna (ameachwa), Seyi Olofinjana (ameachwa), Jay Simpson (ameachwa), Jack Hobbs (Nottingham Forest)

LIVERPOOL
WAPYA
Kolo Toure (Manchester City, huru), Luis Alberto (Seville, £6.8m), Iago Aspas (Celta Vigo, £7.5m), Simon Mignolet (Sunderland, £9m)
WALIOONDOKA
Andy Carroll (West Ham £15.5m), Danny Wilson (Hearts, huru), Jamie Carragher (amestaafu), Jonjo Shelvey (Swansea, £6m), Suso (Almeria, mkopo)

MANCHESTER CITY
WAPYA
Fernandinho (Shakhtar Donetsk, £30m), Jesus Navas (Sevilla, £15m), Alvaro Negredo (Sevilla, £20.6m), Stevan Jovetic (Fiorentina, £25.8m)
WALIOONDOKA
Carlos Tevez (Juventus, £10m), Kolo Toure (Liverpool, huru), Wayne Bridge (Reading, huru), Ryan McGivern (Hibernian, huru), Roque Santa Cruz (Malaga, huru), Karim Rekik (PSV, mkopo), Jeremy Helan (Sheffield Wednesday, ada haikutajwa), Maicon (Roma, huru)

MANCHESTER UNITED
WAPYA
Guillermo Varela (Penarol, £1m)
WALIOONDOKA
Paul Scholes (amestaafu)

NEWCASTLE
WAPYA
Olivier Kemen (Metz, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
James Perch (Wigan, £700,000), Danny Simpson (QPR, huru), Steve Harper (Hull, huru)

NORWICH
WAPYA
Ricky van Wolfswinkel (Sporting Lisbon, £8.6m), Javier Garrido (Lazio, ada haikutajwa), Nathan Redmond (Birmingham, ada haikutajwa), Martin Olsson (Blackburn, ada haikutajwa), Carlo Nash (Stoke, huru), Leroy Fer (FC Twente, ada haikutajwa), Gary Hooper (Celtic, £5m)
WALIOONDOKA
Grant Holt (Wigan, £4m), James Vaughan (Huddersfield, ada haikutajwa), Jed Steer (Aston Villa, huru), Chris Martin (Derby, huru), Marc Tierney (Bolton, huru), Simeon Jackson (Eintracht Braunschweig, huru), Korey Smith (Oldham, huru), Elliott Ward (Bournemouth, huru), Tom Adeyemi (Birmingham, huru), George Francomb (AFC Wimbledon, huru), Lee Camp (ameachwa), Declan Rudd (Preston, mkopo).

SOUTHAMPTON 
WAPYA
Dejan Lovren (Lyon, £8.5m), Victor Wanyama (Celtic, £12m)
WALIOONDOKA
Vegard Forren (Molde, ada haikutajwa), Frazer Richardson (ameachwa), Danny Butterfield (ameachwa), Danny Seaborne (ameachwa), Ryan Dickson (ameachwa), Ben Reeves (MK Dons, huru), Sam Hoskins (Yeovil, huru)

STOKE
WAPYA
Erik Pieters (PSV, £3m), Marc Muniesa (Barcelona, huru)
WALIOONDOKA
Dean Whitehead (Middlesbrough, huru), Carlo Nash (Norwich, huru), Matthew Upson (Brighton, huru), Rory Delap (ameachwa), Matthew Lund (Rochdale, huru), Mamady Sidibe (ameachwa), Michael Owen (amestaafu)

SUNDERLAND
WAPYA
Modibo Diakite (Lazio, huru), Duncan Watmore (Altrincham, ada haikutajwa), Valentin Roberge (Maritimo, huru), Cabral (Basle, huru), David Moberg Karlsson (IFK Gothenburg, huru), Vito Mannone (Arsenal, £2m), Jozy Altidore (AZ Alkmaar, £6m), El Hadji Ba (Le Havre, ada haikutajwa), Emanuele Giaccherini (Juventus, £8.6m)
WALIOONDOKA
Ahmed Elmohamady (Hull, £2m), Titus Bramble (ameachwa), Matthew Kilgallon (Blackburn, huru), Ryan Noble (ameachwa)

SWANSEA
WAPYA
Wilfried Bony (Vitesse Arnhem, £12m), Jose Canas (Real Betis, huru), Jordi Amat (Espanyol, £2.5m), Jonathan De Guzman (Villarreal, mkopo), Alejandro Pozuelo (Real Betis, £425,000), Jonjo Shelvey (Liverpool, £6m), Gregor Zabret (NK Domzale, ada haikutajwa), Alex Gogic (Olympiacos, huru), Jernade Meade (Arsenal, huru) 
WALIOONDOKA
Mark Gower (Charlton, huru), David Cornell (St Mirren, mkopo), Kyle Bartley (Birmingham, mkopo)

TOTTENHAM
WAPYA
Paulinho (Corinthians, £17m), Nacer Chadli (FC Twente, £6m)
WALIOONDOKA
William Gallas (ameachwa), John Bostock (Royal Antwerp, huru), David Bentley (ameachwa), Jake Nicholson (ameachwa), Massimo Luongo (Swindon, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION
WAPYA
Goran Popov (Dynamo Kiev, mkopo)
WALIOONDOKA
Jerome Thomas (Crystal Palace, huru), Gonzalo Jara (Nottingham Forest, huru), Marc-Antoine Fortune (Wigan, huru), Zoltan Gera (ameachwa)

WEST HAM
WAPYA
Andy Carroll (Liverpool, £15.5m), Razvan Rat (Shakhtar Donetsk, huru), Adrian (Real Betis, ada haikutajwa), Danny Whitehead (Stockport County, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Rob Hall (Bolton, huru), Carlton Cole (ameachwa), Gary O'Neil (ameachwa)

Monday, July 29, 2013

YANGA YASHTUKIA JANJA YA AZAM TV


YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.


“HIVI karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:

Watata; Viongozi wa Yanga SC, kutoka kulia Balozi Ammy Mpungwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini, Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji, Waziri George Mkuchika, Mwenyekiti Baraza la Wadhamini, Francis Kifukwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini na Clement Sanga, Makamu Mwenyekiti wa klabu .

1. BODI YA TPL

1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.

1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.

1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA

2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.

2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.

2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.

2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:

2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;

2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;

2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.

3. MIGOGORO YA MASLAHI

3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.

3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.

3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.

4. KUTOKUWA NA UWAZI

4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).

4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.

5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA

5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."

5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo

wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.

Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.

Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.

(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013

Saturday, July 27, 2013

TAIFA STARS YATOLEWA KOMBE LA CHAN
MATUMAINI ya timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa wachezaji wa ndani leo yameota mbawa baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Uganda.

Taifa Stars imepokea kipigo hicho katika mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Kampala, Uganda na kuifanya itolewe kwa jumla ya mabao 4-1, kufuatia kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili zilizopita mjini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Frank Kalanda ndiye aliyeibeba Uganda baada ya kuifungia mabao mawili kati ya matatu. Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.

Frank aliifungia Uganda bao la kwanza dakika ya 10 baada ya kutokea kizaazaa kwenye lango la Taifa Stars kutokana na mabeki wake kujichanganya.

Taifa Stars ilisawazisha dakika ya 14 kwa bao lililofungwa na Amri Kiemba, aliyeunganisha wavuni krosi maridhawa kutoka pembeni ya uwanja iliyopigwa na Mrisho Ngasa.

Bao la pili la Uganda lilifungwa kwa njia ya penalti na Brian Majweda dakika ya 48 baada ya beki David Luhende kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Kosa lililofanywa na kiungo Salum Abubakar dakika ya 62 kutaka kuwapiga chenga mabeki wawili wa Uganda, liliigharimu Taifa Stars baada ya kiungo huyo kupokonywa na mpira na Hassan Waswa, akamgongea Majwega, naye akamsogezea Kalanda aliyefunga bao la tatu.

Friday, July 26, 2013

TAIFA STARS YATUA UGANDA, MECHI KUCHEZWA KESHOTaifa Stars imewasili salama hapa Kampala tayari kwa mechi ya marudiano ya mchujo dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Stars ambayo iliwasili ikitokea jijini Mwanza ilipokuwa imepiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itakwenda Afrika Kusini mwakani imefikia hoteli ya Mt. Zion iliyoko eneo la Kisseka katikati ya Jiji la Kampala.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen ameridhishwa na kiwango cha hoteli hiyo, kwani ndiyo ambayo timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) ilifikia Novemba mwaka jana ilipokuja Kampala kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Stars ambayo ilitiwa chachu na Rais Jakaya Kikwete alipokutana nayo Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati ikiondoka kuja Kampala, na kuitakia kila la kheri itafanya mazoezi yake ya mwisho kesho (Julai 26 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kujiandaa kwa mechi ya Jumamosi.

Kocha Kim amesema ingawa mechi hiyo ni ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda kwani wachezaji wako wako vizuri na ari kwa ajili ya mechi iko juu.

Wachezaji wote wako katika hali nzuri, isipokuwa Khamis Mcha aliyekuwa na maumivu ya goti, lakini kwa mujibu wa madaktari wa timu anaendelea vizuri kwani tayari wanampa mazoezi mepesi.

Kikosi cha kamili cha Stars ilichoko hapa kinaundwa na makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.

Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.

Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jumatatu (Julai 29 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Thursday, July 25, 2013

KIOTA KIPYA CHA MARAHA CHA SERENGETI GOLDEN PARADISE, MBANDE, MBAGALA, DAR ES SALAAM

 

Hoteli ya Serengeti Golden Paradise Resort  imeleta mapinduzi makubwa katika kutoa huduma za hoteli na burudani ya muziki katika maeneo ya Mbande, Mbagala, ambayo yako pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

Licha ya ukumbi wa hoteli hiyo kuwa wa kisasa na wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi kwa wakati mmoja, unaweza kuonekana mdogo kutokana na kujitokeza kwa umati mkubwa wa watu wakati wa maonyesho mbalimbali.
Meneja wa hoteli hiyo, Wambura Sungura anasema kuzinduliwa kwa ukumbi huo kumeleta faraja kubwa kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kutokana na kupata huduma, ambazo wamekuwa wakizikosa na badala yake kulazimika kusafiri kwenda mbali kuzitafuta.

“Kwa sasa ni kama kuunga mkono mpango wa serikali wa kuhakikisha huduma zote muhimu kama hizi za hoteli zinapatikana nje ya miji ili kupunguza kila kitu watu wakifate mjini, matokeo yake kusababisha msongamano mjini bila sababu za msingi,”anasema.
“Pia siku hizi watu hawataki bugudha mijini, badala yake wanataka kwenda sehemu tulivu na zenye hadhi kama hizi kwa kupumzika baada ya shughuli za wiki nzima, hali inayowafanya watafute sehemu nzuri za kupumzika na sehemu za namna hii ni nzuri kwao,”anasema Sungura.

Meneja huyo anasema wameandaa utaratibu wa kuvialika vikundi mbalimbali vya burudani kila mwisho wa wiki ili kutoa fursa kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kutohangaika kusafiri umbali mrefu kwenda mjini au maeneo mengine kutafuta burudani.

“Tunataka watu wasiwe wanahangaika kutoka hapa kutafuta burudani, tutajitahidi kuhakikisha kuwa kila wasanii wanaopendwa na wateja tunawaleta ili kukoga nyoyo zao,”anasema.

Anaongeza kuwa, kwa sasa wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo malazi, vinywaji na chakula, kitu ambacho kama  mteja akifika hapo hawezi kujutia nafsi yake, badala yake atakuwa anatamani kwenda kupata huduma mara kwa mara.
Anasema pamoja na kufungua hoteli hiyo, wanashiriana na wateja kupata maoni yao juu ya namna bora ya kuboresha huduma ili kuleta mageuzi makubwa katika kutoa huduma bora zaidi.

Wednesday, July 24, 2013

OWINO AOTA MBAWA SIMBAJUHUDI za viongozi wa klabu ya Simba kutaka kumrejesha beki wa zamani wa timu hiyo, Joseph Owino kutoka Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), zimegonga mwamba baada ya kukosekana pesa za kumlipa.
Mbali ya kukosekana kwa pesa anazotaka mchezaji huyo, uongozi wa URA  umegoma kumuuza Owino kwa Simba kwa vile amepata ofa nzuri ya kwenda kucheza soka ya kulipwa Qatar, Vietnam na China.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, wameshafanya mazungumzo na Owino na kukubaliana naye mambo kadhaa, lakini dau analotaka ni kubwa.
Hata hivyo, Hanspope hakuwa tayari kutaja dau hilo, lakini alisisitiza kuwa bado wanaendelea na juhudi za kutafuta pesa ili waweze kukamilisha usajili wa mchezaji huyo.
Owino aliichezea Simba msimu wa 2009/2010 akiwa na Emmanuel Okwi na Hilaly Echessa kutoka Kenya na kuiletea mafanikio makubwa, lakini aliachwa msimu uliofuata baada ya kuumia goti.
Baada ya kuumia, beki huyo mahiri alipelekwa India kupatiwa matibabu na aliporea nchini alijiunga na Azam FC, lakini alishindwa kuichezea kutokana na kukosa namba na kuamua kurejea Uganda.
Owino alionyesha umahiri mkubwa katika mechi mbili za kirafiki za kimataifa, ambazo URA ilicheza dhidi ya Simba na Yanga. Katika mechi hizo zilizochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, URA iliichapa Simba mabao 2-1 kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Yanga.
"Kimsingi tumeshazungumza na Owino na ameikubali ofa tuliyompa ili aweze kurudi tena Simba, lakini bado kuna masuala yanayohusu pesa, ambayo hatujayakamilisha,"alisema Hanspope.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili ya Simba alisema, kutokana na benchi la ufundi kuvutiwa na kiwango cha beki huyo, watafanya kila wanaloweza kuhakikisha anarejea Msimbazi na kucheza katika ligi kuu msimu ujao.
Wakati Simba ikiwa katika mikakati hiyo, Meneja wa URA, Sam Okabo amesema hawawezi kumruhusu Owino arejee Simba kwa sababu ampata ofa nzuri Marekani na Asia.
Okabo alisema jana kuwa, si rahisi kwa Owino kurejea Simba kama viongozi wa klabu hiyo wanavyotaka kwa vile mchezaji huyo ni lulu kwa sasa na anawindwa na klabu nyingi.
Kwa sasa, Simba imesaliwa na wachezaji wawili wa kigeni, Abel Dhaira na Hamis Tambwe baada ya uongozi kuvunja mkataba wa Mussa Mudde na pia kusitisha mpango wa kumsajili Robert Ssenkoom kutokana na benchi la ufundi kutoridhishwa na kiwango chake.
Katika hatua nyingine, Hanspope amesema mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Hamis Tambwe kutoka Burundi anatarajiwa kuwasili nchini Jumanne na kujiunga na timu hiyo kwenye kambi yake iliyopo Mbamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam.

CHOMBO AREJESHWA MSIMBAZIUONGOZI wa klabu ya Simba umeamua kumrejesha kiungo wake, Ramadhani Chombo 'Redondo' na tayari amejiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Mbamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Chombo alijiunga na wenzake juzi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Kamwaga alisema mchezaji huyo amerejeshwa kundini baada ya kuomba radhi kwa uongozi na kusamehewa.
Chombo ni miongoni mwa wachezaji watano wa Simba waliosimamishwa msimu uliopita kwa makosa ya nidhamu. Wengine ni Haruna Moshi 'Boban' na Juma Nyoso waliojiunga na Coastal Union ya Tanga.
Kamwaga alisema kwa sasa Simba inajiandaa kwa mechi moja ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu moja kutoka nje itakayochezwa wakati wa tamasha la Simba Day. Hata hivyo, hakutaja jina la timu hiyo.
Alisema Kocha Abdalla Kibadeni ameomba kambi hiyo ili kuwatengeneza wachezaji kimwili, kiakili na kisaikolojia.
Wakati huo huo, Kamwaga amesema mshambuliaji Kigi Makassy anatarajiwa kwenda India katikati ya mwezi ujao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya goti.
Kamwaga alisema jana kuwa, uongozi wa Simba umefanikiwa kupata miadi na madaktari wa India kwa ajili ya kumfanyia operesheni mchezaji huyo Agosti 18 mwaka huu.

SHARP STRIKERS FOUNDATION YAPANIA MAKUBWA KISOKASOKA ya vijana ndio moyo wa mpira wa miguu nchini. Kwa maana hiyo, kama uwekezaji kwa vijana utafanyika kwa umakini na juhudi kubwa, taifa litapiga hatua kubwa kisoka.
Hakuna nchi iliyofanikiwa duniani katika mpira wa miguu au mchezo wowote bila kuwekeza kwa vijana, ambao ndio nguzo kubwa katika mafanikio.
Kwa kutambua umuhimu huo wa kuwekeza kwa vijana, Sharp Strikers Foundation imejikita katika kuwaendeleza vijana, ambao watakuja kuwa tegemeo katika mchezo wa soka nchini.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Salim Mshamu anasema, Sharp Strikers Foundation inajumuisha mafunzo ya mpira wa miguu kwa watoto wa chini ya miaka 17.
Taasisi hiyo ilianzishwa 2011 kwa kuwafanyia usaili watoto kutoka shule mbalimbali za wilaya ya Korogwe.
“Academy hii ipo katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga na mpaka sasa ina jumla ya watoto 27,”ameeleza Mshamu.
Anasema kuwa ili mtoto aendelee kuwa katika ‘Academy’ hiyo, anatakiwa kufanya vizuri katika masomo yake na kama atafanya vibaya , atasimamishwa na uongozi mpaka pale atakapofanikiwa kujituma katika masomo yake shuleni.
Anaeleza kuwa, wanazingatia masomo kwa kutambua kwamba kwa sasa lazima mchezaji awe wa kisasa kwa kuwa na elimu itakayomwezehaa kufanya mambo kwa umakini mkubwa.
“Kama anafanikiwa kufanya vizuri katika masomo yake, atarudishwa na kuendelea na mafunzo,”ameeleza.
Mshamu anaeleza kuwa, tangu walipoanzisha ‘academy’ hiyo, wameshacheza mechi 25, wameshinda 18, wamefungwa tatu na kutoka sare mechi nne.
“Mechi kubwa tuliyocheza ilikuwa dhidi timu ya Azam ya vijana wa chini ya miaka 17. Mechi ya awali tuliweza kuwafunga mabao 4-0 na katika mechi ya marudiano walitufunga mabao 3-1,”amesema.
Kwa mujibu wa Mshamu, mechi hizo zilichezwa wiki iliyopita katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Alisema timu hiyo ilikuwa imefikia katika hoteli ya Serengeti Golden Paradise
Resort, iliyopo Mbande, Mbagala, Dar es Salaam.
Mshamu anasema waliamua kufikia katika hoteli hiyo kutokana na kuwa katika mazingira mazuri kwa utulivu na hivyo kuwapa fursa nzuri vijana wao kuzingatia mafunzo.

NSAJIGWA: KLABU ZIACHE KASUMBA YA KUAJIRI MAKOCHA WA KIGENI


SHADRACK Nsajigwa 'Fuso' ni jina maarufu katika soka ya Tanzania. Ni beki aliyejizolea sifa kemkem kutoka kwa mashabiki wa mchezo huo nchini kutokana na uwezo wake wa kuwadhibiti washambuliaji wa timu pinzani na pia kupanda mbele kusaidia mashambulizi. Katika makala hii ya ana kwa ana iliyoandikwa na ATHANAS KAZIGE, nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, ambaye amestaafu soka, anaelezea mikakati yake katika kazi yake mpya ya ukocha wa soka.

SWALI: Hongera kwa kuhitimu mafunzo ya ukocha wa soka na pia kuajiriwa na klabu ya Lipuli ya Iringa ukiwa kocha mkuu. Ni kipi kilichokuvutia ukaamua kujitosa kwenye fani hiyo?

JIBU: Mchezo wa soka upo kwenye damu yangu. Nilishajipanga mapema kwamba,baada ya kustaafu soka, niendelee kutoa mchango wangu katika mchezo huo kwa kufundisha timu za madaraja mbalimbali.Ni ndoto niliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Ndio sababu kabla hata sijaamua kustaafu soka, nilianza kuchukua mafunzo ya ukocha wa mchezo huo kuanzia katika ngazi mbalimbali na leo hii naweza kujivuna kwa kufanikisha azma yangu hiyo kwa vile ninacho cheti cha kuniwezesha kupata kazi ya ukocha sehemu yoyote hapa nchini na kwa kuanzia, nimeanza kazi hiyo Lipuli.

Mbinu nyingi za kufundisha soka nimezipata kupitia mafunzo mbalimbali niliyopita, lakini nyingine nimezipata kwa sababu ya utundu kutokana na kufundishwa na makocha tofauti katika timu zote nilizochezea.

SWALI: Pamoja na kuipenda kwako kazi hii ya ukocha, huoni kwamba ni ya lawama, hasa iwapo timu itafanya vibaya ama kushindwa kutimiza malengo yake?

JIBU: Ni kweli kazi ya ukocha ina lawama, cha msingi ni kuwa mvumilivu kwa sababu hakuna kazi ya mteremko. Ni kazi ambayo ninaipenda na ninaujua ugumu wake, hivyo nipo tayari kukabiliana na changamoto zozote nitakazokumbana nazo.
Lengo langu kubwa ni kuinua vipaji vya vijana na kuwaendeleza. Sijaridhika kwa elimu niliyoipata kwa sasa. Nitatafuta wadhamini ili waweze kuniendeleza na kuwa kocha wa ngazi za juu zaidi.

SWALI: Ni kawaida ya mashabiki wa soka nchini kuwatolea lugha chafu makocha timu inapofanya vibaya ama kutolewa kafara na uongozi timu inapofungwa mfululizo. Je, upo tayari kukabiliana na changamoto hizi?

JIBU: Kama nilivyokueleza mwanzo, nipo tayari kwa lolote kwa sababu hii ndiyo kazi niliyoamua kuifanya baada ya kustaafu kucheza soka. Binafsi nimevumilia mengi sana nilipokuwa nikiichezea Yanga, ambayo siwezi kuyataja kwa sababu mimi ni mtu mzima, hivyo nina uwezo wa kuvumilia lolote katika kazi yangu hii mpya.

SWALI: Unazungumziaje kasumba iliyopo sasa ya klabu kubwa na zenye uwezo wa kifedha nchini kupenda kuajiri makocha wa kigeni na kuwadharau makocha wazalendo?

JIBU: Kuajiri kocha wa kigeni sio dhambi kwa sababu wakati mwingine wanasaidia kuongeza ujuzi kwa wachezaji wetu na makocha wazawa. Lakini nadhani wakati umefika kwa viongozi wa klabu kubwa nchini kutoa ajira kwa makocha kwa kuzingatia sifa na uwezo wao badala ya kukimbilia makocha wa kigeni, ambao wamekuwa wakilipwa fedha nyingi, lakini kazi wanayoifanya ni ndogo sana.

Kwa kipindi chote nilichocheza soka, nimekutana na kufundishwa na makocha wengi wa kigeni, hivyo najua uwezo na udhaifu wa baadhi yao. Naweza kusema kwamba, baadhi yao walikuwa wababaishaji. Hivyo ni vyema tuwape nafasi makocha wetu wazawa ya kuonyesha uwezo wao kama zinavyofanya baadhi ya timu za ligi kuu za hapa nchini.

SWALI: Ungependa kutoa mwito gani kwa wanasoka wenzako wa zamani, ambao baada ya kustaafu soka, wamekuwa na maisha magumu na pengine hawana la kufanya?

JIBU: Moja ya sababu zilizonifanya niamue kuchukua mafunzo ya ukocha ni kujiandaa kwa maisha yangu ya baadaye baada ya kuwaona baadhi ya wachezaji waliotutangulia wakihangaika. Na hii ndio sababu iliyonifanya niamue kuendelea na mafunzo ya ngazi za juu zaidi ya ukocha ili niweze kutambulika kama kocha wa kimataifa.

Baadhi ya wakati ninapokutana na wachezaji wenzangu wa zamani, huwa nawashawishi kutafuta kitu cha kufanya baada ya kustaafu soka kwa sababu umaarufu hauwezi kuwasaidia lolote. Tunapaswa kujiandaa kwa maisha yetu ya baadaye.

SWALI: Unadhani umestaafu kucheza soka kwa heshima baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka kadhaa?

JIBU: Mwanamichezo yoyote aliyeipatia sifa klabu na nchi yake, anapaswa kuwa na malengo ikiwa ni pamoja na kustaafu akiwa bado na heshima badala ya kusubiri kudhalilishwa. Nimeamua kustaafu soka nikiwa bado nina uwezo, lakini nimeamua kutoa nafasi kwa vijana chipukizi kuonyesha uwezo wao. Uamuzi nilioufanya unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na wachezaji wengine.

SWALI: Unao ushauri wowote kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu wanasoka wa zamani?

JIBU: Naishauri TFF iwasaidie wanasoka wa zamani kupata mafunzo ya ukocha ili waweze kuendelea kutoa mchango wao katika kuinua mchezo huu. Na ni vyema makocha hawa watumike kufundisha timu za vijana kwa lengo la kuibua vipaji vyao na kuwaendeleza.

SWALI: Unapenda kuwaeleza kitu gani viongozi wetu wa soka hapa nchini?

JIBU: Wanapaswa kuweka mbele zaidi maslahi ya wachezaji badala ya kuweka mbele maslahi yao binafsi. Wakumbuke kuwa, wachezaji ndio wanaovuja jasho uwanjani, hivyo wanapaswa kuthaminiwa kwa kulipwa haki zao zote na kwa wakati pasipo kudhulumiwa.

Napenda pia kuwashauri viongozi wa soka nchini, wawakatie bima wachezaji wao ili wawe na kinga baada ya kuumia, badala ya ilivyo sasa, ambapo wachezaji wengi hawana bima, hivyo wanapoumia uwanjani, hakuna wa kuwatibia na viongozi wamekuwa wakiwatelekeza.

Vilevile nawashauri viongozi wa klabu za ligi kuu na zinginezo, kuwaingiza wachezaji wao kwenye mifuko ya pensheni ili waweze kuchangia na kunufaika na makato yao baada ya kustaafu soka.

OMOTOLA APINGA NDOA ZA UTOTONILAGOS, Nigeria
MWANAMAMA nyota katika uigizaji wa filamu wa Nollywood, Omotola Jalade ametaka kusiwepo kipengele kinachoruhusu ndoa za utotoni kwenye katiba ya nchi hiyo.
Akizungumza wakati wa shindano la urembo la MBGN lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini hapa, Omotola alisema anapinga ndoa hizo za utotoni kwa watoto wa kike.
Omotola ameelezea msimamo wake huo wakati ambapo serikali ya nchi hiyo iko katika mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo.
Mwanadada huyo amewataka maseneta wa Nigeria kutopiga kura za kuunga mkono kipengele kinachohusu ndoa hizo.
Omotola alisema atashangaa iwapo maseneta wa Nigeria hawatapitisha sheria, itakayohakikisha kwamba, kila mtoto anakuwa na haki ya kwenda shule kupata elimu.
"Idadi kubwa ya watoto hivi sasa wapo mitaani wakiomba, kunyanyaswa na kubakwa ama kuolewa na wanaume, ambao wanapaswa kuwalinda. Nani anayewalinda watoto wa Nigeria? Je, tusubiri Milala kabla ya kuchukua hatua? Je, tunapaswa kuondoa tangazo la tahadhari kwenye filamu zetu linalosema, 'Haipaswi kutazamwa na watoto wa chini ya miaka 18?" Alihoji.
Mwanamama huyo mwenye watoto wanne ametaka watoto wa kike wa Nigeria wawe na haki ya kupata elimu, kufurahia maisha ya utoto na kuwa na uamuzi juu ya nani anayepaswa kufunga naye ndoa na lini.
"Napinga ndoa za utotoni na mswada wa baraza la seneti unaotaka kuidhinishwa kwa ndoa hizo Nigeria,"alisema.

OGE OGOYE ASHUSHA GHOROFALAGOS, Nigeria
MWANADADA Oge Okoye amedhihirisha kwamba filamu zinalipa baada ya kushusha mjengo wa ghorofa katika moja ya mitaa ya Jiji la Lagos.
Mwigizaji huyo machachari wa Nigeria sasa ameamua kula 'kuku kwa mrija' baada ya kuitumikia fani hiyo kwa miaka mingi na kwa mafanikio makubwa.
Oge, ambaye amekuwa akicheza filamu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, ameshusha mjengo huo kwa kutumia mamilioni ya naira za Nigeria.
Hata hivyo, bado ujenzi wa ghorofa hilo haujakamilika, lakini tayari kumeshawekwa mageti ya vyuma.
Baadhi ya wadau wa fani ya filamu nchini Nigeria, wamempongeza mwanadada huyo kwa uamuzi wake huo wa kujenga nyumba hiyo ya  ghorofa kwa vile waigizaji wenzake wengi wameshindwa kufikia hatua hiyo.
Kwa mujibu wa wadau hao, wacheza filamu wengi wa nchi hiyo wamekuwa wakiishi nyumba za kupanga na kuishia kununua magari ya kifahari.

GENEVIENE ANASA KIMAPENZI KWA MENSAHLAGOS, Nigeria

MCHEZA filamu nyota wa kike wa Nigeria, Gevenieve Nnaji huenda akafunga ndoa na mfanyabiashara wa Ghana, Mathew Mensah.

Genevieve na Mensah wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara na baadhi ya watu walio karibu nao wameeleza kuwa, wapo katika mapenzi mazito.

Marafiki wa Genevieve wameeleza kuwa, mwanadada huyo, ambaye ni mama wa mtoto mmoja, anaonekana kulifurahia penzi hilo.

Awali, Genevieve alikuwa akihusishwa kimapenzi na mwanamuziki D'banj, lakini wote wawili walikuwa wakizikana taarifa hizo na kudai kuwa, uhusiano wao ulikuwa wa kawaida.

Alipoulizwa na rafiki zake kuhusu uhusiano uliopo kati yake na Mensah, Genevieve alidai kuwa ni wa kawaida, lakini wadadisi wa mambo wanahisi kuwa, kuna kitu kingine zaidi kinachoendelea kati yao.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa Genevieve, mwanadada huyo amekuwa akilitaja mara kwa mara jina la Mensah katika mazungumzo yake ya kila siku.

Mensah ni miongoni mwa marafiki wa Genevieve waliohudhuria sherehe ya mcheza filamu huyo kufikisha umri wa miaka 33 iliyofanyika hivi karibuni mjini Lagos.

"Upo uwezekano mkubwa kwa Genevieve kufunga ndoa na Mensah kabla ya mwisho wa mwaka huu. Inawezekana ikawa Desemba," kilisema chanzo cha habari.

Wakati huo huo, Genevieve hivi karibuni alionekana akiwa mjini Beijing, China alikokwenda kwa ziara maalumu.

Mwanadada huyo mwenye mvuto, aliyecheza filamu zaidi ya 80 za Kinigeria, alionekana akitembelea madumba mbalimbali yanayouza majani ya chai na viwanda vya nguo.

Tuesday, July 23, 2013

TUMEJIANDAA KUIKABILI UGANDA-KIM


 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda kwenye mechi ya marudiano ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayochezwa Jumamosi jijini Kampala.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Kim amesema tangu kikosi chake kimeingia kambini Julai 14 mwaka huu, wachezaji wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mazoezi na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
 
“Uganda ni timu bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Mechi itakuwa ngumu, tunaamini tunakwenda kufanya vizuri. Tayari tunayo mikakati kwa ajili ya mechi hiyo, tunakwenda kuikamilisha Kampala,” amesema Kim.
 
Hata hivyo, Kim amesema licha ya mwitikio mzuri wa wachezaji kwenye mazoezi lakini wanakabiliwa na changamoto ya wengi wa wachezaji kuwa wamefunga wakati wachezaji wanapokuwa kambini wanatakiwa kula, kunywa na kupumzika.
 
“Hiki ni kipindi kigumu kwa mpira wa miguu, na suala la kufunga ni la kiimani ambapo hatuwezi kuwazuia wachezaji kufunga. Karibu nusu ya wachezaji wanafunga, hii ni changamoto ambayo tunaiheshimu,” amesema Kim na kuongeza kuwa ni wazi kikosi chake cha kwanza kitakuwa na mabadiliko baada ya beki Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio nchini Uholanzi.
 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaondoka Mwanza kesho (Julai 24 mwaka huu) saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir na kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8.15 mchana.
 
Wachezaji waliomo kwenye msafara huo ni makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.
 
Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Monday, July 22, 2013

RATIBA YA LIGI KUU BARA 2013/2014 24.08.2013 1 YOUNG AFRICANS VS ASHANTI UNITED NATIONAL STADIUM DAR
 24.08.2013 2 MTIBWA SUGAR VS AZAM FC MANUNGU MOROGORO
 24.08.2013 3 JKT OLJORO VS COASTAL UNION SH. AMRI ABEID ARUSHA
 24.08.2013 4 MGAMBO JKT VS JKT RUVU  MKWAKWANI TANGA
 24.08.2013 5 RHINO RANGERS VS  SIMBA SC A.H. MWINYI TABORA
 24.08.2013 6 MBEYA CITY VS KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA
 24.08.2013 7 RUVU SHOOTINGS VS TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI
    
 28.08.2013 8 MTIBWA SUGAR VS KAGERA SUGAR MANUNGU MOROGORO
 28.08.2013 9 RHINO RANGERS VS AZAM FC A.H. MWINYI TABORA
 28.08.2013 10 JKT RUVU VS TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI
 28.08.2013 11 MBEYA CITY VS RUVU SHOOTINGS SOKOINE MBEYA
 28.08.2013 12 MGAMBO JKT VS ASHANTI UNITED MKWAKWANI TANGA
 28.08.2013 13 JKT OLJORO VS SIMBA SC SH. AMRI ABEID ARUSHA
 28.08.2013 14 YOUNG AFRICANS VS COASTAL UNION NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
(29.August-09.Sept. National Team Camp for WCQ against Gambia away)    
14.09.2013 15 SIMBA SC VS MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
14.09.2013 16 COASTAL UNION VS TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA
14.09.2013 17 RUVU SHOOTINGS VS MGAMBO JKT MABATINI  PWANI
14.09.2013 18 JKT OLJORO VS RHINO RANGERS SH. AMRI ABEID ARUSHA
14.09.2013 19 MBEYA CITY VS YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA
14.09.2013 20 KAGERA SUGAR VS AZAM FC KAITABA KAGERA
14.09.2013 21 ASHANTI UNITED VS JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
    
18.09.2013 22 TANZANIA PRISONS VS YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA
18.09.2013 23 SIMBA SC VS MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
18.09.2013 24 KAGERA SUGAR VS  JKT OLJORO KAITABA KAGERA
18.09.2013 25 AZAM FC VS ASHANTI UNITED AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
18.09.2013 26 COASTAL UNION VS RHINO RANGERS MKWAKWANI TANGA
18.09.2013 27 MTIBWA SUGAR VS MBEYA CITY MANUNGU MOROGORO
18.09.2013 28 RUVU SHOOTINGS VS JKT RUVU MABATINI PWANI
    
21.09.2013 29 MGAMBO JKT VS RHINO RANGERS MKWAKWANI  TANGA
21.09.2013 30 TANZANIA PRISONS VS MTIBWA SUGAR SOKOINE MBEYA
22.09.2013 31 JKT RUVU VS JKT OLJORO AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
21.09.2013 32 SIMBA SC VS MBEYA CITY NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
22.09.2013 33 AZAM FC VS YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
21.09.2013 34 KAGERA SUGAR VS ASHANTI UNITED KAITABA KAGERA
22.09.2013 35 COASTAL UNION VS RUVU SHOOTINGS MKWAKWANI  TANGA
    
 28.09.2013 36 YOUNG AFRICANS VS RUVU SHOOTINGS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 28.09.2013 37 RHINO RANGERS VS KAGERA SUGAR A. H. MWINYI TABORA
 29.09.2013 38 ASHANTI UNITED VS MTIBWA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 28.09.2013 39 MBEYA CITY VS COASTAL UNION SOKOINE MBEYA
 28.09.2013 40 MGAMBO JKT VS JKT OLJORO MKWAKWANI TANGA
 29.09.2013 41 JKT RUVU VS SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 29.09.2013 42 TANZANIA PRISONS VS AZAM FC SOKOINE MBEYA
    
 05.10.2013 43 RUVU SHOOTINGS VS SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM
 05.10.2013 44 JKT RUVU VS KAGERA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES  SALAAM
 05.10.2013 45 COASTAL UNION VS AZAM FC MKWAKWANI TANGA
 05.10.2013 46 JKT OLJORO VS MBEYA CITY SH. AMRI ABEID ARUSHA
 25.09.2013 47 RHINO RANGERS VS ASHANTI UNITED A. H. MWINYI TABORA
 06.10.2013 48 MGAMBO JKT  VS TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA
 06.10.2013 49 YOUNG AFRICANS VS MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM
    
09.10.2013 50 RHINO RANGERS VS MBEYA CITY A. H. MWINYI TABORA
09.10.2013 51 JKT OLJORO VS RUVU SHOOTINGS SH. AMRI ABEID ARUSHA
09.10.2013 52 AZAM FC VS MGAMBO JKT AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
09.10.2013 53 MTIBWA SUGAR VS JKT RUVU MANUNGU MOROGORO
12.10.2013 54 KAGERA SUGAR VS YOUNG AFRICANS KAITABA KAGERA
12.10.2013 55 SIMBA SC VS TANZANIA PRISONS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
13.10.2013 56 ASHANTI UNITED VS COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
    
 13.10.2013 57 RUVU SHOOTINGS VS RHINO RANGERS MABATINI PWANI
 13.10.2013 58 MGAMBO JKT VS MBEYA CITY MKWAKWANI TANGA
 13.10.2013 59 AZAM FC VS JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 13.10.2013 60 MTIBWA SUGAR VS JKT OLJORO MANUNGU MOROGORO
 16.10.2013 61 ASHANTI UNITED VS TANZANIA PRISONS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 19.10.2013 62 KAGERA SUGAR VS COASTAL UNION KAITABA KAGERA
 20.10.2013 63 SIMBA SC  VS YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
    
 19.10.2013 64 JKT OLJORO  VS AZAM FC SH. AMRI ABEID ARUSHA
 19.10.2013 65 MTIBWA SUGAR VS MGAMBO JKT MANUNGU MOROGORO
 19.10.2013 66 MBEYA CITY VS JKT RUVU SOKOINE MBEYA
 19.10.2013 67 ASHANTI UNITED VS RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 23.10.2013 68 COASTAL UNION VS SIMBA SC MKWAKWANI TANGA
 23.10.2013 69 TANZANIA PRISONS VS KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA
 23.10.2013 70 YOUNG AFRICANS VS RHINO RANGERS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
    
 26.10.2013 71 TANZANIA PRISONS VS MBEYA CITY SOKOINE MBEYA
 26.10.2013 72 COASTAL UNION VS MTIBWA SUGAR MKWAKWANI TANGA
 26.10.2013 73 JKT OLJORO VS ASHANTI UNITED SH. AMRI ABEID ARUSHA
 26.10.2013 74 YOUNG AFRICANS VS MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 27.10.2013 75 RUVU SHOOTINGS VS KAGERA SUGAR MABATINI PWANI
 27.10.2013 76 SIMBA SC VS AZAM FC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 27.10.2013 77 RHINO RANGERS VS JKT RUVU A. H. MWINYI TABORA
    
 30.10.2013 78 MGAMBO JKT  VS COASTAL UNION MKWAKWANI TANGA
 30.10.2013 79 TANZANIA PRISONS VS JKT OLJORO SOKOINE  MBEYA
 30.10.2013 80 AZAM FC VS RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 30.10.2013 81 SIMBA SC VS KAGERA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 30.10.2013 82 MTIBWA SUGAR VS RHINO RANGERS MANUNGU MOROGORO
 30.10.2013 83 MBEYA CITY VS ASHANTI UNITED SOKOINE  MBEYA
 31.10.2013 84 JKT RUVU VS YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
    
 02.11.2013 85 JKT RUVU VS COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 02.11.2013 86 ASHANTI UNITED VS SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
 03.11.2013 87 KAGERA SUGAR VS MGAMBO JKT KAITABA KAGERA
 03.11.2013 88 AZAM FC VS MBEYA CITY AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
 03.11.2013 89 RHINO RANGERS VS TANZANIA PRISONS A. H. MWINYI TABORA
 03.11.2013 90 RUVU SHOOTINGS VS MTIBWA SUGAR MABATINI PWANI
 03.11.2013 91 YOUNG AFRICANS VS JKT OLJORO NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM

TAIFA STARS KWENDA UGANDA JUMATANO


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya Precision Air, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.

Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.

SIMBA, YANGA DIMBANI OKTOBA 20 LIGI KUU YA BARA


HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, ambayo inaonyesha kuwa, timu kongwe za Simba na Yanga zitakutana Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo iliyotolewa leo inaonyesha kuwa, mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kati ya mabingwa, Yanga na washindi wa pili msimu uliopita, Azam itapigwa Agosti 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kushuka dimbani katika miji saba tofauti.

Katika mechi hizo za ufunguzi,  Yanga itacheza na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro) na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- attached).

Sunday, July 21, 2013

YANGA CHUPUCHUPU KWA URAWachezaji wa URA wakishangilia bao lao la pili dhidi ya Yanga leo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya Jerry Tegete kusawazisha dakika ya 90. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto)

BAO lililofungwa na mshambuliaji Jerry Tegete dakika ya 90 leo limeinusuru Yanga kuadhiriwa na URA ya Uganda baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 2-2 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0. Bao hilo la kuongoza lilifungwa na Litumba Yayo dakika ya 42.

Litumba ndiye aliyeizamisha Simba katika mechi ya jana baada ya kuifungia URA mabao yote mawili ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Bao la pili la URA lilifungwa tena na Litumba dakika ya 61 kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililowapita mabeki wa Yanga na kipa Deogratius Munishi 'Dida' aliyejaribu kuupangua mpira, lakini ulimshinda nguvu.

Mrundi, Didier Kavumbagu aliifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 66 alipounganisha wavuni kwa kichwa krosi maridadi iliyopigwa na Juma Abdul kutoka pembeni ya uwanja.

Tegete aliisawazishia Yanga baada ya kuwazidi nguvu na mbio mabeki wawili wa URA pamoja na kipa wao, Yassin Mugabi.

Mrundi Didier Kavumbangu alianza dakika ya 66 akiunganisha krosi ya beki Juma Abdul kabla ya Tegete kusawazisha dakika ya 90 baada ya kuwazidi nguvu na maarifa kipa wa URA, Yassin Mugabi na mabeki wawili.

WABUKINI KUZICHEZESHA STARS NA UGANDAShirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Madagascar kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

Waamuzi wataongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official).

Kamishna wa mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.

Mechi hiyo namba 38 itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Taifa Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN mwakani nchini Afrika Kusini.

SIMBA HOI KWA URAMshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuifungia Simba bao la kuongoza katika mechi ya kimatifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. URA ilishinda 2-1. (Picha na Bin Zubeiry)

SIMBA jana ilipigwa mweleka wa mabao 2-1 na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na kupokea kichapo hicho, vijana wa Simba, ambao wengi ni wapya walionyesha kiwango cha juu cha soka, hasa kipindi cha kwanza na kuwafanya washangiliwe na mashabiki wao.

Iliwachukua Simba dakika saba kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake mpya, Betram Mwombeki kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Ramadhani Singano 'Messi'. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

URA ilisawazisha dakika ya 60 kwa bao lililofungwa na Lusimba Yayi baada ya mabeki wa Simba kuzubaa kuokoa shambulizi kwenye lango lao.

Simba ilipata pigo dakika ya 65 baada ya Mwombeki kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko beki, Jonathan Mugaba.

Pengo hilo liliiwezesha URA kupata bao la pili dakika ya 75 lililofungwa na Yayi baada ya kupokea pasi kutoka kwa Derick Walulya, aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi.

URA inatarajiwa kushuka tena dimbani leo kucheza na Yanga kwenye uwanja huo.

Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Rahim Juma/Sino Augustino, Samuel Ssenkoom, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Miraj Adam, William Lucian, Betram Mombeki, Zahor Pazi/Twaha Ibrahim na Marcel Boniventura.

Friday, July 19, 2013

ENTER THE DRAGON YATIMIZA MIAKA 40, MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU BRUCE LEEBehind every great man is a great woman, and for martial arts legend Bruce Lee, that woman was Linda Emery, who married her dashing gongfu teacher in the mid-'60s. Linda and Bruce were husband and wife until July 20, 1973, when Bruce died of cerebral edema at the age of 32 ... just six days before the Hong Kong release of what many consider to be his greatest cinematic achievement, "Enter the Dragon."
Upon the 40-year anniversary of both the premiere of "Enter the Dragon" (which is now available in a 40th Anniversary Edition Blu-ray) and the untimely death of its star, we spoke with Linda Lee Cadwell (who has since remarried) about her late husband's legacy and how his abilities and philosophies have inspired countless others to reach their full potential — and beyond.
BRYAN ENK: Does it feel like 40 years have passed since "Enter the Dragon" was first released?
LINDA LEE CADWELL: [Laughs] No, I was actually quite shocked when I realized, "40 years?!" It's a lifetime, to be sure. And like you, a lot of the people who admire "Enter the Dragon" and Bruce were not even born at the time when he was alive. That does put it in perspective and makes it seem like 40 years have passed.
BE: "Enter the Dragon" is considered to be one of the best martial arts films of all time, if not the best. What do you feel have been the most influential aspects of the film over the past four decades and what has made it stand the test of time so well?
LLC: Well it certainly is the gold standard of martial arts films and certainly inspired the genre altogether. I think it's quite obvious really that the outstanding thing about "Enter the Dragon" was Bruce. The storyline is really nothing spectacular and the technical qualities are fine, but the thing that makes it really stand out is of course Bruce. And the parts of it that people admire so much are on different levels — a person can look at "Enter the Dragon" and admire the physicality of it, the combat, the choreography inspired and performed by Bruce, or they can take it a step further and see that there are bits of philosophical wisdom in it, also inspired by Bruce.
BE: Do you have a particularly good behind-the-scenes memory from when the film was in production, something that happened on or off the set?
LLC: Oh my, yes! Bruce had been wanting to do a Hong Kong/American co-production for a long time, that had been his goal when he first went to Hong Kong to make films, that one day the filmmakers in the West would realize his value and talent and would be ready to do something with him. So it was an important landmark for him and it was important for him that the film be a success. So he put his heart and soul in it, and he was very insistent on some changes to the script. Some people have made the comment that he was very nervous to start the film, that he was on the edge of a nervous breakdown because he was so uptight about the film and making sure it was a success but that was not really the case — he just had some very important things to say about the script and how he wanted the film to be and very insistent on some changes. And I must say that in light of 40 years and we're still looking at this movie that he was right, and it's because of Bruce and his insisting on doing certain things and adding certain parts to the film that it's been such a success for four decades.
BE: My favorite part of the film is the "Hall of Mirrors" scene. It's a terrific sequence — the choreography, the building tension and there's something truly iconic about the imagery of the bloody scratches on Bruce's chest. Do you have a favorite scene from the film?
LLC: Well, of course all the combat scenes are spectacular and unmatched over all these years, but my favorite parts of the film are the more philosophical points that Bruce brings to the picture. For instance, when he's talking to the young boy and teaching him — that kind of thing makes the film more than an adventure and a "violent film," it gives it more substance.
BE: How did you and Bruce first meet?
Linda Lee, Brandon Lee, and Bruce Lee, circa 1970 (Photo: Everett)LLC: [Laughs] It's a fun story, actually! I was a senior in high school in Seattle, Washington at Garfield High School. And Bruce used to come to my school, he was five years older and a student of Philosophy at the University of Washington, he was friends with the philosophy teacher at my high school. So he would come to my high school to give lectures on Chinese philosophy; I was not in that class but I can tell you that every girl at my school knew when Bruce Lee was in the house because he was so dashing and so handsome. And one of my girlfriends who happened to be Chinese was taking gongfu lessons from him. And so the summer after I graduated from high school she talked me into taking gongfu lessons with Bruce, so that's how we first met — I was his student and it wasn't long before I was more interested in the teacher than the martial art, though I continued to do it for quite a while. [Laughs]
BE: Bruce is known for founding a martial arts practice and philosophy known as Jeet Kune Do. How would you describe the basic fundamentals of that?
LLC: Well, Bruce would never have described it as a "system," because a "system" is an organization of certain rules and his way of martial arts did not have any set rules — it is what is best for the individual person who is learning it. There was an aura of just responding to what "is" in martial arts, so you would not have a particular set of movements in response to, say, an attack — like in some forms of karate it's like "Well, I will punch in a certain way, I will do this or that in certain sequence." Bruce's art was not like that — it flowed, like he often said, like water flows and can fit into any container, it flowed to fit into any situation that was presented. So that's why he called it his "way" of martial arts, not a "system" of martial arts.
There's a great deal more to it as well, and there are fundamentals to it so that it can be carried on for generations, as it is now. But it's also a way of personal growth, to learn more about yourself — as Bruce used to say, all knowledge is really self-knowledge, you learn more about yourself and how to fit into a variety of situations. So, in a nutshell, that's a way of describing it.
BE: Do you have a particularly good memory involving a fan of Bruce's, either an encounter with a fan or a story that a fan told about Bruce?
LLC: Actually, there are so many that I can lump them all into one person, in a way. [Laughs] I've received letters over the years and had personal acquaintance with so many people who have told me how they're truly so inspired by Bruce. And most of the time, especially after the passing of 40 years, it's because of a wanting to model Bruce as a way of life, in a way of improving their own lives. So not so much "Well, I want to be a martial artist" or "I want to learn how to beat up people" — I think many years ago that was the first thing that impressed people, his fighting ability, but I think after all these years people have discovered there were many more layers to Bruce and he was a person of great depth.
And he did an immense amount of writing, which we are blessed today to still have and has been reproduced a number of times in different forms and I think people use that as an inspiration to improve their own lives.
BE: The 1993 film "Dragon: The Bruce Lee Story" is mostly based on your 1975 book, "Bruce Lee: The Man Only I Knew." How do you feel about the film — was it a good adaptation or was it missing something?
LLC: I have mixed feelings about the film. On the good side I think it hit on the high points of Bruce's life, the turning points, you might say. For instance, when he hurt his back and then he was laid up for six months, in bed a lot of the time, unable to be his usual physical self -- the doctors told him he would be unable to ever do gongfu again and all this stuff. That was certainly a turning point in his life, though the injury did not happen in the way they showed it in the film — they felt they had to make it more dramatic. But the point is he hurt his back and he used that time, the six months or more that he was laid up, to produce most of his writings — the philosophical writings about his method of combat, all kinds of things.
So the film took some liberties, it changed some facts, it had a mythical figure in it that I would not have agreed with but that a person can view on different levels. So there were good things and there were some not so good things and I hope that some day a really wonderful film is made about Bruce.
BE: What are you dedicating your time to these days?
LLC: I have a wonderful life going on. I have a great husband named Bruce Cadwell, I live in Idaho, and between us we have nine grandchildren; I have one grandchild, my daughter's daughter who is ten years old and I like to spend a lot of time with her.
Actually, you know, my daughter Shannon has taken over the role of perpetuating and preserving her father's legacy, so I just show up at certain times and of course I'm interested in that goal as well and we have larger goals of some day wanting to build the Bruce Lee Action Museum and people in Seattle are very interested in sponsoring that. It's a long-term project and that's what we're aiming at in the long run.

MKUTANO MKUU SIMBA LEO, INAKIPIGA NA URA JIONI U/TAIFAMWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, anawakaribisha wanachama wote wa Simba katika Mkutano Mkuu wa Wanachama utakaofanyika kesho katika bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ni wa kawaida wa kila mwaka na unaendeleza utaratibu wa uongozi wa Alhaji Rage kufanya mikutano kama hiyo kwa kadri Katiba ya klabu inavyotaka.
Ikumbukwe kuwa katika miaka ya nyuma, kuna kipindi klabu haikuwa ikifanya mikutano kama hii kwa kipindi kirefu na hivyo huu ni utaratibu mwafaka katika kuendeleza klabu ya SIMBA.
Kwa mwaliko huu, Mwenyekiti anawataka wanachama wote walio hai kuhudhuria mkutano huo na KLABU INASISITIZA KWAMBA WANACHAMA AMBAO HAWATAKUWA HAI HADI ASUBUHI YA SIKU YA MKUTANO HAWATARUHUSIWA KUINGIA MKUTANONI. HII MAANA YAKE NI KWAMBA WANACHAMA HAWARUHUSIWI KULIPIA KADI ZAO KWENYE ENEO LA MKUTANO SIKU YA MKUTANO.
Mkutano unatarajiwa kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama wote wanaombwa kujali muda.
Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utapokea na kujadili Ripoti ya Mapato na Matumizi ya Klabu kwa mwaka ulioisha kama ilivyokaguliwa na wakaguzi wa hesabu, kupokea taarifa ya Mpango Mkakati wa Klabu (Strategic Plan) ulioandaliwa na maprofesa wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT).
MECHI YA SIMBA NA URA
TIMU za Simba na URA ya Uganda zimewasili jijini Dar es Salaam tayari kabisa kwa pambano la kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa Simba kucheza kwenye uwanja huo tangu kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania na ikiwa imetoka katika ziara ya mafanikio ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.
URA imewasili jijini jana ikiwa na msafara wa wachezaji 23 na viongozi sita. Baadhi ya wachezaji maarufu waliokuja na timu hiyo ni Derick Walulya, George Owino na Musa Doca.
Pambano hilo litaanza majira ya saa kumi kamili jioni.
MSIBA
KWA niaba ya Kamati ya Utendaji ya Simba, Wanachama na Wapenzi wa klabu, Mhe; Rag anatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Juma Urongo aliyefariki dunia asubuhi ya leo na kutarajiwa kuzikwa leo jioni huko Tandika jijini Dar es Salaam.
Mzee Urongo alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wazee la Simba na ni miongoni mwa kizazi cha wazee walioanza kuishabikia klabu tangu ikiitwa Sunderland.
Rage amesema binafsi atakosa sana busara, ushauri na maelekezo yam zee huyo ambaye alikuwa shabiki wa Simba katika nyakati nzuri na mbaya.
Mungu na aiweke mahali pema roho ya marehemu Juma Urongo.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

LYATTO AAGA RASMI TFFMAELEZO YA SHUKURANI YA MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF - KWA VIONGOZI NA WADAU WA SOKA NCHINI


1.                   Kama wote tunavyofahamu jana uongozi wangu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulifikia tamati kama mlivyotangaziwa na Rais wa TFF. Kwa heshima kubwa naomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na wadau wa soka kwa ushirikiano mkubwa nilioupata kutoka kwao wakati nikitekeleza majukumu mbalimbali ya TFF.

2.                   Kwa kushirikiana na viongozi wa mpira wa miguu katika TFF na mikoa yote Tanzania Bara, pamoja na wadau wa soka, nimepata fursa kulitumikia soka la nchi yetu kwa nafasi mbalimbali. Kwa pamoja tumetekeleza majukumu ya ujenzi wa misingi ya uongozi bora katika TFF na wanachama wake.

3.                   Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF:

(i)             kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, (Jan 2005 - Jan 2007). Nawashukuru pia wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mhe. Said El-Maamry kwa kunichagua kuwa Katibu wa Kamati hiyo. Ushirikiano mlionipatia ulioniwezesha kulitumikia taifa katika soka na kwa pamoja kurejesha nidhamu kwa kiwango kikubwa.

(ii)           kwa kuniteua kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu, iliyochunguza mkasa wa timu yetu ya Taifa ya wachezaji wa umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) mwezi Juni 2005. Nawashukuru wajumbe wa kamati  hiyo chini ya Dr. Hamad Ndee Mkuu wa Idara ya Michezo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, kwa kunichagua kuwa Katibu wa kamati hiyo iliyoandaa taratibu za mashindano ya vijana  ambazo ni msingi  wa mashindano ya vijana wa umri chini ya miaka 17  hapa nchini.

(iii)          kwa kuniteua kuwa Mjumbe wa Kamati Maalumu iliyotayarisha Programu ya kuendeleza Timu ya Taifa kwa kipindi cha miezi 15 (April 2006 hadi Juni 2007). Progamu iliyochangia Tanzania kiinua kiwango cha ubora wa soka kutoka nafasi ya 165 duniani mwezi Februari 2006 hadi nafasi ya 89 mwezi Desemba 2007.

(iv)         kwa kunipa fursa ya kuwa mjumbe wa Kamati Maalumu ya kuboresha mapato ya TFF mwaka 2009. Nikiwa mjumbe na Katibu wa Kamati hiyo nilipata ushurikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini  na nje ya nchi.  Nina imani kuwa TFF itakamilisha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati na ya wadau wa soka ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia tiketi za elektroniki.

(v)           kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kwa  vipindi viwili; Februari 2009 - Machi 2011 na kuniteua tena kuiongoza Kamati hiyo kwa kipindi cha pili Machi 2011 hadi jana tarehe 18 Julai 2013. Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF kwa imani kubwa iliyoonyesha kwangu na wanakamati wenzangu.
4.                   Nawashukuru wajumbe wote wa wa Mkutano Mkuu wa TFF, kwa ushirikiano mkubwa mliotoa kwangu na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kushiriki kwa amani na utulivu na kuzingatia Katiba za vyama vyenu, Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi na hivyo kufanikisha zoezi la chaguzi za viongozi katika wilaya zote na Mikoa yote ya Tanzania Bara na hivyo kuwezesha kuwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu, ambao  katika kikao chake cha kwanza baada ya chaguzi hizo kimefanya jambo la kihistoria kuweka nguzo za  Mwenendo, Maadili  na Miiko ya uongozi wa soka la nchi yetu. Nilifarijika kuwa sehemu ya Mkutano Mkuu huo nikiwa mwalikwa.

5.                   Nawashukuru viongozi na wafanyakazi wote wa Sekretarieti ya TFF, wajumbe wa Kamati zote za TFF, Wajumbe wa Kamati zote za Uchaguzi za wanachama wa TFF na wanachama wao, kwa ushirikiano mkubwa na wa dhati uliowezesha kuwatumikia wadau wa soka kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

6.                   Nawashukuru sana wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ushirikiano niliopata kutoka kwao kwa muda tuliofanya kazi pamoja. Si jambo rahisi kusimamia chaguzi za mikoa yote na klabu zenye wanachama za Ligi Kuu, hata hivyo kwa kushirikiana na wadau mbalimali wa soka ambao nachukua fursa hii kuwashukuru, kwa pamoja tumeweza kutimiza jukumu hilo kikamilifu. 

7.                   Nawashukuru sana Wandishi na Wahariri wa habari za michezo na pia Wahariri Watendaji wa vyombo vya habari, kwa ushirikiano mzuri nanyi, ushirikiano na uhusiano wa uwazi ambao haukuwa na mikwaruzo ya aina yoyote kwa kipindi chote (Jan 2005-Jul 2013) tulichoshirikiana kwa pamoja kulitumikia soka la nchi yetu.

8.                   Namshukuru sana Rais wa TFF Ndg. Leodegar Tenga kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na kwa wanakamati niliokuwa nao katika kutekeleza majukumu ya umma. Miaka ishirini na tisa (29) iliyopita nilipata fursa ya kufanya kazi ya mpira miguu kwa mara ya kwanza na Ndg. Tenga, nikiwa nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Desemba 1984, wakati Ndg. Tenga alipojitolea kuifundisha timu ya Chuo Kikuu cha DSM. Tangu wakati huo hadi sasa imani  na  ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya umma niliopata kutoka kwa Ndg. Tenga haujawai kutetereka hata kwa siku moja. Ni faraja kubwa kwangu kufanya kazi hizi za umma chini ya kiongozi anayeheshimika na kuaminika na wadau wa soka hapa nchini, Afrika Mashariki na Kati, Afrika na familia ya soka Duniani kwa ujumla.

9.                   Mwisho, kwa viongozi na wadau wote wa mpira wa miguu, nawashukuru na nawatakia kheri, baraka  na mafanikio katika Uchaguzi Mkuu wa TFF na  ujenzi wa  soka la nchi yetu..

Asanteni.
 Deogratias J. Lyatto
19 Julai 2013, Dar es salaam, Tanzania.

Thursday, July 18, 2013

TFF YAFUMUA KAMATI ZAKEJAJI Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto wataongoza kamati muhimu za za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoundwa baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa TFF Leodegar C. Tenga alitangaza jana.

Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa za Nidhamu na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.

Rais Tenga alisema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kikatiba kina jukumu la kuunda Kamati Ndogo za TFF na vyombo vya maamuzi.

“Tulitaka tuwe na watu solid (imara) na makini ambao watatuhakikishia tunakwenda vyema,” alisema Tenga akizungumzia uteuzi huo ambao unahitimisha mchakato wa mageuzi kwenye Shirikisho baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika mwezi Februari kusimamishwa kutokana na baadhi ya wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda FIFA.

Katika kumaliza tatizo hilo, FIFA ilituma ujumbe wake kusikiliza walalamikaji na watu wengine na baadaye kuagiza kuundwa kwa Kamati za Maadili na kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa TFF kwa ajili ya kuingiza vyombo hivyo kwenye katiba kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Tumezingatia pia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao walitaka kamati ziwe na majaji... lakini si rahisi kupata seating judges (majaji walio kazini) ndio maana tunawashukuru wale waliotuambia kuwa wako tayari kutusaidia.

“Tumetafuta majaji na mawakili waandamizi ambao tunaamini watatuhakikishia haki inatendeka na inaonekana inatendeka,” alisema Tenga na kuongeza kuwa pia walizingatia maombi ya wajumbe wengine watatu ambao walitaka kupumzika, akiwataja kuwa ni Deo Lyatto, Sylvester Faya na Idd Mtiginjollah.

Alisema kutokana na mfumo huo mpya, mambo yote yanayohusu masuala ya ndani ya uwanja sasa yatashughulikiwa na Kamati ya Nidhamu, wakati yale ya nje ya uwanja, ambayo yanawahusu viongozi na wanafamilia ya mpira wa miguu kwa ujumla, yatashughulikiwa na Kamati za Maadili.

Tenga alisema mabadiliko hayo pia yamegusa kamati nyingine mbili, yaani Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Uchaguzi ambayo sasa itaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni

Jaji Ihema ataongoza Kamati ya Rufaa za Maadili akisaidiwa na mwanasheria mwingine mwandamizi, Victoria Makani, huku Bi. Mguto, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza vyombo vya vya maamuzi ataongoza Kamati ya Maadili akisaidiwa na makamu wake Francis Kabwe, ambaye Msajili wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi huo, baadhi ya wajumbe wamehamishwa kutoka kamati moja hadi nyingine. Mhe. Murtaza Mangungu, ambaye awali alikuwa Kamati ya Rufaa za Uchaguzi, sasa ataingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili; Kamanda Mohamed Mpinga na Prof Madundo Mtambo wamehamishwa kutoka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi kwenda Kamati ya Maadili.

Wajumbe wapya kwenye Kamati hizo ni pamoja na kocha wa zamani wa Taifa Stars na Reli ya Morogoro, Mshindo Msolla na Kamanda Mstaafu Jamal Rwambow wanaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; mwanasheria maarufu Evodi Mmanda anaingia kwenye Kamati ya Maadili; mwanasheria mwandamizi Mustapha Kambona ambaye anaingia kwenye Kamati ya Nidhamu; Mhe. Mohamed Misanga ambaye anaingia kwenye Kamati ya Maadili na Kanali Iddi Kipingu, ambaye anasifika kwa kuendesha soka la vijana, anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Nidhamu.

Pia Mwanasheria Anne Steven Marealle anakuwa mjumbe kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi; Yohane Masale (Rufaa za Uchaguzi), Allen Kasamala (Rufaa za Uchaguzi);  Francis Kiwanga ambaye pia aningia kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi na mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau ambaye anaingia kwenye Kamati ya Rufaa za Maadili.

Kamati ya Utendaji pia imefanya mabadiliko kwenye Kamati ya Waamuzi ambako mwenyekiti Said Nassoro na katibu Charles Ndagala wa Chama cha Waamuzi wanaingia kwenye kamati hiyo kushika nafasi ya Joan Minja na Riziki Majala.

Wajumbe wa Kamati hizo ni kama ifuatavyo:

Kamati ya Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani (m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza Mangungu.

Kamati ya Maadili: Bi Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod mmanda.

Kamati ya Rufaa za Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo, Ong’wanuhama Kibuta (m/mwenyekiti), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla, ACP Jamal Rwambow.

Kamati ya Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona (m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa na Mohamed Msomali.

Kamati ya Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga (m/mwenyekiti), A. Steven Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala.

Kamati ya Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Kamati ya Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde (m/mwenyekiti), Said Nassoro, Charles Ndagala na Mohamed Nyama.